HISTORIA YA SAMIA SULUHU HASSAN

Samia Suluhu Hassan alizaliwa mnamo tarehe 27/01/1960 katika visiwa vya Zanzibar. Alianza elimu ya msingi mnamo 1966-1972 katika shule tofauti tofauti zilizopo Unguja na Pemba yaani Zanzibar. Alianza katika shule ya CHAWAKA (Unguja), Kisha alihamia katika shule ya msingi ZIWANI (Pemba) na alimaliza katika shule ya msingi ya Mahonda.

Elimu yake ya sekondari alianza 1973-1976 .Alisoma katika shule mbili, 1973-1975 alisoma katika shule ya sekondari ya Ngambo (Unguja) Kisha mwaka 1976 alihamia shule ya Lumumba (Unguja) ambapo alihitimu elimu ya sekondari.

Hakuendelea tena na masomo ya chuo kwa muda huo. Aliajiriwa katika serikali ya Zanzibar Kama mchapishaji ambapo alipanda ngazi na kuwa Afisa mipango mnamo 1987-1988.

Samia Suluhu Hassan alijiendeleza kielimu huku akiwa mtumishi wa serikali kwa kusoma kozi fupi mbalimbali Kama vile Sheti ya takwimu kabla ya kujiunga na Taasisi ya Maendeleo na uongozi ya Mzumbe Morogoro ambapo alifanikiwa kuhitimu stashahada ya juu ya utawala mwaka 1986.

Alisoma Stashahada ya uzamili ya uchumi katika chuo kikuu cha Manchester kilichopo nchini Uingereza Kati ya mwaka 1992-1994.

Hakuchoka kujiendeleza kielimu kwani mnamo 2015 alihitimu shahada ya uzamili katika Maendeleo ya uchumi ya kijamii katika program ya ushirikiano Kati ya Chuo kikuu Huria Cha Tanzania na Chuo kikuu cha Southern New Hampshire kilichopo Uingereza.

Samia Suluhu Hassan aliolewa na Bw Hafidh Ameir (wakati huo alikuwa Afisa wa Kilimo katika serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar )miaka miwili baada ya kuhitimu elimu ya sekondari mwaka 1978. Walijaaliwa kupata watoto wanne, mmoja wapo ni mwakilishi maalum katika bunge la Zanzibar nae ni Wanu Hafidh Ameir (1982).
Samia Suluhu Hassan alikuwa mtu mwenye kufanya kazi na mashirika mbalimbali tangu akiwa mdogo. Akiwa na umri wa miaka 16 alipata kufanya kazi na mashirika ya kimataifa ambapo Kati ya mwaka 1992 hadi 1994 alifanya kazi na shirika la umoja wa mataifa la mpango wa chakula ambapo alihudumia Kama Afisa Miradi, mbali na kufanya kazi serikalini na katika shirika la umoja wa mataifa. Vile vile kwa takribani miaka 10 alijikita na Taasisi zisizo za kiserikali katika harakati za usawa wa kijinsia.

Samia Suluhu Hassan alijiunga rasmi na siasa mnamo mwaka 2000. Wakati huo alichaguliwa kwenye baraza la wawakilishi la Zanzibar Kama mjumbe maalumu.

Nyota yake ilizidi kung'ara tangu alipoingia katika siasa katika serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. Akateuliwa na Mhe.Amani Karume kuwa waziri wa Afya,Jinsia na Watoto.

Mnamo mwaka 2005 alichaguliwa Tena kuwa mjumbe maalumu na kuteuliwa Kama waziri wa Utalii,Biashara na Uwekezaji katika Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. Mnamo 2010 aliweka Nia ya kuwania uwakilishi ambapo alichaguliwa kuwa mwakilishi wa jimbo la Makunduchi huko Zanzibar.

Nyota ya Samia ilizidi kupendeza kwani alichomoza katika baraza la mawaziri la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mnamo 2010 Kama waziri wa maswala ya Muungano katika serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania baada ya kuteuliwa na aliyekuwa Rais Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete.

Mnamo 2014 mwezi Machi Tanzania iliingia kwenye vuguvugu la kubadili katiba huku nyota ya Samia ilichomoza kwa mara nyingine baada ya kuchaguliwa kuwa makamu mwenyekiti wa Bunge maalum la katiba mjini Dodoma. Wakati huu ndipo alipoanzwa kutabiriwa kushika nafasi ya juu zaidi ya kiutawala ambapo mmoja wa wajumbe aliwaasa wajumbe wamfikirie mama Samia kwa nafasi ya juu zaidi kwenye uchaguzi uliokuwa unafuata mwaka 2015.

Nyota yake haikuwahi kufifia na kufikia Julai 2015 , Dkt John Magufuli mara baada ya mpambano mkali ndani ya CCM uliompa ushindi wa kupeperusha bendera ya CCM kwenye uchaguzi mkuu alimpendekeza Samia Suluhu Hassan kuwa mgombea mwenza wake na hatimaye baada ya uchaguzi Samia Suluhu Hassan aliweka historia nyingine ya kupanda katika siasa za Tanzania.

Baada ya kifo Cha Mhe.Rais Dkt John Pombe Magufuli tarehe 17March2021 Samia Suluhu Hassan akashikilia kiti Cha nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na amekuwa Rais wa sita baada ya Julius Nyerere, Ally Hassan Mwinyi, Benjamin Mkapa, Jakaya Kikwete na John Pombe Magufuli.

Wanasemaga siku zote nyota njema huonekana tangu asubuhi. Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan alionekana tangu akiwa mdogo. Hivyo basi ndugu msomaji usikate tamaa katika kupambania ndoto zako kwani utafika tu, jasho la mtu halipotei bure.


Kama umependa historia ya Samia Suluhu Hassan na umejifunza kitu kutoka kwake. Nipe comment hapo chini na uniambie ni nani afate baada ya Samia.

KARIBU TENA

Comments

  1. Baada ya Samia afuate role model wake Madam President......maarufu kama International Admin
    🤲🤲🤲🤲🤲

    ReplyDelete
    Replies
    1. Amiin na Mimi nangoja mje mniandike kwenye blogs sio nijiandike mwenyewe

      Delete
  2. Naomba utuletee Historia ya tajiri namba moja dunian, Elon musk

    ReplyDelete

Post a Comment

Popular posts from this blog

JINSI YA KUTENGENEZA TAMBI NZURI ZA DENGU

JINSI YA KUANDAA VIUNGO VYA PILAU VYENYE HARUFU NZURI.

JINSI YA KUPIKA MAKANGE YA SAMAKI