Posts

JINSI YA KUPIKA MAANDAZI

Image
JINSI YA KUPIKA MAANDAZI LAINI. MAHITAJI YA MAANDAZI 1. Unga - 5 Vikombe. 2. Tui la Nazi zito vugu vugu - 1 ¼ kikombe. 3. Sukari - 3/4 kikombe cha chai. 4. Samli iliyoyayushwa au mafuta - 3 vijiko vya Supu. 5.Hamirah - 2 Vijiko vya Supu. 6. Hiliki - 1/2 Kijiko cha chai. 7. Mafuta ya kukaangia. NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA. 1. Ndani ya kibakuli kidogo, mimina hamira na na vijiko viwili vya kulia vya tui. Weka kando mpaka hamira ianze kufura, kama dakika 5-10. 2. Pasha samli moto: 3. Ndani ya bakuli kubwa au sinia, changanya unga, sukari, iliki na samli ikiwa bado moto moto. 4. Mimina hamira ndani ya mchanganyiko wa unga. 5. Changanya na ukande huku ukitumia lile tui la nazi. Tui likipungua unaweza ukaongeza maziwa. 6. Kanda unga mpaka uwe laini. 7. Kata madonge *12 au 15 uyaweke kwenye baraza iliyonyunyiziwa unga na uyafunike ili yapate kufura na yasikauke. *Ukipenda maandazi manene fanya madonge 12. Ukipenda mepesi fanya madonge 15. 8. Madonge yakifura, ...

JINSI YA KUPIKA DAGAA WATAMU ZAIDI

Image
🥕🧅Jifunze Jinsi Ya Kupika roast la Dagaa mwanza Watamu 🥕🧅 🥕🧅 MAHITAJI 🥕🧅 1️⃣ Dagaa 2️⃣ Limao 3️⃣ Karoti 4️⃣ Bamia 5️⃣ Kituunguu Maji 6️⃣ Kitunguu Thoum 7️⃣ Pilipili Mbuzi 8️⃣ Pilipili Manga 9️⃣ Pilipili Boga 1️⃣0️⃣ Nyanya Maji 1️⃣1️⃣ Tomato Paste 🥕🧅 NAMNA 🥕🧅 1️⃣ Toa Vichwa Dagaa Wako 2️⃣ Chemsha Maji Yakichemka Yaipue 3️⃣ Weka Dagaa Kwenye Maji Ya Moto Kwa Dk20 Ili Uchafu Na Mawe Vitoweke 4️⃣ Waoshe Dagaa Vile Wewe Unataka Kama Na Sabuni, Maji Mara8 Ili Mradi Wawe Salama Kwa Utafunaji 5️⃣ Waweke Kwenye Nyungo/ungo Watawanye Waweke Juani Ili Wakauke Kupunguza Matumizi Ya Mafuta Kipindi Unawakaanga 6️⃣ Kipindi Dagaa Wapo Juani Andaa Viungo Vyako Kwa Usafi Na Kuvikata Kwa Mikato Upendayo 🔛 Bamia 🔛 Karoti 🔛 Pilipili Boga 🔛 Pilipili Manga 🔛 Kitunguu Maji 🔛 Kitunguu Thoum 7️⃣ Weka Sufuria Jikoni Tia Mafuta Ya Kula Weka Na Chumvi Kiasi Yakipata Moto Weka Dagaa Zako Kaanga, Wakianza Kuwa Na Rangi Ya Udhur...

