JINSI YA KUPIKA MAANDAZI
JINSI YA KUPIKA MAANDAZI LAINI. MAHITAJI YA MAANDAZI 1. Unga - 5 Vikombe. 2. Tui la Nazi zito vugu vugu - 1 ¼ kikombe. 3. Sukari - 3/4 kikombe cha chai. 4. Samli iliyoyayushwa au mafuta - 3 vijiko vya Supu. 5.Hamirah - 2 Vijiko vya Supu. 6. Hiliki - 1/2 Kijiko cha chai. 7. Mafuta ya kukaangia. NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA. 1. Ndani ya kibakuli kidogo, mimina hamira na na vijiko viwili vya kulia vya tui. Weka kando mpaka hamira ianze kufura, kama dakika 5-10. 2. Pasha samli moto: 3. Ndani ya bakuli kubwa au sinia, changanya unga, sukari, iliki na samli ikiwa bado moto moto. 4. Mimina hamira ndani ya mchanganyiko wa unga. 5. Changanya na ukande huku ukitumia lile tui la nazi. Tui likipungua unaweza ukaongeza maziwa. 6. Kanda unga mpaka uwe laini. 7. Kata madonge *12 au 15 uyaweke kwenye baraza iliyonyunyiziwa unga na uyafunike ili yapate kufura na yasikauke. *Ukipenda maandazi manene fanya madonge 12. Ukipenda mepesi fanya madonge 15. 8. Madonge yakifura,