Posts

Showing posts from March, 2022

HISTORIA YA ALIKO DANGOTE.

Image
NAFASI ZA SENSA 2022 www.tamisemi.go.tz JIANDAE KUHESABIWA Aliko Dangote alizaliwa tarehe 10 April 1957 katika mji wa Kano nchini Nigeria. Anatokea katika familia ya kitajiri Sana ya wafanya biashara. Aliko Dangote ni mjuu wa Alhajj Alhassan Dantata mfanya biashara mkubwa na tajiri aliyejishughulisha na mashamba makubwa ya Karanga na alifariki mwaka 1955. Dangote alifanikiwa kuanza elimu na tangu alivokuwa mdogo alionesha kupendelea zaidi biashara na alikuwa akiuza pipi na mishumaa. Elimu yake ya chuo kikuu aliipata nchini Misri katika chuo Cha Al -Azhary University (Cairo- Misri) na alisomea masomo ya biashara. Alipofikisha miaka 20 alisajiri kampuni yake ndogo iliyokuwa inajihusisha na uzalishaji wa Sukari na cement iliyoitwa Dangote Group. Familiaya Dangote ilikuwa na maelewano mazuri na serikali ya Nigeria hivyo basi haikuwa ngumu kwake kupata vibali vya kufungua kampuni na Viwanda. Kama inavyofahamika kupata vibali vya biashara na m

KATIKA KIJIJI CHA UJASI

NAFASI ZA SENSA 2022 www.tamisemi.go.tz JIANDAE KUHESABIWA SEHEMU YA 3 Daudi na Chausiku waliishi pamoja kwa muda wa miezi mitatu hivi. Siku moja Daudi akawa mwenye kupanga panga nguo zake na vitu vyake. Chausiku alimuona akashindwa kuvumilia. Chausiku: Mbona sikuelewi Daudi unafanya nini ? Daudi: Napanga vitu vyangu nitoroke nimechoka maisha ya hapa siyawezi nahitaji kuwaona ndugu zangu. Chausiku: Ina mana unataka uniache na nani Mimi (kwa huzuni) dada angu amepoteza maisha kwa ajili yako! Daudi: Natambua hilo mpenzi, sitoondoka peke yangu tutatoroka wote. Hivyo basi Chukua dumu la maji lijaze maji ya kunywa kesho alfajiri tutaanza safari. Basi kesho ilipowadia Daudi akavaa nguo zake za kimjini mjini na akamvalisha Chausiku Suruari na T-shirt wakabeba chakula na dumu la maji tayari kwa safari Daudi : Mpenzi wangu umependeza Sana umekuwa Kama madada duu wa mjini. Basi wakaanza kutoroka na asubuhi kukapambazuka huku wakisonga na safari

KATIKA KIJIJI CHA UJASI

NAFASI ZA SENSA 2022 www.tamisemi.go.tz JIANDAE KUHESABIWA SEHEMU YA 2 Asubuhi kukakucha basi Chausiku akaandaa mazingira ya kupata kifungua kinywa huku dada yake akisafisha mazingira. Mda wote huo Daudi akimtizama Sana Chausiku kwa mazingatio makubwa. Basi wakanywa chai baada ya hapo Nyaukwama alimtakia kila la heri Daudi katika Safari yake. Kisha Chausiku na Daudi wakaanza safari ya kwenda kwa mfalme Zombi kuomba ruhusa. Walipokuwa wakipita njiani watu walishangaa Sana kumuona Chausiku akiwa na mgeni aliyevaa tofauti kabisa na asili yao. Kila walipopita watu waliitana ishara ya kuwashangaa Sana. Walivofika tu kwa mfalme walimkuta amekaa katika kiti chake Cha enzi. Mfalme Zombi alivowaona tu alichukia ghafla Mfalme: Chausiku! ni upuuzi gani huu unafanya kuniletea mtu aliyevaa vitu vya ajabu ajabu mbele yangu,? Walinzi! mtoeni huyu na haya mavazi yake ya ajabu avae Kama wenzake. Basi Daudi akavuliwa nguo na kuvalishwa Kaniki Kama wengine Kisha yey

