MAISHA NI DUARA LEO UKO HAPA KESHO UKO PALE



NAFASI ZA SENSA 2022 www.tamisemi.go.tz JIANDAE KUHESABIWA

Kama wewe hupendelei kusoma sikiliza audio SEHEM YA 5
Basi siku zilipita na miezi ikaenda Doreen akapelekwa hospital kujifungua na alijifungua mtoto wa kiume ambaye alifanana Sana na Joseph. Baba alipoingia kumuangalia mjukuu wake akastuka:
"shit! Yaani nilitarajia atafanana na Mimi au wewe mama yake yani ameenda kufanana tena na yule maskini!! Namchukia Sana huyu mtoto yeye pamoja na baba yake"
Akaondoka kwa hasira na wote wakarudi nyumbani. Wakati Doreen akiendelea na kumnyonyesha mwanae Kuna siku aliandika barua Kisha akaificha na kukaa nayo. Ilipofika siku moja kabla ya kutimia miezi mitatu alimwita Grace chumbani kwake na kumuomba kwa namna yoyote aifikishe ile barua kwa Joseph.
Kisha akaenda kuzungumza na mama yake: "Mama, najua kwamba naondoka na ninamuacha mwanangu kwa miaka mingi. Naomba unitunzie mwanangu kwa gharama zozote nampenda Sana" (Huku akilia)
Basi baba akamchukua Doreen kwenda nae mjini kufanya Shopping za vitu. Grace nae akaenda hadi anapofanya kazi Joseph na kumkabidhi ile barua . Joseph aliifungua na kuisoma: "Mpenzi wangu Joseph, unajua the way ninavyokupenda na nitazidi kuendelea kukupenda. Najua yote yalitokea ni kwa sababu ya matabaka ya kimaisha baina yetu. Naomba upambane Sana maana nahisi unajukumu kubwa Sana mbeleni. Mimi nitapotea katika upeo wa macho yako nakwenda mbali Sana, ila tambua sasahivi tumeongezeka. Nakupenda Sana sweetheart na nitazidi kukupenda milele. Nakutakia maisha mema"
Joseph kila alivyojaribu kuitafsiri ile barua hakuielewa inamaanisha nini, akaikunja tu na kuiweka mfukoni. Kesho nayo haikuwa mbali siku ya safari ikawadia. Familia nzima ilitoka kumsindikiza Doreen mpaka Airport, Doreen akambusu mwanae ambae hata jina hakupewa tangu azaliwe kisha akaenda kupanda ndege tayari kwa safari ya Ukraine.
Basi wakaagana pale na ndege ya kina Doreen ilipoondoka familia nzima iligeuza safari na moja kwa moja hadi kwa kina Joseph. Walishuka mama, baba na Josten ndani ya gari baba akiwa amembeba mtoto na wakaingia ndani kwa kina Joseph bila kubisha hodi. Wakamkuta mama Joseph na Rose, hawakuchelewa , baba akamuweka mtoto chini Kisha kwa ukali akamwambia mama Joseph:
"Huyo ni mjukuu wako ambae unajua kijana wako alichokifanya kwa binti yetu, hatuhitaji kupoteza muda tumewasaidia kumlea akiwa tumboni na mpaka Sasa leo ametimiza miezi mitatu. Mchukueni sisi hatuwezi kukaa na huyu mwanaharam na mtamtafutia jina wenyewe. Na katika kipindi hicho hatutarajii mtu yeyote kuja kutuomba msaada wa aina yoyote vinginevyo atauawa."
Mama Joseph alilalamika kwa uchungu
"Kwanini mnaamua kukitesa kiumbe kisicho na hatia, nyinyi mnaona kabisa hali yetu huyu mtoto atateseka Sana, mwanamke mwenzangu (huku akimuelekea mama Doreen kwa huruma) naomba uwe na huruma na huyu mtoto unaujua uchungu wa mtoto " mama Doreen akadakia
"Ishia hapo hapo! Huruma ninayo ila sio kwa watoto wa haram, mume wangu! Twondokeni!) Josten alimkata jicho la dharau mama Joseph Kisha akamtemea mate kwa pembeni na kuondoka.
