MAISHA NI DUARA LEO UKO HAPA KESHO UKO PALE

Kama wewe hupendelei kusoma basi sikiliza audio WAHUSIKA WAKUU
✓Familia ya1
-Joseph
-mama Joseph
-Rose (mdogo wa Joseph)
✓Familia ya Pili
-Doreen
-Baba Doreen
-Mama Doreen
-Josten (Kaka wa Doreen)
-Grace (Housegirl)
NB: Simulizi ina sehemu 7 tu
SEHEM YA 1
Katika mtaa mmoja uliosheheni nyumba zenye hadhi ya kimataifa na gharama Sana kulikuwa pia na kijumba kidogo na dhalili kabisa Cha kina Joseph mwanafunzi wa darasa la Saba aliyekuwa akiishi na mama yake na mdogo wake Rose ambae bado alikuwa Yuko chekechea. Lakini pia kulikuwa na nyumba nzuri mithili ya Kasri ya kifalme aliyekuwa akipatikana binti mrembo Sana mwenye umbo la kuvutia na sura ya kuwaka waka (Doreen) ambae naye pia alikuwa darasa la Saba aliyesoma katika shule za International kuanzia chekechea mpaka shule ya msingi. Nyumbani kwao kulifurika magari mengi ya kifahari kiasi Cha kwamba hata akibeba handbag ya pink basi ataangalia na gari ya pink ili kumetisha.
Basi katika harakati za kimaisha na kupita pita Doreen akajikuta anampenda kijana Joseph bila kutarajia na kumwambia. Doreen aliendelea kukaa kimya na kuficha hisia zake mpaka alipohitimu masomo ya msingi akaanza sekondari katika shule nyingine ya International huku kwa upande wa Joseph alishindwa kuendelea na masomo ingawa alifaulu.
Ni kwa sababu ya kipato tu na yeye kuwa ndio tegemezi kwa mdogo wake na mama yake ambaye alikuwa mgonjwa mara kwa mara. Haikuwa ajabu kwa familia ya kina Joseph kushinda siku nzima bila kula au kula mlo mmoja tu (ugali dagaa uchungu). Hivyo basi ilimlazimu Joseph kwenda kuanza biashara ya kuuza mitumba mjini ili aweze kutimizia haja za familia yake. Siku moja Doreen akaamua kumtolea uvivu Joseph, alimfata hadi kwenye mitumba na akamueleza hisia zake.
Ooh! bahati ilioje kwa masikini Kama mimi Joseph kupendwa na binti mzuri namna hii. (Joseph alijisemea kimoyomoyo). Lakini Joseph akamuuliza,
"hivi imekuwaje kuwaje hadi wewe umenipenda Mimi maana tuna hadhi tofauti za kimaisha, Mimi ni masikini tu na wewe ni tajiri, Sina Cha kukupa fukara Mimi."
Doreen alimtoa wasiwasi kwa kumwambia
""mapenzi hayaangalii hadhi ya mtu, Mimi nimekupenda wewe pamoja na madhaifu yako yote""
Basi Joseph alifarijika na hakusita kumkubalia Doreen, wakaingia katika mahusiano. Penzi jipya mjini la Fukara na binti wa kitajiri lilipamba moto. Siku zote hizo Joseph hakutaka kumfahamisha mama yake Kama yupo katika mahusiano.
Siku moja Doreen akaamua ampe mtaji Joseph ili aangalie biashara nyingine. Joseph aliamua kuachana na mitumba na kufungua duka pamoja na genge pale pale kwao.
Basi ikawa Doreen kila akitoka shule lazima apitie gengeni kwa Joseph kumsabahi na kudeka deka kidogo.
Ikafika hatua Sasa Mama Joseph akahisi kitu na akaamua kumtolea uvivu mwanae.
"Joseph mwanangu naomba nikuulize, hivi huyu binti wa kitajiri namuona anakujaga Mara kwa mara hapa, Kuna nini Kati yenu? " Joseph aliamua kumtoa wasi wasi mama yake kwa kumwambia,
