HISTORIA YA SAMIA SULUHU HASSAN
Samia Suluhu Hassan alizaliwa mnamo tarehe 27/01/1960 katika visiwa vya Zanzibar. Alianza elimu ya msingi mnamo 1966-1972 katika shule tofauti tofauti zilizopo Unguja na Pemba yaani Zanzibar. Alianza katika shule ya CHAWAKA (Unguja), Kisha alihamia katika shule ya msingi ZIWANI (Pemba) na alimaliza katika shule ya msingi ya Mahonda. Elimu yake ya sekondari alianza 1973-1976 .Alisoma katika shule mbili, 1973-1975 alisoma katika shule ya sekondari ya Ngambo (Unguja) Kisha mwaka 1976 alihamia shule ya Lumumba (Unguja) ambapo alihitimu elimu ya sekondari. Hakuendelea tena na masomo ya chuo kwa muda huo. Aliajiriwa katika serikali ya Zanzibar Kama mchapishaji ambapo alipanda ngazi na kuwa Afisa mipango mnamo 1987-1988. Samia Suluhu Hassan alijiendeleza kielimu huku akiwa mtumishi wa serikali kwa kusoma kozi fupi mbalimbali Kama vile Sheti ya takwimu kabla ya kujiunga na Taasisi ya Maendeleo na uongozi ya Mzumbe Morogoro ambapo alifanikiwa kuhitimu stashahada ya juu ya utawala