Mama Joseph alichanganyikiwa Sana na hapo hapo alidondoka chini na kupoteza faham, Mtoto alikuwa analia sana. Rose akaenda kuchukua kanga na kumfunga mbeleko mtoto huku akimpepea mama yake. Mama alipata ugonjwa wa kupooza pale pale. Wakati Joseph anarudi kutoka kazini akashangaa kumkuta Rose amembeba mtoto. Kwa mshangao mkubwa:
"Rose! Huyo mtoto wa nani uliyembeba na mbona analia sana" Rose hakumjibu kitu aliendelea kumbembeleza mtoto, Joseph akamsogelea kwa karibu alishangaa kuona yule mtoto anafanana naye Sana, lakini hakuelewa chochote Kama ni wa kwake, akaingia ndani kumuangalia mama akamkuta ana hali mbaya amepooza upande mmoja.
Alichanganyikiwa sana asijue chochote kinachoendelea. Rose alikuja na kumsimulia kilichotokea,Joseph akarudi kumtizama mtoto anajiona kabisa ni yeye akambeba mwanae na kumbusu huku akijaribu kukumbushia maneno ya kwenye barua ndo akapata maana ya maneno "sasaivi tumeongezeka"
Basi alijikuta ana jukumu zito la kumhudumia mama ambaye ni mgonjwa, kumhudumia mdogo wake na kumhudumia mwanae. Hayakuwa majukumu rahisi kabisa kwake, ikambidi aongeze na jukumu lingine la kuweka mfanyakazi kwa ajili ya kumlea mtoto.
Maisha yalizidi kuwa magumu Sana kwenye familia yao maana na biashara zilikuwa ngumu. Ilimbidi aongeze na biashara za kacha na vitu vya asili ili kuongeza riziki kidogo maana sehem hiyo ilikuwa ikitembelewa na watalii Mara kwa mara. Baada ya miezi Kama miwili ivi mtoto alikuwa anaumwa Sana, na walivyompeleka hospital daktari akamwambia :
"Mtoto utumbo umejikunja, anatakiwa afanyiwe operation haraka Sana ndani ya siku tatu vinginevyo atapoteza maisha. Operation ita gharimu sio chini ya million tatu, nikutakie itekelezaji mwema katika hilo"
Joseph alizidi kuchanganyikiwa zaidi asijue kipi cha kufanya. Alirudi akamshirikisha mama yake naye ndo akawa Kama amemzidishia ugonjwa. Ilimbidi auze kibanda chake chote na nguo zote kwa bei ya hasara, akawashirikisha wafanya biashara wenzake wakajichanga changa jumla ikapatikana laki Saba.
Hakuwa na namna nyingine ya kufanya maana ameshamaliza njia zote. Lakini akawaza kwanini asiende kwa kina Doreen kuomba msaada. Mama yake alimkataza akamwambia kuwa utauawa bure huko asije akakanyaga.
Ikiwa imebakia siku moja Joseph alikata shauri japo mama yake alimkataza kwenda. Alipofika getini kwa Kina Doreen mlinzi alimkataza kuingia lakini akafosi kuingia kwa nguvu akafika hadi karibu na mlango wa kuingia sebuleni, mlinzi akaja kumzuia. Wakawa wanafokeana sana kwa sauti.
Joseph:"Unanizuia wakati mimi naleta taarifa muhimu mtoto anaumwa anatakiwa apate matibabu ya haraka na vinginevyo huenda akapoteza maisha wewe Unanizuia!"
Baba Doreen kwa ndani aliisikia sauti ya Joseph na akachukia Sana kwanini amekanyaga nyumbani kwake. Akanyanyuka na kwenda chumbani kwake, akavuta droo na kutoa bastola akajaza risasi akatoka nje na kumkuta Joseph, akamlenga vichwani na kuvuta risasi ammiminie kichwani.

Kama umependezwa na simulizi yangu ya leo weka comment hapo chini au Kama unaswali nitakujibu punde.

KARIBU TENA

Comments

Popular posts from this blog

JINSI YA KUTENGENEZA TAMBI NZURI ZA DENGU

JINSI YA KUANDAA VIUNGO VYA PILAU VYENYE HARUFU NZURI.

JINSI YA KUPIKA MAKANGE YA SAMAKI