JINSI YA KUANDAA VIUNGO VYA PILAU VYENYE HARUFU NZURI.



NAFASI ZA SENSA 2022 www.tamisemi.go.tz JIANDAE KUHESABIWA

Karibu kwa mara nyingine ukiwa na International Admin leo nitaenda kukuonesha namna ya kuandaa viungo vya pilau vyenye harufu. Ni rahisi sana, enjoy!
MAHITAJI
✓ Mdalasini mzima vijiti vikubwa vitano
✓ Binzari nyembamba kibakuli kidogo kimoja
✓Karafuu kibakuli kidogo kimoja
✓ Pilipili manga kibakuli kidogo kimoja
✓ Hiliki nzima kibakuli kidogo kimoja
✓ Uwatu kibakuli kidogo kimoja
✓Mustard seed kibakuli kidogo kimoja

MATAYARISHO
1. Chukua frying pan weka jikoni weka na viungo vyako vyote Kisha koroga kidogo kidogo ili usiviunguze (Moto uwe wa kiasi visiungue)
2. Ukimaliza ipua na viache vipoe
3. Chukua blender ya kusagia viungo na uvisage Kisha vitakuwa tayari kutumiwa (Kama hauna blender chukua kinu kidogo na mchi na uviponde ponde Kisha chekecha kwa kichujio Cha chai, japo itakuchukua mda kidogo)

Kama umependezwa na pishi langu la leo weka comment hapo chini au Kama unaswali nitakujibu punde.

KARIBU TENA

Comments

Popular posts from this blog

VITU VYA KUFANYA KARIBIA NA MITIHANI.

CHEKA WITH INTERNATIONAL ADMIN