JINSI YA KUPIKA MAKANGE YA SAMAKI

Image
Kaributena katika blog yangu uko na International Admin leo naenda kukuletea pishi la Makange ya samaki. Makange ni kati ya mboga rahisi sana kupika na utashangaa kujua kuwa huenda ulikuwa unajichelewesha kuandaa mboga hiyo nyumbani kwako kwa kuogopa vile unayakuta katika hoteli kubwa nyingi na yanavyowekwa kwenye sahani. Huenda umetamani kupika mboga ya makange kwa muda mrefu lakini ukadhani kwa namna ulivyowahi kuiona kwenye sahani, siyo mboga rahisi kupika. TUANZE MAHITAJI ✓ Kitunguu kimoja ✓ Nyanya kubwa 3 ✓ Karoti moja ✓ Hoho moja ✓ Ndimu moja ✓Kitunguu saumu na tangawizi iliyosagwa kijiko kimoja (vyote kwa pamoja) ✓ Tomato fresh 2 ✓ Chumvi kiasi ✓ Binzari nyembamba na pilipili manga ya unga kijiko kimoja cha chakula ✓ Curry powder kijiko kimoja cha chakula ✓ Binzari ya mchuzi kijiko kimoja cha chai ✓ Soya sauce ya kukoza vijiko 3 vya chakula ✓ Maji robo kikombe ✓ Mafuta ya kupikia vijiko 3-4 ✓ Spice ya samaki kijiko 1 Cha chakula ✓ Samaki mkubwa mmo...

HISTORIA YA SAMIA SULUHU HASSAN

Image
Samia Suluhu Hassan alizaliwa mnamo tarehe 27/01/1960 katika visiwa vya Zanzibar. Alianza elimu ya msingi mnamo 1966-1972 katika shule tofauti tofauti zilizopo Unguja na Pemba yaani Zanzibar. Alianza katika shule ya CHAWAKA (Unguja), Kisha alihamia katika shule ya msingi ZIWANI (Pemba) na alimaliza katika shule ya msingi ya Mahonda. Elimu yake ya sekondari alianza 1973-1976 .Alisoma katika shule mbili, 1973-1975 alisoma katika shule ya sekondari ya Ngambo (Unguja) Kisha mwaka 1976 alihamia shule ya Lumumba (Unguja) ambapo alihitimu elimu ya sekondari. Hakuendelea tena na masomo ya chuo kwa muda huo. Aliajiriwa katika serikali ya Zanzibar Kama mchapishaji ambapo alipanda ngazi na kuwa Afisa mipango mnamo 1987-1988. Samia Suluhu Hassan alijiendeleza kielimu huku akiwa mtumishi wa serikali kwa kusoma kozi fupi mbalimbali Kama vile Sheti ya takwimu kabla ya kujiunga na Taasisi ya Maendeleo na uongozi ya Mzumbe Morogoro ambapo alifanikiwa kuhitimu stashahada ya juu ya utawala...

VITU VYA KUFANYA KARIBIA NA MITIHANI.

Image
Karibu sana,basi leo tuko na namna ya kujiandaa wakati wa kukaribia mitihani ili uweze kufanya vizuri. 1. ACHA UOGA Kuna watu wanaogopa Sana wakikaribia kufanya mitihani na hii hali hupelekea kokosa hali ya kutojiamini na kusoma kwa ku panic. 2. JUA MADA ZOTE ZA KILA SOMO UNALOSOMA. Kuna watu wanaingia kwenye mtihani bila kujua hilo somo Lina mada zipi. Hatakama ukashindwa kujua moja kwa moja kila mada lakini kwa uchache ujue mada inahusu nini. 3. SOMA KWA LENGO (TARGET) Tumia muda mwingi kusoma kile unachokielewa kuliko kukimbiza Kurasa /Slides hata Kama hauelewi. Hii itakufanya ushindwe kujiamini ukiingia katika mtihani kwani kila utakachokutana nacho utakuwa hukijui vizuri unajua juu juu tu. Lakini ukiingia na kitu ambacho umekielewa vizuri ukikutana nacho utakijibu kwa weledi na kukupa hamasa ya kujibu maswali mengine vizuri. 4. SOMA MITIHANI ILIYOPITA (Past Papers) Kusoma mitihani iliyopita hii itakusaidia kukupa muongozo wa maswali yanavokuwa lakini pia ...

