Posts

Showing posts with the label Histori za watu maarufu

HISTORIA YA SAMIA SULUHU HASSAN

Image
Samia Suluhu Hassan alizaliwa mnamo tarehe 27/01/1960 katika visiwa vya Zanzibar. Alianza elimu ya msingi mnamo 1966-1972 katika shule tofauti tofauti zilizopo Unguja na Pemba yaani Zanzibar. Alianza katika shule ya CHAWAKA (Unguja), Kisha alihamia katika shule ya msingi ZIWANI (Pemba) na alimaliza katika shule ya msingi ya Mahonda. Elimu yake ya sekondari alianza 1973-1976 .Alisoma katika shule mbili, 1973-1975 alisoma katika shule ya sekondari ya Ngambo (Unguja) Kisha mwaka 1976 alihamia shule ya Lumumba (Unguja) ambapo alihitimu elimu ya sekondari. Hakuendelea tena na masomo ya chuo kwa muda huo. Aliajiriwa katika serikali ya Zanzibar Kama mchapishaji ambapo alipanda ngazi na kuwa Afisa mipango mnamo 1987-1988. Samia Suluhu Hassan alijiendeleza kielimu huku akiwa mtumishi wa serikali kwa kusoma kozi fupi mbalimbali Kama vile Sheti ya takwimu kabla ya kujiunga na Taasisi ya Maendeleo na uongozi ya Mzumbe Morogoro ambapo alifanikiwa kuhitimu stashahada ya juu ya utawala

HISTORIA YA ALIKO DANGOTE.

Image
NAFASI ZA SENSA 2022 www.tamisemi.go.tz JIANDAE KUHESABIWA Aliko Dangote alizaliwa tarehe 10 April 1957 katika mji wa Kano nchini Nigeria. Anatokea katika familia ya kitajiri Sana ya wafanya biashara. Aliko Dangote ni mjuu wa Alhajj Alhassan Dantata mfanya biashara mkubwa na tajiri aliyejishughulisha na mashamba makubwa ya Karanga na alifariki mwaka 1955. Dangote alifanikiwa kuanza elimu na tangu alivokuwa mdogo alionesha kupendelea zaidi biashara na alikuwa akiuza pipi na mishumaa. Elimu yake ya chuo kikuu aliipata nchini Misri katika chuo Cha Al -Azhary University (Cairo- Misri) na alisomea masomo ya biashara. Alipofikisha miaka 20 alisajiri kampuni yake ndogo iliyokuwa inajihusisha na uzalishaji wa Sukari na cement iliyoitwa Dangote Group. Familiaya Dangote ilikuwa na maelewano mazuri na serikali ya Nigeria hivyo basi haikuwa ngumu kwake kupata vibali vya kufungua kampuni na Viwanda. Kama inavyofahamika kupata vibali vya biashara na m

SAFARI YA MAFANIKIO YA BAKHRESA

Image
NAFASI ZA SENSA 2022 www.tamisemi.go.tz JIANDAE KUHESABIWA Leonimeona niwasogezee historia ya Billionaire wetu kutoka Tanzania ambaye anajulikana Sana kwa jina la Bakhresa. Jina lake kamili anaitwa SAID SALIM BAKHRESA. ALIZALIWA WAPI? Bakhresa alizaliwa mwaka 1949 huko Zanzibar na alianza elimu ya msingi, mpaka alipofikia umri wa miaka 14 Bakhresa aliacha shule kutokana na ugumu wa maisha ya nyumbani kwao. Hata hivyo baba yake alikuwa na madeni mengi sana hivyo akaamua aanze kufanya biashara ya viazi vya kuchemsha ili kukidhi familia yake. Mnamo 1960 Bakhresa akajihusisha pia na biashara ya kununua mabaki ya viumbe vya baharini Kama vile mifupa na magome ya viumbe Kisha aliyauza Mombasa (Kenya). Kutoka Kenya pia alinunua ngozi za viatu na kuja kuvishona huku Tanzania na kuviuza. Ilipofika1970 aliirudia Tena biashara yake ya viazi lakini akiwa ameiboresha na aliongezea mikate. Akaona haitoshi akaamua kununua mgahawa kutoka kwa mhindi ukiwa na jina l