HISTORIA YA ALIKO DANGOTE.
Aliko Dangote alizaliwa tarehe 10 April 1957 katika mji wa Kano nchini Nigeria. Anatokea katika familia ya kitajiri Sana ya wafanya biashara.
Aliko Dangote ni mjuu wa Alhajj Alhassan Dantata mfanya biashara mkubwa na tajiri aliyejishughulisha na mashamba makubwa ya Karanga na alifariki mwaka 1955.
Dangote alifanikiwa kuanza elimu na tangu alivokuwa mdogo alionesha kupendelea zaidi biashara na alikuwa akiuza pipi na mishumaa.
Elimu yake ya chuo kikuu aliipata nchini Misri katika chuo Cha Al -Azhary University (Cairo- Misri) na alisomea masomo ya biashara.
Alipofikisha miaka 20 alisajiri kampuni yake ndogo iliyokuwa inajihusisha na uzalishaji wa Sukari na cement iliyoitwa Dangote Group. Familiaya Dangote ilikuwa na maelewano mazuri na serikali ya Nigeria hivyo basi haikuwa ngumu kwake kupata vibali vya kufungua kampuni na Viwanda. Kama inavyofahamika kupata vibali vya biashara na mambo mbalimbali sio kazi rahisi hivyo unaweza kujifunza kitu katika familia ya kina Aliko Dangote.
Dangote alizidi kufanya biashara na Amerika ya kusini na Brazili hivyo alizidi kupata mafanikio na akamiliki mali nyingi sana. Hakuacha kuendelea na biashara zake nchini Nigeria na alikuza Sana uchumi wa nchi hiyo kwa kiasi kikubwa sana.
USIYOYAJUA KUHUSU DANGOTE
✓Aliko Dangote ana wafanyakazi zaidi ya elfu ishirini na tano
✓Aliko Dangote anazalisha sukari Afrika tani laki nane kwa mwaka 800,000
✓Aliko Dangote anaviwanda vingi katika nchi kumi na nne za Afrika
✓Aliko Dangote anamiliki asilimia 85 ya hisa katika kampuni yake
✓Aliko Dangote anazalisha cement tani million 45.6 kwa mwaka
✓Aliko Dangote ni rafiki mkubwa wa Bill gate na wanasikilizana
✓Aliko Dangote ni mtu asiye na majivuno
✓Lakini pia usisahau kuwa Dangote yeye ndio tajiri namba moja Afrika na alikuwa tajiri namba 30 kwa dunia nzima kwa takwimu za mwaka 2013.
JE? •Kwanini mimi na wewe tusitamani kuwa kama Aliko Dangote au zaidi yake?
•Kwanini mimi na wewe tusifikirie kujiajiri tuje tusaidie na vijana wengine kunyanyua uchumi wa Tanzania?
Kama umependa historia ya Dangote na umejifunza kitu kutoka kwake. Nipe comment hapo chini na uniambie ni nani afate baada ya Dangote.
Comments
Post a Comment