VIGEZO VYA KULIPWA YOUTUBE

Image
Karibu sana katika blog yangu Leo naenda kukuletea vigezo vya kulipwa YouTube. Kwanza kabisa mtu yeyote anaweza kumiliki account ya YOUTUBE na akalipwa. Kitendo Cha wewe kuwa na account ya email ya Google (Gmail) tayari inakufanya uwe na YouTube account. YouTube ni mtandao ambao unazidi kushika Kasi na kuingizia kipato watu wengi kila siku. Una uwezo wa kuweka videos zako watu wakaangalia na ukalipwa pia. VITU VYA KUWA NAVYO WAKATI WA KUFUNGUA ACCOUNT YA YOUTUBE 1. Fungua Gmail account katika simu yako. JINSI YA KUFUNGUA GMAIL ACCOUNT ✓ Ingia Google ✓ Andika Gmail sign up ✓ Utaletewa form ya kujaza taarifa zako binafsi ✓ Kisha utakubaliana na masharti ya Gmail kwa kubonyeza kitufe kilichoandikwa Agree baada ya kujaza form yako ✓ Tayari utakuwa na Google account (Gmail) 2. Baada ya kuwa na account ya Google utaingia youtube uta click kwenye icon ya juu kabisa upande wa kulia itakayokuwa inawakilisha Gmail account yako. 3. Utaenda katika my channel 4. Ut...

JINSI YA KUJITENGENEZEA JINA (BRAND) KUPITIA MITANDAO

Image
Kwanza, unatakiwa ujitambue wewe ni Nani na unafanya nini mitandaoni Kisha uje uyafanye yafuatayo: 1. WEKA PROFILE PICTURE (DP) . Watu wengi wanaweka picha za katuni, midoli, maua, wananyama, logo, au picha za watu wengine. Hakuna mtu ambae anavutiwa na vikatuni nakadhalika. Unachotakiwa kufanya ni kuweka professional photo. Professional photo haipigwi mwili mzima, Wala watu hawaweki mapozi. Unaweza kuangalia hapa chini mfano wa professional photo na itapendeza Kama utaipiga na simu au kamera yenye quality. Professional photo huanza kuvuta makini ya mtu na kukufanya uonekane uko makini (serious) na unachokifanya. 2. WEKA ACCOUNT YAKO PUBLIC Kuna watu account zao wanaziweka private Sana Sana Instagram. Kama unataka kufanya biashara au watu wajue unachokifanya usiweke account yako private. Weka Public kila mmoja aweze kuona unachokifanya. 3. TENGENEZA WAFUASI WENYE THAMANI (VALUABLE FOLLOWERS). Kuna watu wanatabia ya ku follow watu hovyohovyo kwa lengo la kujipatia follower...

JINSI YA KUTENGENEZA MANGO PICKLE (CHACHANDU YA EMBE) NYUMBANI

Image
Karibu tena katika darasa letu la mapishi basi leo naenda kukuletea namna ya kuandaa achari ya embe nyumbani unaweza kula kwa ugali au chochote ukipendacho. MAHITAJI. ✓Maembe mabichi (usitumie embe zilizoiva au zilizoanza kuiva) ✓ Pilipili mbichi (kama ukipenda) ✓ Achari masala ✓Masala ya kuwasha ✓ Mafuta ya kupikia ✓ Binzari ya njano (tumeric powder) ✓ Chumvi kiasi. MATAYARISHO. ✓ Osha vizuri embe zako na uzikate Kate saizi uipendayo lakini usimenye maganga (Kata vikonyo cha juu na chini) ✓ Loweka embe zako weka na chumvi kwa muda wa siku mbili au tatu Kisha utazianika kwa siku moja au mbili. (Angalia zisikauke Sana zitaleta ugumu wakati wa kula) ✓ Weka mafuta jikoni mpaka yapate moto Kisha yatoe yaweke pembeni yapoe yawe Kama ulivyoyatoa dukani. ✓Chukua chombo chenye nafasi ya kutosha changanya vitu vyote pamoja na mafuta mpaka vichanganyike vizuri ✓ Kisha anika mchanganyiko wako kwa siku kadhaa ili uive vizuri na hapo utakuwa tayari kwa matumizi...

