JINSI YA KUTENGENEZA TAMBI NZURI ZA DENGU



NAFASI ZA SENSA 2022 www.tamisemi.go.tz JIANDAE KUHESABIWA

Kwanza kabisa nikuhakikishie kuwa tambi za namna hii ni nzuri na tofauti kabisa na unazoziona barabarani. Kajaribu halafu utarudi kutoa mrejesho hasa kwa wajasiriamali hizi utaziuza Sana.
MAHITAJI
1. Unga wa dengu (8-10)Kg
2. Sukari (2Kg)
3. Ngano (2Kg)
4. Manjano (kijiko 1)
5. Chicken Masala (Kijiko 1)
6. Kitunguu swaum kilichopondwa kiasi
7.Baking powder ya Simba ya blue (nusu kijiko)
8. Pilipili manga (Kijiko 1)
9. Chumvi kiasi
10. Maji ya vuguvugu (lita 3-4)
11. Mafuta ya kula

NAMNA YA KUTENGENEZA
✓ Changanya mchanganyo wote kasoro maji mpaka vichanganyike
✓ Weka maji ya vugu vugu mpaka
mchanganyo wako uwe laini Kama ugali wa mtoto
✓ Chota mchanganyo wako weka kwenye kifaa Cha kutengenezea tambi
✓ Hakikisha mafuta yamepata moto vizuri
✓ Kaanga tambi kwenye mafuta (Koroga Mara moja)
✓ Chuja mafuta kwenye tambi baada ya kuzitoa jikoni
> ✓ Subiri zipoe na tambi zako zitakuwa tayari kuliwa au kuzipaki kwa biashara

Kama umependeza somo langu la leo weka comment hapo chini au Kama unaswali nitakujibu punde.

KARIBU TENA

Comments

Post a Comment

Popular posts from this blog

VITU VYA KUFANYA KARIBIA NA MITIHANI.

CHEKA WITH INTERNATIONAL ADMIN

JINSI YA KUANDAA VIUNGO VYA PILAU VYENYE HARUFU NZURI.