MAISHA NI DUARA LEO UKO HAPA KESHO UKO PALE
SEHEMU YA 6
Wakati anataka kufytua risasi mama Doreen akamdaka mkono na ikamkosa ikapiga pembeni. Joseph alichomoka mbio mpaka miguu ikagusa kisogo.
Mama Doreen akamshika mume wake na kuingia nae chumbani.
"Mume wangu, unataka yule mtoto abaki yatima? Em achana nae yule"
Baba Doreen akapunguza jazba Kisha wakarudi sebleni kuangalia Television. Wakati wanaangalia TV mama Doreen akakumbuka maneno ya mwanae kabla hajaondoka kuwa amtunzie mwanae. Basi akaingiwa na wasiwasi kuwa mtoto akifa mwanae akirudi itakuwaje. Basi akaingia chumbani na kubeba kiasi Cha fedha Kisha akatoka na kumuaga mumewe sebleni.
"Mume wangu, natoka kidogo naenda saloon" basi akaruhusiwa na njiani akakutana na Joseph alikuwa hata hajafika mbali maana alikuwa anatembea kwa miguu.
Akapaki gari na kumwita ndani ya gari.
Mama:"Umesema mtoto ana shida gani?" Joseph: "Mtoto anatakiwa kufanyiwa operation utumbo wake umejikunja na amebakisha siku moja tu ambayo ni kesho vinginevyo atapoteza maisha"
Mama: " Operation ni bei gani?" Joseph: "Ni milioni tatu mama angu"
Basi akaingia ndani ya pochi na kumpa milion tatu na nusu kwa ajili ya matibabu. Haraka Sana Joseph alirudi kwa daktari kulipia ili mtoto afanyiwe operation mapema.
Operation kwa mtoto ikafanyika usiku huo huo , Joseph alilala huko huko hospital kwenye bench la wagonjwa. Ilipofika asubuh Joseph alimkimbilia daktari kumuulizia hali ya mtoto.
Lakini daktari akamwambia aendelee kuwa mvumilivu kwani hajaamka bado. Wakakaa hadi saa mbili asubuhi mtoto hajaamka, saa nne mtoto hajaamka, saa kumi na mbili mtoto hajaamka. Daktari akakata tamaa kwa mtoto, akaamua aende kuhakikisha mara ya mwisho Kama bado haamki, akakuta kwa mbali Sana mapigo ya moyo yana dunda.
Akamwambia Joseph, kuwa na amani kila kitu kitakuwa sawa. Basi mtoto akaruhusiwa kutoka hospital baada ya hali yake kuwa nzuri, lakini alipangiwa aina za vyakula vya kuvila pamoja na dawa ambavyo bado vilizidi kumuongezea majukumu Joseph.
Joseph akarudi kwenye biashara yake huku mama yake amepooza mwili mzima kadiri siku zinavyokwenda ndo alivozidi kuwa na hali mbaya. Siku moja wakaja watalii (Mr& Mrs Otto von Admin) kutoka Ujerumani wakahitaji kijana anayeweza kuwaendesha wakati wa utalii kwa siku watamlipa laki moja ila tu awe anajua kuongea kingereza.
Vijana wengi walijitokeza ila kwa kuwa wengi hawajui kingereza basi Joseph akapata bahati maana alikuwaga anaongea na Doreen. Akawa anawatembeza sehem zote walizozihitaji kwa muda wa wiki.
Siku moja waliamua kumuuliza kwanini anaonekana Kama mtu mwenye msongo wa mawazo. Akawaelezea hali ya mama yake ndo inayomfanya awe na stress.
Basi wakamhurumia na kumwambia tu pole. Basi ikafika siku mbili kabla Mr & Mrs Otto von Admin kuondoka . Mrs akaanzisha mada:
"Unajua nimeguswa Sana na changamoto ya yule kijana, halafu nimempenda ni mstaarabu Sana. Kwanini tusimsaidie? "
Basi wakaongea pale wenyewe vizuri na kesho wakamkaribisha katika hoteli ya kifahari Sana. Joseph alipoingia alibaki tu akishangaa shangaa huku na kule maana hajawahi kufika sehemu Kama hiyo tangu azaliwe.
Basi wakaongea pale baadhi ya mambo na kumuuliza, "Hivi kwa mfano ukipewa milioni mia moja sasahivi utafanya nin?" Akajibu:
"Cha Kwanza kabisa nitahakikisha mama angu anapona, na Cha pili nitatanua biashara zangu nifanye biashara nzuri, Kisha nitampeleka mdogo wangu shule nzuri akapate elimu asiwe Kama mimi na pia nitahakikisha mwanangu anaishi mazingira mazuri."
Wakamwambia haya sawa tumekusikia, sisi kesho tunarudi kwetu ujerumani tutaomba utusindikize mpaka Airport.
Kama umependezwa na simulizi yangu ya leo weka comment hapo chini au Kama unaswali nitakujibu punde.
Comments
Post a Comment