JINSI YA KUPIKA BIRIANI TAMU YA KUKU

Image
Kaributena katika darasa letu la mapishi basi leo naenda kukuletea namna ya kuandaa biriani nzuri ya kuku. MAHITAJI kuku 1kg Mchele wa basmati/ wakawaida (Hapa nitatumia nusu) Vitunguu maji 1/4 Nyanya zilizosagwa tano Nyanya ya mkebe Vitunguu saumu punje 10 Pilipili za kijani 4 Mafuta 1/4 Mdalasini vijiti 5 Hiliki punje 10 Tangawizi vijiko 2 vya chakula Majani ya nanaa yaliyokatwa kibakuli kidogo 1 Binzari nyembamba kijiko 1 cha chai Chumvi kijiko 1 cha chai Manjano 1/2 kijiko cha chai Zafarani 1/2 kijiko cha chai Kotmiri iliyokatwa 1/4 kikombe Maziwa ya mtindi kikombe 1 Njegere (ukipenda) JINSI YA KUANDAA Loweka mchele w kwa dakika 15 hadi 30 Weka mafuta kwenye sifuria, yakishapata moto kaanga vitunguu maji hadi viwe na rangi ya brown kisha chota vitunguu robotatu ya ulivyovikaangaweka pembeni vingine vibaki kwenye sufuria. Twanga kwa pamoja binzari nyembamba, kitunguu swaumu, tangawizi, nusu ya pilipili na vijiti vya mdalasini, kisha weka robo tatu ya vit...

PILAU TAMU YA NYAMA.

Image
NAFASI ZA SENSA 2022 www.tamisemi.go.tz JIANDAE KUHESABIWA Karibu tena, basi leo International Admin anakuletea namna ya kupika pilau tamu ya nyama. Usiondoke angalia mwanzo mwisho, enjoy! MAHITAJI ✓ Mchele (unaweza kuwa basmati au wakawaida) ✓ Nyama (mbuzi au ng'ombe) ✓ Viazi mbatata kiasi ✓ Unga wa pilau (nimeelekeza katika post ya nyuma hapo namna ya kuandaa) ✓ Chumvi kiasi ✓ Mafuta kiasi ✓ Vitunguu maji vitatu kitunguu swaum kilichopondwa ✓Binzari nyembamba (uzile) uloweke kwenye maji kidogo. . NAMNA YA KUPIKA 1. Chemsha nyama yako mpaka iive itie na chumvi kiasi (Supu iweke pembeni) 2. Kaanga viazi mbatata na viive (visiwe brown) Kisha vitoe vikiwa bado na rangi nyeupe. (Wengine hawakaangi, ila ukikaanga mbatata zako zitakuwa na ladha nzuri zaidi) 3. Kaanga vitunguu maji mpaka viwe brown (angalia visiungue vitabadili ladha ya chakula) 4. Weka mdalasini kaanga pamoja, Kisha weka uzile na hiliki na unga wa pilau kidogo Kish...

JINSI YA KUANDAA VIUNGO VYA PILAU VYENYE HARUFU NZURI.

Image
NAFASI ZA SENSA 2022 www.tamisemi.go.tz JIANDAE KUHESABIWA Karibu kwa mara nyingine ukiwa na International Admin leo nitaenda kukuonesha namna ya kuandaa viungo vya pilau vyenye harufu. Ni rahisi sana, enjoy! MAHITAJI ✓ Mdalasini mzima vijiti vikubwa vitano ✓ Binzari nyembamba kibakuli kidogo kimoja ✓Karafuu kibakuli kidogo kimoja ✓ Pilipili manga kibakuli kidogo kimoja ✓ Hiliki nzima kibakuli kidogo kimoja ✓ Uwatu kibakuli kidogo kimoja ✓Mustard seed kibakuli kidogo kimoja MATAYARISHO 1. Chukua frying pan weka jikoni weka na viungo vyako vyote Kisha koroga kidogo kidogo ili usiviunguze (Moto uwe wa kiasi visiungue) 2. Ukimaliza ipua na viache vipoe 3. Chukua blender ya kusagia viungo na uvisage Kisha vitakuwa tayari kutumiwa (Kama hauna blender chukua kinu kidogo na mchi na uviponde ponde Kisha chekecha kwa kichujio Cha chai, japo itakuchukua mda kidogo) Kama umependezwa na pishi langu la leo weka comment hapo chini au Kama unaswal...

JINSI YA KUPIKA NDIZI MASALA.

