KATIKA KIJIJI CHA UJASI
SEHEMU YA 2
Asubuhi kukakucha basi Chausiku akaandaa mazingira ya kupata kifungua kinywa huku dada yake akisafisha mazingira. Mda wote huo Daudi akimtizama Sana Chausiku kwa mazingatio makubwa.
Basi wakanywa chai baada ya hapo Nyaukwama alimtakia kila la heri Daudi katika Safari yake. Kisha Chausiku na Daudi wakaanza safari ya kwenda kwa mfalme Zombi kuomba ruhusa. Walipokuwa wakipita njiani watu walishangaa Sana kumuona Chausiku akiwa na mgeni aliyevaa tofauti kabisa na asili yao. Kila walipopita watu waliitana ishara ya kuwashangaa Sana. Walivofika tu kwa mfalme walimkuta amekaa katika kiti chake Cha enzi. Mfalme Zombi alivowaona tu alichukia ghafla
Mfalme: Chausiku! ni upuuzi gani huu unafanya kuniletea mtu aliyevaa vitu vya ajabu ajabu mbele yangu,? Walinzi! mtoeni huyu na haya mavazi yake ya ajabu avae Kama wenzake.
Basi Daudi akavuliwa nguo na kuvalishwa Kaniki Kama wengine Kisha yeye na Chausiku wakapiga magoti mbele ya mfalme.
Chausiku: Ewe mfalme ulietukuka! mbele yako ni kijana msamalia mwema aliyekuwa anaenda Kijiji Cha jirani kusalimia ndugu zake amepotea njia Jana na kujikuta yupo ndani ya himaya ya Ujasi, nikamhifadhi kwa muda wa usiku tu na Leo nimemleta mbele zako anaomba ruhusa ya kurudi kwao.
Kwa ukali kabisa
Mfalme: Chausiku! Umefanya kosa kubwa Sana kumkaribisha mtu bila ruhusa yangu, kama ni mvamizi je? Unastahili adhabu. (Huku akiwageukia walinzi) mchukueni Chausiku na achapwe viboko arobaini Kisha awekwe kwenye zizi la ng'ombe kwa wiki moja.
Pale pale Daudi akadakia
Daudi: Samahani mfalme, yote yasingetokea sama na Mimi, nipo tayari kuibeba adhabu ya Chausiku.
Basi mfalme akaamrisha Daudi achapwe na atupwe kwenye zizi la ng'ombe kisha baada ya wiki ataitisha mkutano na wananchi ili atoe maamuzi. Baada ya Daudi kuchapwa na kutupwa katika zizi la ng'ombe akashangaa kuona mtu anaingia bandani, kumbe alikuwa ni Chausiku.
Daudi: Chausiku! umekuja kufanya nini tena huku wewe haustahili kuwa hapa !
Chausiku: Kama wewe ulikuwa tayari kuchukua adhabu yangu, kwanini na Mimi nishindwe kukaa na wewe? Sitoondoka nitakaa humu humu na wewe mwanzo mwisho.
Daudi: Hakika wewe ni mwanamke jasiri sijapata kuona, nakupenda sana Chausiku
Basi walikumbatia kwa furaha na wakakaa wote mpaka wiki ilipotimia mfalme akapiga lamgambo na wanakijiji wakajaa kusikikiza hukumu
Mfalme: Najua kila mmoja anafaham kwamba Chausiku ametuletea laana kubwa kijijini kwetu. Hivyo basi nikiwa Kama mfalme na mtawala wa himaya hii ya Ujasi, napenda kutoa amri kwamba Daudi hataondoka kwao atabaki kuwa mwanakijiji mwenzenu.
Wananchi walifurahia Sana na kupiga nderemo na vifijo, ghafla sauti ikasikika.
Chausiku: Sio haki! Sio haki! kijana wawatu amekukosea nini, mruhusu arudi kwao akawaone ndugu zake (huku akilia)
Mfalme: Puumbavu! Unabishana na amri ya mtawala sio? Unajifanya kiburi na jeuri mbele yangu sio! Sasa kichwa chako Leo kitakuwa kafara ya Kijiji. Walinzi! Mchinjeni huyu na wananchi washuhudie!
Basi Chausiku akakamatwa na walinzi, akalazwa sehemu ya kafara na shoka likainuliwa na wakati Lina shuka chini sauti ikaskika.
Nyaukwama: Acha! Acha! nipo tayari kufa kwa ajili ya Chausiku, lakini nina ombi. Baada ya kunichinja naomba Daudi aruhusiwe kwenda kwao na mdogo wangu Chausiku aishi kwa amani.
Mfalme: hilo Wala halina tabu, ilimradi tu damu imwagike hapa.
Basi Nyaukwama akachukuliwa na kuwekwa sehemu ya kafara Kisha shoka likainuliwa na kutua kwa nguvu shingoni kwake, damu ziliruka nyingi Sana huku akipapatika kwa uchungu wa umauti na akafa pale pale. Chausiku alilia Sana , Kisha mfalme akanadi
Mfalme: Ebu naomba Daudi atandikwe tena viboko mia, Kisha hataondoka kwao atabaki kuwa mwanakijiji mwenzenu Kama nilivosema mwanzo.
Daudi alitandikwa viboko mia wakati huo Chausiku alizidi kulia tu, watu walitawanyika na Chausiku na Daudi walirudi kuishi pamoja.
Kama umependezwa na Simulizi yangu weka maoni yako hapo chini na usikose muendelezo wake.
👍❤️
ReplyDeleteKaribu sana
Delete