JINSI YA KUPIKA MAKANGE YA SAMAKI

Kaributena katika blog yangu uko na International Admin leo naenda kukuletea pishi la Makange ya samaki. Makange ni kati ya mboga rahisi sana kupika na utashangaa kujua kuwa huenda ulikuwa unajichelewesha kuandaa mboga hiyo nyumbani kwako kwa kuogopa vile unayakuta katika hoteli kubwa nyingi na yanavyowekwa kwenye sahani. Huenda umetamani kupika mboga ya makange kwa muda mrefu lakini ukadhani kwa namna ulivyowahi kuiona kwenye sahani, siyo mboga rahisi kupika.
TUANZE


MAHITAJI
✓ Kitunguu kimoja
✓ Nyanya kubwa 3
✓ Karoti moja
✓ Hoho moja
✓ Ndimu moja
✓Kitunguu saumu na tangawizi iliyosagwa kijiko kimoja (vyote kwa pamoja)
✓ Tomato fresh 2
✓ Chumvi kiasi
✓ Binzari nyembamba na pilipili manga ya unga kijiko kimoja cha chakula
✓ Curry powder kijiko kimoja cha chakula
✓ Binzari ya mchuzi kijiko kimoja cha chai
✓ Soya sauce ya kukoza vijiko 3 vya chakula
✓ Maji robo kikombe
✓ Mafuta ya kupikia vijiko 3-4
✓ Spice ya samaki kijiko 1 Cha chakula
✓ Samaki mkubwa mmoja -sato
✓ Vitunguu vichanga vilivyokatwa kikombe 1

MATAYARISHO
✓ Osha vizuri samaki wako mkatie ndimu, chumvi na kitunguu Saumu. Muache kwa muda viungo vikolee kisha mkaange.
✓ Osha vizuri viungo vyako yani kitunguu, hoho,Karoti na nyanya.
✓ Kata kitunguu, hoho na Karoti mapande makubwa kiasi kutoka juu kuja chini ziwe ndefu ndefu (usikate kwa mduara)
✓ Weka mafuta kwenye pan ya kukaangia Kisha kaanga vitunguu maji (angalia visiungue na visiwe brown ila viive)
✓ Weka Kitunguu Saumu na tangawizi mbichi
✓ Weka pilipili hoho na Karoti ulizozikata ndefu Kisha funika uache ziive kwa dakika 2
✓ Weka nyanya zilizosagwa au kukatwa katwa pamoja na chumvi kiasi . (Acha kwa dakika 2-3)
✓ Weka samaki wako sato uliyemkaanga
✓ Weka binzari nyembamba, pilipili manga, curry powder, spice ya samaki, binzari ya mchuzi, Soya sauce, ndimu, na vitunguu vichanga. Koroga Kisha acha kwa dakika 3-5 kwa Moto wa kiasi mpaka ikauke.


NB:
✓ usimgeuze geuze samaki hatakiwi kuvunjika geuza viungo kwa pembeni.
✓ Unaweza kutumia sato mbichi (wakuchemsha)sio lazima wa kukaanga
✓ Unaweza kuweka pilipili na majani ya kotmil ukipenda
✓ Karoti usikate mapande manene Sana ili ziive vizuri
✓ Unaweza kutumia limao Kama mbadala wa ndimu
✓ Unaweza kula makange yako kwa ugali, ndizi za kukaanga, viazi, mihogo, chips, wali, n.k

Kama umependezwa na pishi langu la leo weka comment hapo chini au Kama unaswali nitakujibu punde.

KARIBU TENA

Comments

Popular posts from this blog

VITU VYA KUFANYA KARIBIA NA MITIHANI.

CHEKA WITH INTERNATIONAL ADMIN

JINSI YA KUANDAA VIUNGO VYA PILAU VYENYE HARUFU NZURI.