"Ah! Mama hakuna chochote baina yetu ila tu ni mteja wangu wa kudumu huwa anakuja Mara kwa mara"
mama Joseph akamtahadharisha mwanae "naomba uwe makini na kazi isije ikawa mna mahusiano na huyo mtoto sio hadhi yako kabisa, sitaki mahusiano Mimi maana nyinyi vijana?? Haya me siongei Sana"
Basi siku zilikatika wakati Rose akiwa ameshaanza darasa la Kwanza na Kaka yake Joseph akitekeleza majukumu yake ya kumhudumia mdogo wake.
Siku moja Josten aligundua kuwa mdogo wake yupo katika mahusiano na Joseph, alichukia Sana maana mdogo wake alikuwa anatoka kimapenzi na kijana wa kimaskini hivyo basi akaona anaidhalisha familia yao.
Siku moja Joseph akiwa gengeni kwao mara akashangaa kuona Range nyeupe inaingia na kupaki karibu ya genge lake. Mara akashangaa kumuona Josten ndani ya Suti Kali akiwa amekasirika mithili ya numbu akitoka kwenye gari moja kwa moja akaenda gengeni
"Hey! Kijana wa kimaskini mpumbavu mmoja naomba uachane na mdogo wangu leo leo, utaleta laana tu katika familia yetu na usipofanya hivyo nitakuua"
Basi akaondoka kwa jazba akavuta mlango wa gari kwa hasira Kisha akakaa kwenye Range akashusha kioo Cha gari Kisha akamtizama kwa jicho la upande liliojaa hasira akasonya Kisha akapandisha vioo vya gari na kutimua vumbi namna hiyo.
Joseph alifikiria Sana Kisha akaona tu ni ajali kazini hatakiwi kukata tamaa kirahisi hivyo. Hakumshirikisha Doreen Wala mama yake aliamua kukaa kimya tu na kuendeleza mahusiano yao.
Zilipita Kama wiki tatu hivi. Siku moja akiwa ameenda sokoni kufanya manunuzi ya gengeni aliamua kumuacha mdogo wake Rose gengeni kwa Muda. Ghafla ziliingia gari nyingi Sana pale katika uwanja wa kina Joseph kumbe alikuwa ni Josten na watu wake kibao wamefika. Moja kwa moja wakasogea hadi karibu na genge wakashangaa kumuona Rose na sio Joseph. Josten akamuuliza Rose kwa hasira na ukali
"Yupo wapi huyu mwana haram" kwa uwoga kabisa Rose alibaki akitetemeka tu bila kusema chochote. Wakamvuta Rose na kumtoa nje ya genge Kisha wakaanza kuvunja vunja banda na kumwaga mwaga kila kilichopo ili kutia hasara. Kisha wakaingia ndani bila hodi wakamkuta mama Joseph. Josten akaanza kufoka
"Huyu mwana haram wako nilishamkanya kuachana na mdogo wangu hakuniskia, Sasa leo tungemkuta tungemuua nitoe tu Salam za mwisho, Kama ataendelea kutoka na mdogo wangu basi tutakapomkukuta popote pale utaletewa maiti yake, stupid muziishenz!!"
Mama Joseph alidondoka chini ghafla na kuishiwa na nguvu. Josten aliondoka bila kujali chochote kuhusu yule mama.

Kama umependezwa na simulizi yangu ya leo weka comment hapo chini au Kama unaswali nitakujibu punde.

KARIBU TENA

Comments

Post a Comment

Popular posts from this blog

VITU VYA KUFANYA KARIBIA NA MITIHANI.

CHEKA WITH INTERNATIONAL ADMIN

JINSI YA KUANDAA VIUNGO VYA PILAU VYENYE HARUFU NZURI.