Image
NAFASI ZA SENSA 2022 www.tamisemi.go.tz JIANDAE KUHESABIWA Karibu tena katika darasa letu la mapishi mbalimbali ukiwa na mimi International Admin. Basi leo tupo na pishi la ndizi mshale za masala. Enjoy! MAHITAJI ✓ Ndizi mshale . ✓ Binzari ya njano ( Turmeric powder) ✓Nyama ✓ Karoti ✓Njegere ✓ Vitunguu maji ✓ Tangawizi ✓ Kitunguu swaum ✓ Mafuta kiasi ✓ Nazi ✓ Curry Powder MATAYARISHO. 1. Chemsha nyama ikishaiva menya ndizi mshale osha na uziweke. 2. Weka binzari ya njano (Turmeric powder) kijiko kimoja Cha chai weka na chumvi kiasi 3. Weka curry powder kijiko kimoja Cha chakula. 4. Chukua tangawizi na kitunguu swaum vilivyosagwa weka 4. Weka kitunguu maji, njegere na Karoti Kisha koroga taratibu usivunje ndizi acha mpaka ndizi na njegere ziive. 5. Weka tui zito la nazi koroga kidogokidogo mpaka liive (Kama chumvi utaona imepungua unaweza kuongeza kidogo) 6. Ndizi zako zitakuwa tayari kupakuliwa utakunywa na kinywaji chochote ukipen...

MAPISHI YA KUKU SEKELA.

Image
NAFASI ZA SENSA 2022 www.tamisemi.go.tz JIANDAE KUHESABIWA Karibuni sana katika darasa letu zuri la mapishi. Leo tutaangalia namna ya kumtengeneza kuku mtamu wa sekela au wengine wanaita Tandoor Chicken MAHITAJI ✓ Kuku 1Kg.(mpasue kati) ✓Ukwaju 1/2pakti (katika kikombe kimoja Cha maji) ✓kitunguu Swaum (kijiko 1 Cha chakula) ✓Tangawizi (kijiko 1 Cha chakula ) ✓Binzari nyembamba ya unga (uzile) - kijiko 1 Cha chai. ✓Pilipili manga (kijiko 1 Cha chai) ✓Chumvi kiasi ✓Tandoori masala (kijiko 1 Cha chai) NAMNA. ✓ Safisha kuku vizuri Kisha wachuje maji (wengine wanapenda kutoa ngozi) ✓Loweka Ukwaju na maji kikombe kimoja Kisha koroga mpaka urojo uwe mzito Chuja Kama tui la nazi ondoa kokwa Kisha mimina kwenye kuku. ✓weka vitunguu swaum na tangawizi Kisha changanya ✓ weka pilipili manga, uzile na chumvi Kisha changanya vizuri. ✓weka tandoori masala Kisha changanya vizuri na uache Kama dakika 30 ivi viungo vikolee vizuri kisha mpake ...

PESA HUWA ZINAJIFICHA WAPI?

Image
NAFASI ZA SENSA 2022 www.tamisemi.go.tz JIANDAE KUHESABIWA Watu wengi siku hizi tunahangaika kutafuta pesa lakini hatujui pesa zimejificha wapi. Hapa nataka nikuoneshe sehemu tano ambazo pesa hujificha. 1.KIPAJI CHAKO Watu wengi wenye vipaji sasa hivi ndio wanaoingiza pesa ndefu Sana kwa urahisi ndani ya muda mchache na wanahitajika Kila siku. Chukulia mfano. Mkandarasi akatangaza uwepo wake ukumbini kiingilio Tsh.500/= watakuja watu wangapi? Wewe utakwenda? Lakini diamond platnumz akitangaza atakuwepo kwa kiingilio Cha shilingi elfu tatu maelfu ya watu watamiminika. Watu wengi sasa hivi wanalipwa kwa kuhudumia watu wengi mfano Mbwana Samatta akiingia uwanjani maelfu na Malaki ya watu hufurahi hivyo basi anapata pesa nyingi kutokana na watu wengi na kupata balozi mbalimbali. Lakini daktari atahudumia wagonjwa tu waambao kwa siku huenda akahudumia sio zaidi ya mia moja.Hivyo basi hata Kama una taaluma yako lakini bado unatakiwa ukijue kipaji chak...

