PESA HUWA ZINAJIFICHA WAPI?



NAFASI ZA SENSA 2022 www.tamisemi.go.tz JIANDAE KUHESABIWA

Watu wengi siku hizi tunahangaika kutafuta pesa lakini hatujui pesa zimejificha wapi. Hapa nataka nikuoneshe sehemu tano ambazo pesa hujificha. 1.KIPAJI CHAKO
Watu wengi wenye vipaji sasa hivi ndio wanaoingiza pesa ndefu Sana kwa urahisi ndani ya muda mchache na wanahitajika Kila siku. Chukulia mfano. Mkandarasi akatangaza uwepo wake ukumbini kiingilio Tsh.500/= watakuja watu wangapi? Wewe utakwenda? Lakini diamond platnumz akitangaza atakuwepo kwa kiingilio Cha shilingi elfu tatu maelfu ya watu watamiminika. Watu wengi sasa hivi wanalipwa kwa kuhudumia watu wengi mfano Mbwana Samatta akiingia uwanjani maelfu na Malaki ya watu hufurahi hivyo basi anapata pesa nyingi kutokana na watu wengi na kupata balozi mbalimbali. Lakini daktari atahudumia wagonjwa tu waambao kwa siku huenda akahudumia sio zaidi ya mia moja.Hivyo basi hata Kama una taaluma yako lakini bado unatakiwa ukijue kipaji chako. Hakuna mtu asiye na kipaji duniani anza kukitafuta utakijua. Your talent is your money (kipaji chako ndo pesa yako) mfano yule kijana aliyeshinda katika mashindano ya kuchekesha ya cheka2 aliyeshida 10M za kitanzania. Japokuwa ni mwanafunzi wachuo lakini hatukumtambua kwa taaluma yake tulimtambua kwa kipaji chake, Nicki wa pili ni msomi mkubwa lakin hatumtambui kwa taaluma yake tunamtambua kwa kipaji chake. Hivyo basi kama unategemea taaluma pekee itachukua muda sana kutambulika kwa watu na hata utakapokosa kazi au kujiajiri kwa taaluma yako basi jitahidi kipaji chako kikuokoe.
2.MATATIZO
Matatizo ya watu ni pesa. Watu wanakutana na changamoto mbalimbali ambazo wewe ukizitatua zitakuingizia pesa. Mfano watu walihangaika sana wakishikwa na haja pindi wapo safarini lakini kuna watu wamejenga vyoo vya njiani na wanaingiza pesa ndefu tu. Watu walikuwa na shida ya vinywaji wawapo njiani, na kuna watu wakaweka vinywaji na maji ya kandoro.
3.BIDHAA
Watu Kila siku wanahitaji bidhaa mbalimbali ziwe vyakula,mavazi, vifaa vya ujenzi au vya kutumia tu n.k mfano tunaona kwa bakhresa, Mo dewj na Aliko Dangote wanavojishughulisha na bidhaa mbalimbali na wanajiingizia pesa.
4.TAARIFA
Watu wanapenda habari mbalimbali ziwe za udaku, michezo,Mambo ya mungu,yaliyojiri duniani, n.k wote tunaona Millard ayo, tbc, itv,wasafi media, n.k vyombo vyote hivyo vinatoa taarifa na watu wanapenda wanavifatilia na vinaingiza pesa ndefu sana.
5.UJUZI WAKO
Iwe unajua kutengeneza cake, iwe unajua kushona ,kujenga, computer, make up, kufundisha n.k ujuzi wako ni pesa mimi binafsi sijasomea ualimu lakini najua nina kipaji cha kufundisha na Kila kipindi nikiwa likizo nafundisha na nalipwa pesa vizuri tu, Sasa kwanini usitumie ujuzi wako kujikwamua kiuchumi au ndo unangoja uje ufanye kazi juu ya kile ulichosomea tu.

Kama umependezwa na somo langu la leo weka comment hapo chini au Kama unaswali nitakujibu punde.

KARIBU TENA

Comments

Popular posts from this blog

JINSI YA KUTENGENEZA TAMBI NZURI ZA DENGU

JINSI YA KUANDAA VIUNGO VYA PILAU VYENYE HARUFU NZURI.

JINSI YA KUPIKA MAKANGE YA SAMAKI