JINSI YA KUPIKA BIRIANI TAMU YA KUKU

Kaributena katika darasa letu la mapishi basi leo naenda kukuletea namna ya kuandaa biriani nzuri ya kuku.
MAHITAJI
kuku 1kg
Mchele wa basmati/ wakawaida (Hapa nitatumia nusu)
Vitunguu maji 1/4
Nyanya zilizosagwa tano
Nyanya ya mkebe
Vitunguu saumu punje 10
Pilipili za kijani 4
Mafuta 1/4
Mdalasini vijiti 5
Hiliki punje 10
Tangawizi vijiko 2 vya chakula
Majani ya nanaa yaliyokatwa kibakuli kidogo 1
Binzari nyembamba kijiko 1 cha chai
Chumvi kijiko 1 cha chai
Manjano 1/2 kijiko cha chai
Zafarani 1/2 kijiko cha chai
Kotmiri iliyokatwa 1/4 kikombe
Maziwa ya mtindi kikombe 1
Njegere (ukipenda)
JINSI YA KUANDAA
Loweka mchele w kwa dakika 15 hadi 30
Weka mafuta kwenye sifuria, yakishapata moto kaanga vitunguu maji hadi viwe na rangi ya brown kisha chota vitunguu robotatu ya ulivyovikaangaweka pembeni vingine vibaki kwenye sufuria.
Twanga kwa pamoja binzari nyembamba, kitunguu swaumu, tangawizi, nusu ya pilipili na vijiti vya mdalasini, kisha weka robo tatu ya vitunguu pembeni kisha kaanga vilivyobaki kwa dakika tatu.
Weka nyanya kisha koroga kwa dakika tano
Weka vipande vya kuku acha viive kwa dakika 10-15 na vikauke
Weka pilipili, kotmiri na masala ya kuku kisha weka mtindi koroga kisha acha lichemke mpaka liwe zito
Chemsha maji kwa hiliki na mdalasini na chumvi kisha weka mchele hakikisha hauivi kabisa acha kwa dakika tano baada ya hapo mwaga maji.
Panga wali na masala.
Kwanza chemsha maji ½ kikombe katika sufuria utakayopikia biryani. Maji yakishachemka anza kuweka wali kisha rosti nyunyiza vitunguu vilivyokaangwa baadhi,malizia na wali kisha ukishaweka wali weka vitunguu vilivyobaki juu. Kama una tumia zaafarani… Zaafarani kawaida hurowekwa kwenye vijiko vyenye maziwa ya vugu vugu na kumwagilia kwa juu.chukua kibakuli weka maji yauvuguvugu tia manjano au rangi ya njano koroga na umwagie juu ya wali kwa mistari ili birian yako iwe na rangi 2 nyeupe na njano.palia wali wako kama una tumia mkaa, au weka kwenye oven.
Weka moto mdogo kwa dakika 30. Baada ya hapo chakula chako kitakuwa tayar


Kama umependezwa na pishi langu la leo weka comment hapo chini au Kama unaswali nitakujibu punde.

KARIBU TENA

Comments

Post a Comment

Popular posts from this blog

JINSI YA KUTENGENEZA TAMBI NZURI ZA DENGU

JINSI YA KUANDAA VIUNGO VYA PILAU VYENYE HARUFU NZURI.

JINSI YA KUPIKA MAKANGE YA SAMAKI