HISTORIA YA ALIKO DANGOTE.

Image
NAFASI ZA SENSA 2022 www.tamisemi.go.tz JIANDAE KUHESABIWA Aliko Dangote alizaliwa tarehe 10 April 1957 katika mji wa Kano nchini Nigeria. Anatokea katika familia ya kitajiri Sana ya wafanya biashara. Aliko Dangote ni mjuu wa Alhajj Alhassan Dantata mfanya biashara mkubwa na tajiri aliyejishughulisha na mashamba makubwa ya Karanga na alifariki mwaka 1955. Dangote alifanikiwa kuanza elimu na tangu alivokuwa mdogo alionesha kupendelea zaidi biashara na alikuwa akiuza pipi na mishumaa. Elimu yake ya chuo kikuu aliipata nchini Misri katika chuo Cha Al -Azhary University (Cairo- Misri) na alisomea masomo ya biashara. Alipofikisha miaka 20 alisajiri kampuni yake ndogo iliyokuwa inajihusisha na uzalishaji wa Sukari na cement iliyoitwa Dangote Group. Familiaya Dangote ilikuwa na maelewano mazuri na serikali ya Nigeria hivyo basi haikuwa ngumu kwake kupata vibali vya kufungua kampuni na Viwanda. Kama inavyofahamika kupata vibali vya biashara na m...

KATIKA KIJIJI CHA UJASI

NAFASI ZA SENSA 2022 www.tamisemi.go.tz JIANDAE KUHESABIWA SEHEMU YA 3 Daudi na Chausiku waliishi pamoja kwa muda wa miezi mitatu hivi. Siku moja Daudi akawa mwenye kupanga panga nguo zake na vitu vyake. Chausiku alimuona akashindwa kuvumilia. Chausiku: Mbona sikuelewi Daudi unafanya nini ? Daudi: Napanga vitu vyangu nitoroke nimechoka maisha ya hapa siyawezi nahitaji kuwaona ndugu zangu. Chausiku: Ina mana unataka uniache na nani Mimi (kwa huzuni) dada angu amepoteza maisha kwa ajili yako! Daudi: Natambua hilo mpenzi, sitoondoka peke yangu tutatoroka wote. Hivyo basi Chukua dumu la maji lijaze maji ya kunywa kesho alfajiri tutaanza safari. Basi kesho ilipowadia Daudi akavaa nguo zake za kimjini mjini na akamvalisha Chausiku Suruari na T-shirt wakabeba chakula na dumu la maji tayari kwa safari Daudi : Mpenzi wangu umependeza Sana umekuwa Kama madada duu wa mjini. Basi wakaanza kutoroka na asubuhi kukapambazuka huku wakisonga na safari ...

KATIKA KIJIJI CHA UJASI

NAFASI ZA SENSA 2022 www.tamisemi.go.tz JIANDAE KUHESABIWA SEHEMU YA 2 Asubuhi kukakucha basi Chausiku akaandaa mazingira ya kupata kifungua kinywa huku dada yake akisafisha mazingira. Mda wote huo Daudi akimtizama Sana Chausiku kwa mazingatio makubwa. Basi wakanywa chai baada ya hapo Nyaukwama alimtakia kila la heri Daudi katika Safari yake. Kisha Chausiku na Daudi wakaanza safari ya kwenda kwa mfalme Zombi kuomba ruhusa. Walipokuwa wakipita njiani watu walishangaa Sana kumuona Chausiku akiwa na mgeni aliyevaa tofauti kabisa na asili yao. Kila walipopita watu waliitana ishara ya kuwashangaa Sana. Walivofika tu kwa mfalme walimkuta amekaa katika kiti chake Cha enzi. Mfalme Zombi alivowaona tu alichukia ghafla Mfalme: Chausiku! ni upuuzi gani huu unafanya kuniletea mtu aliyevaa vitu vya ajabu ajabu mbele yangu,? Walinzi! mtoeni huyu na haya mavazi yake ya ajabu avae Kama wenzake. Basi Daudi akavuliwa nguo na kuvalishwa Kaniki Kama wengine Kisha yey...