KATIKA KIJIJI CHA UJASI

Image
International Admin WAHUSIKA 1. Chausiku 2. Nyaukwama (Dada wa chausiku) 3. Daudi. 4.Zombi (mfalme) SEHEM YA 1 Katika Kijiji kimoja Cha Ujasi kulikuwa na mfalme mmoja gaidi Sana aliyeitwa Zombi. Mfalme Zombi aliweka masharti magumu Sana katika himaya yake ya kwamba haruhusiwi mtu yeyote kuingia ndani ya Kijiji bila ya ruhusa ya mfalme, na hairuhusiwi mtu yeyote kutoka nje ya Kijiji bila ya ruhusa ya mfalme na endapo atatoka atakutana na mauza uza na mambo ya kutisha Sana huko njiani. Mfalme Zombi alikuwa ni gaidi Sana kiasi Cha kila mtu alimuogopa Sana aliposikia jina lake limetajwa. Watu wa Kijiji Cha Ujasi walikuwa hawavai nguo za kawaida Kama hivi Sasa ila wao wanaume walijifunga kaniki nyeusi chini na wanawake walijifunga kaniki nyeusi chini na kwenye maziwa tu. Siku moja chausiku alienda shamba kulima na baada ya hapo akaanza kukata kuni, akiwa tayari amefungasha mzigo wake wa kuni ghafla anasikia kukuru kakara za majani Kama Kuna mtu anamfata. Hamad

JINSI YA KUTENGENEZA UBUYU WA BABU ISSA

Image
NAFASI ZA SENSA 2022 www.tamisemi.go.tz JIANDAE KUHESABIWA Kama ambavyo tunajua ubuyu huu ni pendwa Sana na watu hasa kwa wewe mjasiriamali ni vema ukajifunza. MAHITAJI 1. Sukari (vikombe 2 vya chai) 2. Maji (Vikombe vikubwa 2) 3. Ubuyu wa tunda (vikombe 4) 4. Ubuyu wa Unga (nusu kikombe) 5. Pilipili ya Unga (robo kijiko) 6. Chumvi ya Unga (Robo kijiko) 7. Hiliki ya Unga (robo kijiko ) 8. Rangi nyekundu au yoyote. NAMNA ✓ Chukua sifuria weka maji yachemke changanyana sukari, chumvi, pilipili ya Unga, rangi na hiliki ✓ Mimina ubuyu wa tunda na kuroga kwa dakika mbili ✓ Mimina ubuyu wa Unga na koroga ✓Baada ya hapo Mimina kwenye chombo Cha wazi na uache upoe Kama umependeza somo langu la leo weka comment hapo chini au Kama unaswali nitakujibu punde. KARIBU TENA

SAFARI YA MAFANIKIO YA BAKHRESA

Image
NAFASI ZA SENSA 2022 www.tamisemi.go.tz JIANDAE KUHESABIWA Leonimeona niwasogezee historia ya Billionaire wetu kutoka Tanzania ambaye anajulikana Sana kwa jina la Bakhresa. Jina lake kamili anaitwa SAID SALIM BAKHRESA. ALIZALIWA WAPI? Bakhresa alizaliwa mwaka 1949 huko Zanzibar na alianza elimu ya msingi, mpaka alipofikia umri wa miaka 14 Bakhresa aliacha shule kutokana na ugumu wa maisha ya nyumbani kwao. Hata hivyo baba yake alikuwa na madeni mengi sana hivyo akaamua aanze kufanya biashara ya viazi vya kuchemsha ili kukidhi familia yake. Mnamo 1960 Bakhresa akajihusisha pia na biashara ya kununua mabaki ya viumbe vya baharini Kama vile mifupa na magome ya viumbe Kisha aliyauza Mombasa (Kenya). Kutoka Kenya pia alinunua ngozi za viatu na kuja kuvishona huku Tanzania na kuviuza. Ilipofika1970 aliirudia Tena biashara yake ya viazi lakini akiwa ameiboresha na aliongezea mikate. Akaona haitoshi akaamua kununua mgahawa kutoka kwa mhindi ukiwa na jina l

JINSI YA KUTENGENEZA TAMBI NZURI ZA DENGU

Image
NAFASI ZA SENSA 2022 www.tamisemi.go.tz JIANDAE KUHESABIWA Kwanza kabisa nikuhakikishie kuwa tambi za namna hii ni nzuri na tofauti kabisa na unazoziona barabarani. Kajaribu halafu utarudi kutoa mrejesho hasa kwa wajasiriamali hizi utaziuza Sana. MAHITAJI 1. Unga wa dengu (8-10)Kg 2. Sukari (2Kg) 3. Ngano (2Kg) 4. Manjano (kijiko 1) 5. Chicken Masala (Kijiko 1) 6. Kitunguu swaum kilichopondwa kiasi 7.Baking powder ya Simba ya blue (nusu kijiko) 8. Pilipili manga (Kijiko 1) 9. Chumvi kiasi 10. Maji ya vuguvugu (lita 3-4) 11. Mafuta ya kula NAMNA YA KUTENGENEZA ✓ Changanya mchanganyo wote kasoro maji mpaka vichanganyike ✓ Weka maji ya vugu vugu mpaka mchanganyo wako uwe laini Kama ugali wa mtoto ✓ Chota mchanganyo wako weka kwenye kifaa Cha kutengenezea tambi ✓ Hakikisha mafuta yamepata moto vizuri ✓ Kaanga tambi kwenye mafuta (Koroga Mara moja) ✓ Chuja mafuta kwenye tambi baada ya kuzitoa jikoni > ✓ Subiri zipoe na tambi zako zitak

