JINSI YA KUTENGENEZA MANGO PICKLE (CHACHANDU YA EMBE) NYUMBANI

Karibu tena katika darasa letu la mapishi basi leo naenda kukuletea namna ya kuandaa achari ya embe nyumbani unaweza kula kwa ugali au chochote ukipendacho.
MAHITAJI.
✓Maembe mabichi (usitumie embe zilizoiva au zilizoanza kuiva)
✓ Pilipili mbichi (kama ukipenda)
✓ Achari masala
✓Masala ya kuwasha
✓ Mafuta ya kupikia
✓ Binzari ya njano (tumeric powder)
✓ Chumvi kiasi.
MATAYARISHO.

✓ Osha vizuri embe zako na uzikate Kate saizi uipendayo lakini usimenye maganga (Kata vikonyo cha juu na chini)
✓ Loweka embe zako weka na chumvi kwa muda wa siku mbili au tatu Kisha utazianika kwa siku moja au mbili. (Angalia zisikauke Sana zitaleta ugumu wakati wa kula)
✓ Weka mafuta jikoni mpaka yapate moto Kisha yatoe yaweke pembeni yapoe yawe Kama ulivyoyatoa dukani.
✓Chukua chombo chenye nafasi ya kutosha changanya vitu vyote pamoja na mafuta mpaka vichanganyike vizuri
✓ Kisha anika mchanganyiko wako kwa siku kadhaa ili uive vizuri na hapo utakuwa tayari kwa matumizi.


NB:
√ Usiweke maji hata kidogo kwani yakiingia maji hata kidogo baada ya wiki itaweka utando mweupe na haitofaa tena kwa matumizi
√ Mafuta weka mengi ili kusaidia isiharibike kwa haraka kwani ina uwezo wa kukaa mwaka mzima. (Wakati wa kupakua unaweza kuchukua kijiko na kupunguza mafuta).
√ Hakikisha hauongei hovyo wakati unaandaa kwani mate yakiingia hufanya ichache kwa haraka

Kama umependezwa na pishi langu la leo weka comment hapo chini au Kama unaswali nitakujibu punde.

KARIBU TENA

Comments

Popular posts from this blog

JINSI YA KUTENGENEZA TAMBI NZURI ZA DENGU

JINSI YA KUANDAA VIUNGO VYA PILAU VYENYE HARUFU NZURI.

JINSI YA KUPIKA MAKANGE YA SAMAKI