KATIKA KIJIJI CHA UJASI



NAFASI ZA SENSA 2022 www.tamisemi.go.tz JIANDAE KUHESABIWA

SEHEMU YA 3
Daudi na Chausiku waliishi pamoja kwa muda wa miezi mitatu hivi. Siku moja Daudi akawa mwenye kupanga panga nguo zake na vitu vyake. Chausiku alimuona akashindwa kuvumilia.
Chausiku: Mbona sikuelewi Daudi unafanya nini ?
Daudi: Napanga vitu vyangu nitoroke nimechoka maisha ya hapa siyawezi nahitaji kuwaona ndugu zangu.
Chausiku: Ina mana unataka uniache na nani Mimi (kwa huzuni) dada angu amepoteza maisha kwa ajili yako!
Daudi: Natambua hilo mpenzi, sitoondoka peke yangu tutatoroka wote. Hivyo basi Chukua dumu la maji lijaze maji ya kunywa kesho alfajiri tutaanza safari.
Basi kesho ilipowadia Daudi akavaa nguo zake za kimjini mjini na akamvalisha Chausiku Suruari na T-shirt wakabeba chakula na dumu la maji tayari kwa safari
Daudi : Mpenzi wangu umependeza Sana umekuwa Kama madada duu wa mjini.
Basi wakaanza kutoroka na asubuhi kukapambazuka huku wakisonga na safari yao . Lakini kwa sababu mfalme aliweka mazindiko mtu akitoroka mambo ya ajabu yatatokea tokea. Basi upepo mkali ukaanza kuvuma katika Kijiji Cha Ujasi na watu wakaanza kuchanganyikiwa.
Wakati huo Chausiku na Daudi wanashangaa kuona damu zinatapakaa njiani wakakokimbia na upepo mkali Sana. Ghafla sauti kubwa ya ajabu ikaanza kusikika Kijiji kizima.
Sauti : Chausiku na Daudi wanatoroka, Kijiji kizima kitaangamia, ataanza kufa mfalme na wananchi watafuatia
Sauti ilijirudia rudia Mara nyingi na watu walianza kulia wakiwalaani Chausiku ba Daudi, mfalme alichanganyikiwa Sana asijue la kufanya. Watu wote na mfalme wakajikusanya sehem moja Kama kufa wafe kwa pamoja.
Wakati huo Chausiku na Daudi wakiwa porini wamekaa chini ukatokea mzimu wa Nyaukwama
Mzimu wa Nyaukwama: Chukueni hii dawa pulizeni Mara tatu, hali itakaa shwari i'la mfalme atakufa, Kisha mrudi mkawaelezee wana Kijiji
Basi wakafanya Kama walivyoambiwa na kule mfalme akaanza kufa, basi wananchi walichanganyikiwa Sana walijua Sasa zamu yao inafuata. Mara wakashangaa kuwaona Chausiku na Daudi wakaanza kuwarushia mawe maana wanataka kuwaletea umati.
Ghafla hali ikatulia wakaacha kuwapiga ndipo Chausiku na Daudi wakaanza kuwaelezea na kuwaaminisha kuwa watakuwa salama. wananchi wakapiga kelele
Wananchi: Kuanzia leo, Daudi mfalme Chausiku Malkia Walirudia rudia kuimba na kuwashangilia Kama mashujaa. Walikaa kwa muda wa wiki mbili Kisha mfalme na malkia wakasafiri kwenda mjini na walipirudi waliwaletea wananchi wao mavazi ya kisasa na maendeleo Kama kwenye jamii za kisasa, hakukuwa tena na Mila na tamaduni za ajabu ajabu watu wakapeleka watoto shule na wakaishi raha mustarehe.

MWISHO


Kama umependezwa na simulizi yangu hii na umejifunza kitu weka comment hapo chini au Kama unaswali nitakujibu punde.

KARIBU TENA

Comments

Popular posts from this blog

VITU VYA KUFANYA KARIBIA NA MITIHANI.

CHEKA WITH INTERNATIONAL ADMIN

JINSI YA KUANDAA VIUNGO VYA PILAU VYENYE HARUFU NZURI.