JINSI YA KUJITENGENEZEA JINA (BRAND) KUPITIA MITANDAO

Kwanza, unatakiwa ujitambue wewe ni Nani na unafanya nini mitandaoni Kisha uje uyafanye yafuatayo:
1. WEKA PROFILE PICTURE (DP) .
Watu wengi wanaweka picha za katuni, midoli, maua, wananyama, logo, au picha za watu wengine. Hakuna mtu ambae anavutiwa na vikatuni nakadhalika. Unachotakiwa kufanya ni kuweka professional photo. Professional photo haipigwi mwili mzima, Wala watu hawaweki mapozi. Unaweza kuangalia hapa chini mfano wa professional photo na itapendeza Kama utaipiga na simu au kamera yenye quality. Professional photo huanza kuvuta makini ya mtu na kukufanya uonekane uko makini (serious) na unachokifanya.
2. WEKA ACCOUNT YAKO PUBLIC
Kuna watu account zao wanaziweka private Sana Sana Instagram. Kama unataka kufanya biashara au watu wajue unachokifanya usiweke account yako private. Weka Public kila mmoja aweze kuona unachokifanya.
3. TENGENEZA WAFUASI WENYE THAMANI (VALUABLE FOLLOWERS).
Kuna watu wanatabia ya ku follow watu hovyohovyo kwa lengo la kujipatia followers. Wengine wanadiriki kununua account zenye followers wengi ili wafanye biashara. Unaweza kuwa na followers wengi lakini hawaelewi na hawavutiwi na kile unachokifanya. Utaishia kupata likes nyingi lakini huoni wateja kwa sababu followers wako hawakuelewi. Ni Mara nyingi Sana tunaona Instagram mtu anataka auze cake au magari lakini anaenda kununua account iliyokuwa na followers wengi waliokuwa wanapostiwa udaku, wewe unavokuja kuanza ku post magari na cake zako wao watakuwa hawakuelewi Wala hawavutiwi na wewe. Utaishia kupata likes tu lakini wateja huwaoni. Sasa ufanye nini kupata valuable followers:
✓Kama unatumia Facebook na wewe ni Mpenzi wa mapishi, afya, mipira, n.k ingia kwenye group la kile ukipendacho anza kuwaomba urafiki wale watu wa kwenye group kwasababu mpaka wamejiunga maana yake wanapenda hiko kitu Kama wewe. Utafanya hivyo kwa magroup yote uyapendayo.
✓ Kama ni Instagram followe watu ambao wana content za vile unavyovipenda. Unaweza kukuta wewe ni mtu wa heshima lakini kwa tabia ya ku follow follow hovyo uka follow watu wenye maudhui yasiyofaa katika jamii.
4. ONESHA USHIRIKIANO KWA WENGINE (INTERACTION)
Ukiingia kwenye mtandao like, comment, jibu message za wengine ili kuifanya account yako iwe active. System za mitandao zilivyo kadiri utakavokuwa kuwa active na wewe utazidi kupata marafiki/ wafuasi wapya na activity za account yako huongezeka Kama likes, viewers,n.k kwahiyo unatakiwa uwe active.
5. EPUKA MAKOSA YA UANDISHI (TYPING ERRORS, GRAMMAR ERRORS).
Haya ni makosa ya uandishi, kutumia lugha isiyo rasmi/ya kihuni /mtaani humfanya mtu asione umakini wako. Au kutumia vifupisho vya maneno mfano watu wengi huwa wanaandika hivi:
•Cm | Simu
•Xawa| Sawa
•Pw| Poa
•nc| Nice
•Gud| Good
N.k kwa hiyo unatakiwa uandike kitu rasmi ili kuvuta makini ya mtu. Kwahiyo utapitia tena post yako uangalie Kama lugha imekaa sawa sawa ndo u post.
6. USIWEKE VITU VYENYE MTAZAMO HASI.
Usiweke vitu vyenye ukakasi katika jamiii kwani hii itakufanya uwapoteze baadhi ya watu kutokana na vile unavyoviweka katika page yako. Usiwe hasi mitandaoni kwani itafanya watu wakuone ni mwenye chuki, n.k hivyo wasivutiwe na page yako.
7. USIWEKE MAMBO BINAFSI MTANDAONi.
Kuna watu wana post mahusiano yao, na shida zao mitandao. Akiwa na furaha utamjua na siku akiamka na huzuni utajua. Watu wakiachana tayari ashaingia mitandaoni kupost "It's Over" n.k akiunguza mboga atapost, akiibiwa atapost, mtu akimkera atapost, n.k
Watu hawavutiwi na watu ambao wanatumia mitandao kujitangaza matatizo yao.
9. TATUA MATATIZO YA WATU.
Account yako iwe ina post vitu ambavyo vitaleta ushawishi katika jamii na kumfanya mtu aanze kukufatili. Kuna watu kila siku wanatembelea page fulani fulani kwa ajili ya mapishi, mahusiano, kupata habari, michezo, burudani, kupata hamasa nakadhalika.
Tumia account yako ku post vitu vitakavyoifanya jamii ianze kuvutiwa na wewe kuliko kupost shida zako maana hakuna wa kukusaidia dhaidi ya kujidhalilisha, hakuna mtu atakusaidia ukipost mtoto wako amevunja TV nyumbani n.k
10. KUWA NA BURUDANI SOMETIMES ( BE FUNNY)
Usiwe serious Sana Kuna mda inabidi uweke na vitu ambavyo vitamburudisha mtu ili avutiwe zaidi kuja tembelea account yako Mara kwa mara.
11. USIWEKE MANENO MENGI SANA NA USIPOST HOVYO
Watu wengi ni wavivu wa kusoma, unaweza kuandika caption yako tu fupi ikasindikizwa na video ili mtu atizame kuliko kusoma Sana. Pia usiwe una post hovyo. Unakuta mtu amepost picha za sehemu moja na siku moja karibia post 6 zote hazina caption za maana. Hii inaboa, wengine kila baada ya muda anapost tu, kuwa na ratiba yako ya kupost. Post nyingi humchosha mfatiliaji wako. Nitaandaa post maalum itakayokuonesha muda wa kupost katika mitandao.
NB:
✓ Kufanya account yako iwe na valuable followers sio Jambo la kustukiza (over night ) . Itakuchukua muda kupata valuable followers
✓ Hakikisha unatatua matatizo ya watu kupitia page zako
✓ Onesha ujuzi/kipaji wako ili watu wakufate unufaike na ujuzi/kipaji chake. Kama wewe ni mchekeshaji, mwanamuzi, fundi, mpishi,n.k usipoweka wazi ni ngumu Sana watu kujua kile kilicho ndani yako.


Kama upependezwa na umejifunza kitu kutokana na post yangu hii ya leo. Weka Comment hapo chini 👇👇👇👇

KARIBU TENA

Comments

Post a Comment

Popular posts from this blog

JINSI YA KUTENGENEZA TAMBI NZURI ZA DENGU

JINSI YA KUANDAA VIUNGO VYA PILAU VYENYE HARUFU NZURI.

JINSI YA KUPIKA MAKANGE YA SAMAKI