MAISHA NI DUARA LEO UKO HAPA KESHO UKO PALE



NAFASI ZA SENSA 2022 www.tamisemi.go.tz JIANDAE KUHESABIWA

Kama wewe hupendelei kusoma sikiliza audio SEHEM YA 4
Baada ya Doreen kupimwa baba yake alipewa majibu Kisha akarudi wodini kwa mke wake.
Mama: " Vipi mume wangu ulimpima Doreen"
Baba: "Exactly, she is pregnant !"(Ni mjamzito) Mama akaanza kuhuzunika huku machozi yakimlenga, baba Doreen alibaki tu akizunguka zunguka anaenda mbele na kurudi nyuma. Mama akamuomba mumewe amuitie binti yake.
Doreen akaitwa wodini kwa mama yake na kwa ukali kabisa. "Naomba uniambie hii mimba ni ya nani?" Doreen akawa anasita huku akilia na baada ya kubanwa Sana akaamua kusema: "Mimba ni ya Joseph yule jirani yetu"
Mama: "Whaaaaaaat!! yule kijana mchafu wa kimasikini anaenuka uvundo??? Ulikosa nini mwanangu nyumbani, kwanini lakini umeamua kutudhalilisha hivi, tena na kijana wa kimaskini, hukuona wanaume wote wa hadhi yako lakini." Mama aliendelea kulalamika tu kwa masikitiko makubwa Doreen nae alilia Sana akiomba kusamehewa. Kisha akatoka nje ya wodi ya mama yake na kwenda kukaa nje alipokaa Josten na Grace. Baba yake akaingia wodini kwa mama yake: "Wife, vipi amekwambia mimba ni ya nani" mama kwa kuchoka kabisa
"yah! ameniambia mume wangu, ni ya yule kijana wa kimaskini. Joseph pale karibu na nyumbani"
"Whaaaaaaat!! Maskini ndo anampa mimba mwanangu??? Hii siwezi kukubali" Akatoka nje na kwenda kumfokea Sana Doreen kiasi Cha kwamba mpaka Daktari alikuja:
"Samahani mzee, tayari imeshatokea hata ukimlaumu haitosaidia kitu. Ni vema mkarudi nyumbani na kuyazungumza kwa utaratibu maana mnavo bwatizana hapa mnawasumbua wagonjwa wengine na wanahitaji utulivu"
Basi waliamua kurudi nyumbani na kuyazungumza, mama nae alikuwa tayari amepata nafuu aliruhusiwa kurudi nyumbani. Wakafika sebleni kila mmoja akiwa amepoa na kukaa kimya. Ndipo baba akaamua kufanya maamuzi.
"Najua wote Sasa mnafaham Kama Doreen ni mjamzito, Sasa basi atakaa hapa nitamgharamikia kila kitu Kinachohitajika kwa mjamzito mpaka atakapojifungua. Kisha atamnyonyesha mwanae kwa muda wa miezi mitatu then nitampeleka Ukraine kusoma na atamuacha mtoto. Lakini sambamba na hilo nitampokonya simu na computer ili asije akafanya mawasiliano yoyote na huyo kijana kutoka Sasa. Na asitokee yeyote kutumika kwenda kinyume na hivyo, in addition to that (na nyongeza katika hilo) Hatotoka nje tena, madaktari kwa ajili ya clinic watakuja humu humu, I'm done ( nimemaliza)" Baba akaondoka sebleni kwa jazba sana.

Kama umependezwa na simulizi yangu ya leo weka comment hapo chini au Kama unaswali nitakujibu punde.

KARIBU TENA

Comments

Popular posts from this blog

VITU VYA KUFANYA KARIBIA NA MITIHANI.

CHEKA WITH INTERNATIONAL ADMIN

JINSI YA KUANDAA VIUNGO VYA PILAU VYENYE HARUFU NZURI.