SAFARI YA MAFANIKIO YA BAKHRESA



NAFASI ZA SENSA 2022 www.tamisemi.go.tz JIANDAE KUHESABIWA

Leonimeona niwasogezee historia ya Billionaire wetu kutoka Tanzania ambaye anajulikana Sana kwa jina la Bakhresa. Jina lake kamili anaitwa SAID SALIM BAKHRESA.

ALIZALIWA WAPI?
Bakhresa alizaliwa mwaka 1949 huko Zanzibar na alianza elimu ya msingi, mpaka alipofikia umri wa miaka 14 Bakhresa aliacha shule kutokana na ugumu wa maisha ya nyumbani kwao. Hata hivyo baba yake alikuwa na madeni mengi sana hivyo akaamua aanze kufanya biashara ya viazi vya kuchemsha ili kukidhi familia yake.
Mnamo 1960 Bakhresa akajihusisha pia na biashara ya kununua mabaki ya viumbe vya baharini Kama vile mifupa na magome ya viumbe Kisha aliyauza Mombasa (Kenya). Kutoka Kenya pia alinunua ngozi za viatu na kuja kuvishona huku Tanzania na kuviuza.
Ilipofika1970 aliirudia Tena biashara yake ya viazi lakini akiwa ameiboresha na aliongezea mikate. Akaona haitoshi akaamua kununua mgahawa kutoka kwa mhindi ukiwa na jina la AZAM (neno la kihindi ) likiwa na maana ya "UKUBWA" na ukifatilia kwa makini ndugu msomaji jina hili ndo analolitumia mpaka leo.
Mnamo 1990 aliamua kuwekeza katika uzalishaji wa nafaka ambapo mpaka hivi Leo viwanda vyake vinategemewa Sana katika nchi za Afrika Mashariki na Kati katika upatikanaji wa nafaka.
Mpaka kufikia mwaka 2000 jina la AZAM lilikuwa Sana kiasi Cha watu kutunga msemo "Amka na AZAM" yaani ukiamka unakula vitafunwa vya Azam, mchana chakula Cha Azam na usiku pia Azam.
Bakhresa bado akaendelea kujikita zaidi katika uzalishaji wa vinywaji pamoja na uwekezaji katika mpira wa mguu na ana timu yake inayosimamiwa na wakurugenzi mahiri (watoto) wake inayojulikana Kama Azam football. Akaongeza pia bidhaa za ice cream, chapati na matunda. Kila kukicha Bakhresa ni mtu ambae anazidi kuongeza bidhaa katika uwekezaji wake na amekuwa mtu ambae anashikilia uchumi mkubwa Sana kwa hapa Tanzania na Afrika. Mpaka hapo napenda nikushawishi ndugu msomaji wa blog hakikisha haukati tamaa na unajitahidi kukua kimawazo Kama alivyofanya au zaidi ya alivyofanya Bakhresa. Niambie kwenye comment unataka nikusogee historia ya nani baada ya Bakhresa.

Kama umependeza somo langu la leo weka comment hapo chini au Kama unaswali nitakujibu punde.

KARIBU TENA

Comments

Post a Comment

Popular posts from this blog

JINSI YA KUTENGENEZA TAMBI NZURI ZA DENGU

JINSI YA KUANDAA VIUNGO VYA PILAU VYENYE HARUFU NZURI.

JINSI YA KUPIKA MAKANGE YA SAMAKI