MAISHA NI DUARA LEO UKO HAPA KESHO UKO PALE

NAFASI ZA SENSA 2022 www.tamisemi.go.tz JIANDAE KUHESABIWA SEHEMU YA 7 Kesho ikafika akawasindikiza Airport wakati wanataka kuondoka Mr. Otto von Admin akatoa kadi ya bank na kumkabidhi Joseph "Joseph, sisi ni wafanya biashara wakubwa Sana ujerumani. Tulikuja kutalii Tanzania na bahati nzuri tumekutana na kijana mkarimu Sana na mwenye changamoto Sana. Tumeamua kukufungulia account ya bank na kukuwekea kiasi kidogo Cha fedha kitakachokutosha kufanya Yale uliyotuambia jana. Kwenye account tumeweka kiasi Cha shilingi Million Mia Saba tuna imani itakutosha kufanya Yale uliyotuambia. Baada ya mwaka mmoja tutarudi Tanzania kushuhudia Kama uliyotuahidi umeyatekeleza. Yote kwa yote Ahsante Sana kwa ukarimu wako, Mwenyezi mungu akutangulie" Mrs Otto von Admin akamkabidhi kikaratasi na kumwambia "Na hi ndio password ya kadi yako, utabadilisha mwenyewe" Joseph akaanza kububujikwa na machozi, alivyoulizwa sababu ya kulia ni nini. Akasema yeye t

MAISHA NI DUARA LEO UKO HAPA KESHO UKO PALE

NAFASI ZA SENSA 2022 www.tamisemi.go.tz JIANDAE KUHESABIWA SEHEMU YA 6 Wakati anataka kufytua risasi mama Doreen akamdaka mkono na ikamkosa ikapiga pembeni. Joseph alichomoka mbio mpaka miguu ikagusa kisogo. Mama Doreen akamshika mume wake na kuingia nae chumbani. "Mume wangu, unataka yule mtoto abaki yatima? Em achana nae yule" Baba Doreen akapunguza jazba Kisha wakarudi sebleni kuangalia Television. Wakati wanaangalia TV mama Doreen akakumbuka maneno ya mwanae kabla hajaondoka kuwa amtunzie mwanae. Basi akaingiwa na wasiwasi kuwa mtoto akifa mwanae akirudi itakuwaje. Basi akaingia chumbani na kubeba kiasi Cha fedha Kisha akatoka na kumuaga mumewe sebleni. "Mume wangu, natoka kidogo naenda saloon" basi akaruhusiwa na njiani akakutana na Joseph alikuwa hata hajafika mbali maana alikuwa anatembea kwa miguu. Akapaki gari na kumwita ndani ya gari. Mama: "Umesema mtoto ana shida gani?" Joseph: "Mtoto anatakiwa kufanyiw

MAISHA NI DUARA LEO UKO HAPA KESHO UKO PALE

Image
NAFASI ZA SENSA 2022 www.tamisemi.go.tz JIANDAE KUHESABIWA Kama wewe hupendelei kusoma sikiliza audio SEHEM YA 5 Basi siku zilipita na miezi ikaenda Doreen akapelekwa hospital kujifungua na alijifungua mtoto wa kiume ambaye alifanana Sana na Joseph. Baba alipoingia kumuangalia mjukuu wake akastuka: "shit! Yaani nilitarajia atafanana na Mimi au wewe mama yake yani ameenda kufanana tena na yule maskini!! Namchukia Sana huyu mtoto yeye pamoja na baba yake" Akaondoka kwa hasira na wote wakarudi nyumbani. Wakati Doreen akiendelea na kumnyonyesha mwanae Kuna siku aliandika barua Kisha akaificha na kukaa nayo. Ilipofika siku moja kabla ya kutimia miezi mitatu alimwita Grace chumbani kwake na kumuomba kwa namna yoyote aifikishe ile barua kwa Joseph. Kisha akaenda kuzungumza na mama yake: "Mama, najua kwamba naondoka na ninamuacha mwanangu kwa miaka mingi. Naomba unitunzie mwanangu kwa gharama zozote nampenda Sana" (Huku akilia) Basi baba a

