PILAU TAMU YA NYAMA.



NAFASI ZA SENSA 2022 www.tamisemi.go.tz JIANDAE KUHESABIWA

Karibu tena, basi leo International Admin anakuletea namna ya kupika pilau tamu ya nyama. Usiondoke angalia mwanzo mwisho, enjoy!
MAHITAJI
✓ Mchele (unaweza kuwa basmati au wakawaida)
✓ Nyama (mbuzi au ng'ombe)
✓ Viazi mbatata kiasi
✓ Unga wa pilau (nimeelekeza katika post ya nyuma hapo namna ya kuandaa)
✓ Chumvi kiasi
✓ Mafuta kiasi
✓ Vitunguu maji vitatu
kitunguu swaum kilichopondwa
✓Binzari nyembamba (uzile) uloweke kwenye maji kidogo.
. NAMNA YA KUPIKA
1. Chemsha nyama yako mpaka iive itie na chumvi kiasi (Supu iweke pembeni)
2. Kaanga viazi mbatata na viive (visiwe brown) Kisha vitoe vikiwa bado na rangi nyeupe. (Wengine hawakaangi, ila ukikaanga mbatata zako zitakuwa na ladha nzuri zaidi)
3. Kaanga vitunguu maji mpaka viwe brown (angalia visiungue vitabadili ladha ya chakula)
4. Weka mdalasini kaanga pamoja, Kisha weka uzile na hiliki na unga wa pilau kidogo Kisha kaanga. Mwisho weka kitunguu swaum na ukaange kidogo
5. Osha mchele, uchuje maji kisha weka mchele changanya na mchanganyiko wa jikoni Kisha mimina supu ya nyama weka nyama na viazi mbatata koroga (usikoroge Sana mara mbili inatosha) Kisha acha maji yakaukie.
6. Funika sifuria kwa karatasi ya foil ili kuacha harufu na kuivisha vizuri taratibu taratibu Kisha weka ufuniko wa sifuria kwa juu na moto kiasi. (Kumbuka kupunguza Moto chini) .
7.Baada ya dakika kadhaa pindua chakula chako na funika tena .
8.Chakula chako kikishaiva kitakuwa tayari kuliwa na unaweza kupakua kwa saladi au kachumbari uipendayo.

Kama umependezwa na pishi langu la leo weka comment hapo chini au Kama unaswali nitakujibu punde.

KARIBU TENA

Comments

Popular posts from this blog

JINSI YA KUTENGENEZA TAMBI NZURI ZA DENGU

JINSI YA KUANDAA VIUNGO VYA PILAU VYENYE HARUFU NZURI.

JINSI YA KUPIKA MAKANGE YA SAMAKI