JINSI YA KUPIKA NDIZI MASALA.



NAFASI ZA SENSA 2022 www.tamisemi.go.tz JIANDAE KUHESABIWA

Karibu tena katika darasa letu la mapishi mbalimbali ukiwa na mimi International Admin. Basi leo tupo na pishi la ndizi mshale za masala. Enjoy!
MAHITAJI
✓ Ndizi mshale
. ✓ Binzari ya njano ( Turmeric powder)
✓Nyama
✓ Karoti
✓Njegere
✓ Vitunguu maji
✓ Tangawizi
✓ Kitunguu swaum
✓ Mafuta kiasi
✓ Nazi
✓ Curry Powder
MATAYARISHO.
1. Chemsha nyama ikishaiva menya ndizi mshale osha na uziweke.
2. Weka binzari ya njano (Turmeric powder) kijiko kimoja Cha chai weka na chumvi kiasi
3. Weka curry powder kijiko kimoja Cha chakula.
4. Chukua tangawizi na kitunguu swaum vilivyosagwa weka
4. Weka kitunguu maji, njegere na Karoti Kisha koroga taratibu usivunje ndizi acha mpaka ndizi na njegere ziive.
5. Weka tui zito la nazi koroga kidogokidogo mpaka liive (Kama chumvi utaona imepungua unaweza kuongeza kidogo)
6. Ndizi zako zitakuwa tayari kupakuliwa utakunywa na kinywaji chochote ukipendacho.

Kama umependezwa na pishi langu la leo weka comment hapo chini au Kama unaswali nitakujibu punde.

KARIBU TENA

Comments

Popular posts from this blog

VITU VYA KUFANYA KARIBIA NA MITIHANI.

CHEKA WITH INTERNATIONAL ADMIN

JINSI YA KUANDAA VIUNGO VYA PILAU VYENYE HARUFU NZURI.