MAISHA NI DUARA LEO UKO HAPA KESHO UKO PALE
SEHEMU YA 7
Kesho ikafika akawasindikiza Airport wakati wanataka kuondoka Mr. Otto von Admin akatoa kadi ya bank na kumkabidhi Joseph
"Joseph, sisi ni wafanya biashara wakubwa Sana ujerumani. Tulikuja kutalii Tanzania na bahati nzuri tumekutana na kijana mkarimu Sana na mwenye changamoto Sana. Tumeamua kukufungulia account ya bank na kukuwekea kiasi kidogo Cha fedha kitakachokutosha kufanya Yale uliyotuambia jana. Kwenye account tumeweka kiasi Cha shilingi Million Mia Saba tuna imani itakutosha kufanya Yale uliyotuambia. Baada ya mwaka mmoja tutarudi Tanzania kushuhudia Kama uliyotuahidi umeyatekeleza. Yote kwa yote Ahsante Sana kwa ukarimu wako, Mwenyezi mungu akutangulie"
Mrs Otto von Admin akamkabidhi kikaratasi na kumwambia "Na hi ndio password ya kadi yako, utabadilisha mwenyewe"
Joseph akaanza kububujikwa na machozi, alivyoulizwa sababu ya kulia ni nini. Akasema yeye tangu amezaliwa hajawahi hata kushika million nne kwa pamoja, leo hii anaenda kumiliki million Mia Saba ni kitu ambacho alihisi Kama anaota.
Basi wajerumani wakaondoka zao, na Joseph akafanya Kama alivoahidi mama alipelekwa India kwa matibabu na akapona. Alifungua biashara nyingi Sana na kubwa Sana mjini akawa maarufu kila Kona. Mdogo wake alikuwa anasoma shule nzuri Sana ya International.
Baada ya mwaka mmoja, baba Doreen kumbe alichukuaga mkopo na akashindwa kuulipa kwa wakati hivyo basi mali zake zote zilitaifishwa. Joseph alizidi kupanuka kibiashara na kuwa maarufu kiasi Cha kwamba akawa haitwi Joseph anaitwa Mr.Joe
Hakutamani kupata mwanamke mwingine yeyote mbali na mama mtoto wake Doreen. Miaka ikakatika Doreen akahitimu masomo yake Ukraine na akarudi Tanzania.
Alivyofika kwao pale akashangaa kukuta wamiliki ni watu wengine hivyo basi akaelekezwa kwenye nyumba yao mpya ambayo ilikuwa ni yakawaida mnooo. Alivokutana na mama yake baada ya kufika home.
Mama :"Doreen, hivi ushakutana na Mr.Joe!" (Kwa shauku kubwa)
Doreen:"Mr.Joe ni nani Kwanza mimi nataka nijue mwanangu yupo wapi"
Mama:"Mr.Joe huyo ni mzazi mwenzako bwana Joseph yule na mtoto alikuja akamchukua akakae nae sasaivi amekuwa big boss na amehamia jijini Dar es Salaam. Hivyo basi kesho ikiwezekana uende DSM ukamsalimie na ukamuone mtoto wenu na ikiwezekana mtuongezee mjukuu mwingine"
Basi kesho Doreen akafunga safari mpaka Mbezi beach kwenye ofisi kuu ya Mr.Joe alivyofika akaambiwa hawezi kumuona boss maana yuko busy Sana na hawaitambui appointment yake.
Basi wakajaribu kumpigia simu Mr.Joe na kumwambia kuwa ni Doreen. Mr.Joe alimruhusu apite, alivyoingia ndani Mr.Joe alimfata na kumkumbatia kwa nguvu kabisa :"I miss you darling, it has been a long time sijakuona kwenye upeo wa macho yangu" Doreen akalia:"Naomba unisamehe Sana kwa makosa ya wazazi wangu"
Mr.Joe: "Katika maisha dunia siku zote ni duara,Leo upo mashariki na kesho aliyekuwa mashariki atakuwa magharibi na aliyekuwa magharibi atakuwa mashariki. Nililazimishwa kukuacha sababu sikuwa na uwezo, na nimejitahidi kutafuta kile wazazi wako walichohitaji niwe nacho ili niweze kukumiliki tena. Nilikuwa na kusubiri kwa hamu urudi mpenzi wangu na taratibu za harusi zote zilishakuwa tayari ulikuwa wewe tu ndo haupo. Nakupenda Sana mke wangu mtarajiwe, kifo tu ndo kije kitutenganishe"
Basi walifanikiwa kufunga ndoa ya kifahari Sana na wakaenda Canada kula fungate, walivyorudi maisha yakaendelea kwa raha mustarehe. Baba Doreen, mama Doreen na Josten walienda kuomba msamaha familia ya kina Joseph na walisamehewa bila hiyana. Joseph aliwapa mitaji shemeji yake na wakwe zake, mama Joseph alirudi kuwa kijana kama unavomuona mama Dangote.
<
Na hii ndio maana ya MAISHA NI DUARA LEO UKO HAPA KESHO UKO PALE
Kama umependezwa na simulizi yangu hii na umejifunza kitu weka comment hapo chini au Kama unaswali nitakujibu punde.
🔥🔥🔥👏👏👏Keep it up💪...very nice reading with alot to learn
ReplyDeleteIt more amazing dear , be creative zaidi, I appreciate it
ReplyDelete