MAISHA NI DUARA LEO UKO HAPA KESHO UKO PALE

Image
NAFASI ZA SENSA 2022 www.tamisemi.go.tz JIANDAE KUHESABIWA Kama wewe hupendelei kusoma sikiliza audio SEHEM YA 4 Baada ya Doreen kupimwa baba yake alipewa majibu Kisha akarudi wodini kwa mke wake. Mama: " Vipi mume wangu ulimpima Doreen" Baba: "Exactly, she is pregnant !" (Ni mjamzito) Mama akaanza kuhuzunika huku machozi yakimlenga, baba Doreen alibaki tu akizunguka zunguka anaenda mbele na kurudi nyuma. Mama akamuomba mumewe amuitie binti yake. Doreen akaitwa wodini kwa mama yake na kwa ukali kabisa. "Naomba uniambie hii mimba ni ya nani?" Doreen akawa anasita huku akilia na baada ya kubanwa Sana akaamua kusema: "Mimba ni ya Joseph yule jirani yetu" Mama: "Whaaaaaaat!! yule kijana mchafu wa kimasikini anaenuka uvundo??? Ulikosa nini mwanangu nyumbani, kwanini lakini umeamua kutudhalilisha hivi, tena na kijana wa kimaskini, hukuona wanaume wote wa hadhi yako lakini." Mama aliendelea kulalamik

MAISHA NI DUARA LEO UKO HAPA KESHO UKO PALE

Image
NAFASI ZA SENSA 2022 www.tamisemi.go.tz JIANDAE KUHESABIWA Kama wewe hupendelei kusoma sikiliza audio SEHEM YA 3 Mara baada ya kupambazuka Joseph aliamua kumtumia Doreen message akimuomba waonane. Basi jioni ikafika na Joseph alionana na Doreen wakatembea umbali wa Kilometer mbili bila kuongeleshana chochote, wakafika katika daraja Joseph akasimama na kumwambia Doreen. " Nataka niku suprize!" Doreen akafurahi Sana lakini Joseph hakuonesha kuwa mwenye furaha. Joseph kwa upole kabisa "I love you So much Doreen" Doreen akamjibu "I know that sweetheart, ooh Leo umeniamulia uniongelee kimombo baby " (huku akicheka) Joseph "Ah! Si unajua tena nimekaa na wewe Sana kwahiyo saivi kizungu hakinipigi chenga". Joseph akaendelea kusema "Unajua katika maisha Classes is inevitable (matabaka hayakwepeki) , wewe ni binti wa kitajiri Sana Doreen, haustahili kuwa na mtu Kama Mimi. Mimi ni fukara siwezi kuwa na wewe"

MAISHA NI DUARA LEO UKO HAPA KESHO UKO PALE

Image
NAFASI ZA SENSA 2022 www.tamisemi.go.tz JIANDAE KUHESABIWA Kama wewe hupendelei kusoma sikiliza audio SEHEM YA 2 Baada ya masaa kadhaa Joseph alirudi nyumbani kwao na mizigo yake kabla kuingia ndani alikuta unga umetapakaa ardhini mithili ya mchanga wa beach na vitu vingine vyote viko chini na banda limebomolewa. Akaingia tu ndani kwao huku akiwa mwenye mshangao Kama rubani aliyepoteza mawasiliano akashangaa kumkuta mama yake ana hali mbaya sana na mdogo wake Rose akimpepea. Akashindwa hata asijue la kufanya akabaki tu kumuuliza Rose "Kimetokea nini?" Rose alimkata jicho tu Kaka yake bila kumwambia chochote basi ikabidi tu naye ajumuike kumuuguza mama pale kwa muda huku hata haelewi kilichotokea. Ikafika jioni hali ya mama ikawa nafuu kidogo ndipo mama alipoanza kuongea. "Rose mwanangu, naomba utupishe kidogo nina maongezi na Kaka yako!" Rose akawaacha wafanye mazungumzo: ""Joseph mwanangu, yote haya yasingetokea sam

MAISHA NI DUARA LEO UKO HAPA KESHO UKO PALE

Image
Kama wewe hupendelei kusoma basi sikiliza audio WAHUSIKA WAKUU ✓Familia ya1 -Joseph -mama Joseph -Rose (mdogo wa Joseph) ✓Familia ya Pili -Doreen -Baba Doreen -Mama Doreen -Josten (Kaka wa Doreen) -Grace (Housegirl) NB: Simulizi ina sehemu 7 tu SEHEM YA 1 Katika mtaa mmoja uliosheheni nyumba zenye hadhi ya kimataifa na gharama Sana kulikuwa pia na kijumba kidogo na dhalili kabisa Cha kina Joseph mwanafunzi wa darasa la Saba aliyekuwa akiishi na mama yake na mdogo wake Rose ambae bado alikuwa Yuko chekechea. Lakini pia kulikuwa na nyumba nzuri mithili ya Kasri ya kifalme aliyekuwa akipatikana binti mrembo Sana mwenye umbo la kuvutia na sura ya kuwaka waka (Doreen) ambae naye pia alikuwa darasa la Saba aliyesoma katika shule za International kuanzia chekechea mpaka shule ya msingi. Nyumbani kwao kulifurika magari mengi ya kifahari kiasi Cha kwamba hata akibeba handbag ya pink basi ataangalia na gari ya pink ili kumetisha. Basi katika harakati za kimaisha na kupita pita