KATIKA KIJIJI CHA UJASI

Image
International Admin WAHUSIKA 1. Chausiku 2. Nyaukwama (Dada wa chausiku) 3. Daudi. 4.Zombi (mfalme) SEHEM YA 1 Katika Kijiji kimoja Cha Ujasi kulikuwa na mfalme mmoja gaidi Sana aliyeitwa Zombi. Mfalme Zombi aliweka masharti magumu Sana katika himaya yake ya kwamba haruhusiwi mtu yeyote kuingia ndani ya Kijiji bila ya ruhusa ya mfalme, na hairuhusiwi mtu yeyote kutoka nje ya Kijiji bila ya ruhusa ya mfalme na endapo atatoka atakutana na mauza uza na mambo ya kutisha Sana huko njiani. Mfalme Zombi alikuwa ni gaidi Sana kiasi Cha kila mtu alimuogopa Sana aliposikia jina lake limetajwa. Watu wa Kijiji Cha Ujasi walikuwa hawavai nguo za kawaida Kama hivi Sasa ila wao wanaume walijifunga kaniki nyeusi chini na wanawake walijifunga kaniki nyeusi chini na kwenye maziwa tu. Siku moja chausiku alienda shamba kulima na baada ya hapo akaanza kukata kuni, akiwa tayari amefungasha mzigo wake wa kuni ghafla anasikia kukuru kakara za majani Kama Kuna mtu anamfata. Hamad...

JINSI YA KUTENGENEZA UBUYU WA BABU ISSA

Image
NAFASI ZA SENSA 2022 www.tamisemi.go.tz JIANDAE KUHESABIWA Kama ambavyo tunajua ubuyu huu ni pendwa Sana na watu hasa kwa wewe mjasiriamali ni vema ukajifunza. MAHITAJI 1. Sukari (vikombe 2 vya chai) 2. Maji (Vikombe vikubwa 2) 3. Ubuyu wa tunda (vikombe 4) 4. Ubuyu wa Unga (nusu kikombe) 5. Pilipili ya Unga (robo kijiko) 6. Chumvi ya Unga (Robo kijiko) 7. Hiliki ya Unga (robo kijiko ) 8. Rangi nyekundu au yoyote. NAMNA ✓ Chukua sifuria weka maji yachemke changanyana sukari, chumvi, pilipili ya Unga, rangi na hiliki ✓ Mimina ubuyu wa tunda na kuroga kwa dakika mbili ✓ Mimina ubuyu wa Unga na koroga ✓Baada ya hapo Mimina kwenye chombo Cha wazi na uache upoe Kama umependeza somo langu la leo weka comment hapo chini au Kama unaswali nitakujibu punde. KARIBU TENA

SAFARI YA MAFANIKIO YA BAKHRESA

Image
NAFASI ZA SENSA 2022 www.tamisemi.go.tz JIANDAE KUHESABIWA Leonimeona niwasogezee historia ya Billionaire wetu kutoka Tanzania ambaye anajulikana Sana kwa jina la Bakhresa. Jina lake kamili anaitwa SAID SALIM BAKHRESA. ALIZALIWA WAPI? Bakhresa alizaliwa mwaka 1949 huko Zanzibar na alianza elimu ya msingi, mpaka alipofikia umri wa miaka 14 Bakhresa aliacha shule kutokana na ugumu wa maisha ya nyumbani kwao. Hata hivyo baba yake alikuwa na madeni mengi sana hivyo akaamua aanze kufanya biashara ya viazi vya kuchemsha ili kukidhi familia yake. Mnamo 1960 Bakhresa akajihusisha pia na biashara ya kununua mabaki ya viumbe vya baharini Kama vile mifupa na magome ya viumbe Kisha aliyauza Mombasa (Kenya). Kutoka Kenya pia alinunua ngozi za viatu na kuja kuvishona huku Tanzania na kuviuza. Ilipofika1970 aliirudia Tena biashara yake ya viazi lakini akiwa ameiboresha na aliongezea mikate. Akaona haitoshi akaamua kununua mgahawa kutoka kwa mhindi ukiwa na jina l...