MAPISHI YA KUKU SEKELA.



NAFASI ZA SENSA 2022 www.tamisemi.go.tz JIANDAE KUHESABIWA

Karibuni sana katika darasa letu zuri la mapishi. Leo tutaangalia namna ya kumtengeneza kuku mtamu wa sekela au wengine wanaita Tandoor Chicken
MAHITAJI
✓ Kuku 1Kg.(mpasue kati)
✓Ukwaju 1/2pakti (katika kikombe kimoja Cha maji)
✓kitunguu Swaum (kijiko 1 Cha chakula)
✓Tangawizi (kijiko 1 Cha chakula )
✓Binzari nyembamba ya unga (uzile) - kijiko 1 Cha chai.
✓Pilipili manga (kijiko 1 Cha chai)
✓Chumvi kiasi
✓Tandoori masala (kijiko 1 Cha chai)

NAMNA.
✓ Safisha kuku vizuri Kisha wachuje maji (wengine wanapenda kutoa ngozi)
✓Loweka Ukwaju na maji kikombe kimoja Kisha koroga mpaka urojo uwe mzito Chuja Kama tui la nazi ondoa kokwa Kisha mimina kwenye kuku.
✓weka vitunguu swaum na tangawizi Kisha changanya
✓ weka pilipili manga, uzile na chumvi Kisha changanya vizuri.
✓weka tandoori masala Kisha changanya vizuri na uache Kama dakika 30 ivi viungo vikolee vizuri kisha mpake mafuta kiasi kabla ya kuchoma.


NAMNA YA KUCHOMA.
1. Wapange kuku kwenye nyavu ya juu (ipake mafuta kidogo) na weka treya tupu katika nyavu ya pili
2. Kwenye kitufe Cha selector na temperature kote weka grill (hapo kuku wako ataiva katika Moto wa juu)
3. Choma kwa dakika 25-30 (watachuja maji yatadondokea kwenye treya tupu)
4.Ondoa treya iliyodondokewa na maji baada ya kuku wako kukauka na kupata rangi vizuri
5. Kisha badilisha kitufe Cha selector weka bake na kwenye temperature weka 350° acha kwa dakika 10-15 ili wachomeke vizuri kwa moto wa chini.
6.Wakishakauka vizuri watoe na upange kwenye sahani unaweza Kula na saladi au pilipili.
NB:
* Kama huna oven unatumia jiko la mkaa.
* Kubadilisha vitufe katika kuchoma kuku kunasaidia kuku wako kuiva vizuri pande zote bila kugeuzageuza.
* Tandoori masala unaweza kutengeneza mwenyewe


Kama umependezwa na pishi langu la leo weka comment hapo chini au Kama unaswali nitakujibu punde.

KARIBU TENA

Comments

Post a Comment

Popular posts from this blog

VITU VYA KUFANYA KARIBIA NA MITIHANI.

CHEKA WITH INTERNATIONAL ADMIN

JINSI YA KUANDAA VIUNGO VYA PILAU VYENYE HARUFU NZURI.