VITU VYA KUFANYA KARIBIA NA MITIHANI.

Karibu sana,basi leo tuko na namna ya kujiandaa wakati wa kukaribia mitihani ili uweze kufanya vizuri.
1. ACHA UOGA
Kuna watu wanaogopa Sana wakikaribia kufanya mitihani na hii hali hupelekea kokosa hali ya kutojiamini na kusoma kwa ku panic.
2. JUA MADA ZOTE ZA KILA SOMO UNALOSOMA.
Kuna watu wanaingia kwenye mtihani bila kujua hilo somo Lina mada zipi. Hatakama ukashindwa kujua moja kwa moja kila mada lakini kwa uchache ujue mada inahusu nini.
3. SOMA KWA LENGO (TARGET)
Tumia muda mwingi kusoma kile unachokielewa kuliko kukimbiza Kurasa /Slides hata Kama hauelewi. Hii itakufanya ushindwe kujiamini ukiingia katika mtihani kwani kila utakachokutana nacho utakuwa hukijui vizuri unajua juu juu tu. Lakini ukiingia na kitu ambacho umekielewa vizuri ukikutana nacho utakijibu kwa weledi na kukupa hamasa ya kujibu maswali mengine vizuri.
4. SOMA MITIHANI ILIYOPITA (Past Papers)
Kusoma mitihani iliyopita hii itakusaidia kukupa muongozo wa maswali yanavokuwa lakini pia itakupa muongozo wakati wa kusoma. Kuna sehemu huenda ukapuuzia haitoweza kutoka kwenye mtihani lakini ukikuta katika mitihani iliyopita itakufanya upate uzoefu wa mtihani mapema na uweze kujiandaa vizuri.
5. EPUKA KUKARIRI
Hakikisha unachokisoma una kielewa ili hata kitakapoulizwa kwa namna nyingine uweze kuelewa. Unapo kariri mstari mpya unasahau wa zamani, na swali linapoulizwa kivingine tu tayari unashindwa kuelewa ufanye nini na swali linataka nini.
6. SOMA NOTES FUPI ZENYE MAWAZO YA MSINGI ( Summary)
Ukiwa umebakisha mda mchache kuingia kwenye mtihani tumia Summary zako kusomea na sio vitabu. Hii itakufanya kukumbushia vitu vingi kwa muda mchache.
7. EPUKA USUMBUFU.
Usumbufu wowote utakaokufanya utumie muda mwingi kuliko kujiandaa na mitihani achana nao. Hapa nazungumzia changamoto za kifamilia, marafiki, wapenzi, vyama mbalimbali, mitandao ya kijamii n.k
8. SOMA KWENYE MAKUNDI. ( Group Discussion)
Pata muda wa kujadiliana na wenzako hii itakufanya kukumbuka kwa urahisi, kuelewa vizuri sehemu zinazokutatiza na kukupa mori ya kutoogopa mtihani. Lakini pia usisahau kupata mda kwa ajili ya kupitia wewe mwenyewe. Kukaa mwenyewe mda wote wa kusoma hutia hofu ya mtihani na unaweza kuelewa ndivyo sivyo na hakuna wa kukukosoa.
9. KAA NA WATU WENYE MTAZAMO CHANYA. (Positive thinker)
Epuka kukaa karibu na watu wanaokutisha tisha na kukukatisha tamaa kuhusu mtihani. "Huu mtihani sidhani Kama tutatoboa, yaani hata ukimeza slide yule ticha kazi bure tu, ng'ombe hanenepi siku ya mnada, Kama umeshindwa kuelewa siku zote utaelewa ndani ya siku moja,n.k" Kaa mbali na watu wa namna hii mara nyingi huwa washakata tamaa wanataka wasikie raha zaidi na wewe ukikata tamaa, aghalabu huwa wamesoma Sana mpaka hawajui wasome wapi hivyo wanavyokuona unasoma wanajihisi Kama bado hawajasoma na hutaka kukukatisha tamaa.
10. ANDAA MAPEMA MAZINGIRA YA MTIHANI NA UWAHI.
Kama Kuna vifaa utavihitaji siku ya mtihani andaa kabisa. Na wewe mwenyewe jitayarishe mapema na hakikisha ubawasili mapema eneo la mtihani. Kwani kufika kwa kuchelewa huanza kukupa hofu kabla ya kufanya mtihani wenyewe. Na ikiwezekana dakika 10 kabla ya mtihani acha kabisa kujadili mambo ya mtihani unaweza kupiga story nyingine za kawaida tu. Hii itakusaidia kuondoa hofu kwani ukisikia mtu anataja kitu ambacho hujakisoma tayari unaanza hofu.
11. EPUKA KUJADILI MTIHANI BAADA YA MTIHANI.
Hata Kama mtihani ulikuwa rahisi vipi au mgumu vipi usianze kuulizia majibu ya mtihani Mara tu baada ya kutoka kwenye mtihani kwani ukisikia jibu tofauti na ulichokijaza hii hukunyima amani ya kufanya vizuri na mitihani inayokuja.
12. MUOMBE MUNGU
Cha mwisho lakini sio kwa umuhimu. Muombe Sana mwenyezi mungu akujaalie kumbukumbu na kuyajaza yale yanayotakiwa kwenye mtihani. Kwani mbele yake hakuna kinachoshindikana, unaweza ukasoma lakini kwa bahati mbaya ukajikuta umesahau katika mtihani basi usichoke kumuomba mungu kabla ya mtihani,wakati wa mtihani na baada ya mtihani hii hukufanya uwe mwenye kujiamini na huondoa hali ya woga.


Kama upependezwa na umejifunza kitu kutokana na post yangu hii ya leo. Weka Comment hapo chini πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡

KARIBU TENA

Comments

  1. Ahsante sana kwa somo zuri na la kugusa maisha ya wapambanaji

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ahsante sana pia kwa comment nzuri
      Karibu Sana ufurahie huduma

      Delete

Post a Comment

Popular posts from this blog

CHEKA WITH INTERNATIONAL ADMIN

JINSI YA KUANDAA VIUNGO VYA PILAU VYENYE HARUFU NZURI.