VITU VYA KUFANYA KARIBIA NA MITIHANI.
Karibu sana,basi leo tuko na namna ya kujiandaa wakati wa kukaribia mitihani ili uweze kufanya vizuri. 1. ACHA UOGA Kuna watu wanaogopa Sana wakikaribia kufanya mitihani na hii hali hupelekea kokosa hali ya kutojiamini na kusoma kwa ku panic. 2. JUA MADA ZOTE ZA KILA SOMO UNALOSOMA. Kuna watu wanaingia kwenye mtihani bila kujua hilo somo Lina mada zipi. Hatakama ukashindwa kujua moja kwa moja kila mada lakini kwa uchache ujue mada inahusu nini. 3. SOMA KWA LENGO (TARGET) Tumia muda mwingi kusoma kile unachokielewa kuliko kukimbiza Kurasa /Slides hata Kama hauelewi. Hii itakufanya ushindwe kujiamini ukiingia katika mtihani kwani kila utakachokutana nacho utakuwa hukijui vizuri unajua juu juu tu. Lakini ukiingia na kitu ambacho umekielewa vizuri ukikutana nacho utakijibu kwa weledi na kukupa hamasa ya kujibu maswali mengine vizuri. 4. SOMA MITIHANI ILIYOPITA (Past Papers) Kusoma mitihani iliyopita hii itakusaidia kukupa muongozo wa maswali yanavokuwa lakini pia