KATIKA KIJIJI CHA UJASI
WAHUSIKA
1. Chausiku
2. Nyaukwama (Dada wa chausiku)
3. Daudi.
4.Zombi (mfalme)
SEHEM YA 1
Katika Kijiji kimoja Cha Ujasi kulikuwa na mfalme mmoja gaidi Sana aliyeitwa Zombi. Mfalme Zombi aliweka masharti magumu Sana katika himaya yake ya kwamba haruhusiwi mtu yeyote kuingia ndani ya Kijiji bila ya ruhusa ya mfalme, na hairuhusiwi mtu yeyote kutoka nje ya Kijiji bila ya ruhusa ya mfalme na endapo atatoka atakutana na mauza uza na mambo ya kutisha Sana huko njiani.
Mfalme Zombi alikuwa ni gaidi Sana kiasi Cha kila mtu alimuogopa Sana aliposikia jina lake limetajwa. Watu wa Kijiji Cha Ujasi walikuwa hawavai nguo za kawaida Kama hivi Sasa ila wao wanaume walijifunga kaniki nyeusi chini na wanawake walijifunga kaniki nyeusi chini na kwenye maziwa tu.
Siku moja chausiku alienda shamba kulima na baada ya hapo akaanza kukata kuni, akiwa tayari amefungasha mzigo wake wa kuni ghafla anasikia kukuru kakara za majani Kama Kuna mtu anamfata. Hamad! alishangaa kumuona mwanaume amevaa bukta T-shirt na raba huku amebeba begi la mkononi akimfuata. Alidhania ni kiumbe Cha ajabu Sana maana hakuwahi kumuona mtu Kama huyo tangu azaliwe na akaanza kukimbia.
Daudi alimkimbiza na Chausiku alipodondoka chini basi Daudi alimkaribia na kumwambia. Daudi: Usiniogope, Mimi ni msamalia mwema tu nimetoka mjini nilikuwa naenda Kijiji Cha jirani kusalimia ndugu zangu Sasa nashangaa nimejikuta katika Kijiji hiki nadhani nimepotea. Hivyo basi nilikuwa naomba msaada wako maana jioni imeshaanza kuingia na sina pa kwenda.
Chausiku: Aanhaa kumbe! Unaonekana wewe ni mtu wa dunia nyingine, ivi unaitwa Nani.
DAudi: Naitwa Daudi
Chausiku: Unaonekana pia wewe ni msomi na mtanashati maana hayo majina ni ya watu wa mjini kabisa (huku akitabasam) Mimi naitwa Chausiku
Daudi: Oh! Chausiku au naweza kukwita cha Night (huku akicheka)
Chausiku: Chanaiti ndio kitu gani
Daudi: Ni jina lako kwa kizungu au kingereza
Chausiku: Aanhaa kumbe, basi nimefurahi Sana kuitwa jina la kizungu naimani na mimi Kuna siku nitaenda kwa wazungu. Lakini nina hofu kubwa juu yako.
Daudi: Hofu gani tena?
Chausiku: Mfalme wetu ni gaidi sana, haruhusu mtu yeyote kuingia kijinini bila ruhusa yake na haruhusu mtu yeyote kutoka kijinini bila ridhaa yake, sidhani Kama atakuruhusu urudi kwenu mjini.
Daudi: Oh! nadhani hayo ni kwa ajili ya wanahimaya yake. Sidhani Kama mgeni Kama mimi ataninyimia ruhusa. Wewe nisaidie hifadhi kwa leo kisha ya Ngoswe tumuachie Ngoswe tutajua kesho hiyo hiyo.
Basi wakaanza safari ya kurudi nyumbani kwa kina Chausiku. Walivyofika walimkuta Nyaukwama amekaa nje na kwa mshangao kabisa akashangaa Sana anachokiona machoni.
Nyaukwama: Chausiku! ni kitu gani hiki unaleta?
Chausiku: Daada! hata mgeni hajakaa chini unaanza kuhamaki? tutulie kwanza tule Kisha nitakuelezea kuhusu mgeni.
Basi wakatulia wakala na wakaanza kufahamishana.
Nyaukwama: Pole Sana Daudi kwa yaliyokukuta, ila nina hofu Sana kuhusu mfalme hiyo kesho. Sidhani Kama atakuruhusu kurudi kwenu. Haya kumekucha Sasa tukalale.
Basi Chausiku alienda kulala kwa dada yake Nyaukwama na kumpisha Daudi katika chumba chake. Daudi alijikuta akimfikiria Sana Chausiku katika usiku ule kuliko safari yake ya kurudi kwao.
Kama umependezwa na Simulizi yangu weka maoni yako hapo chini na usikose muendelezo wake.
Hahahaha hahahaha hahahaha hahahaha waoooh international admin big up ... Practice make it perfect keep going
ReplyDeleteThanks a lot dear
Delete