MAISHA NI DUARA LEO UKO HAPA KESHO UKO PALE



NAFASI ZA SENSA 2022 www.tamisemi.go.tz JIANDAE KUHESABIWA

Kama wewe hupendelei kusoma sikiliza audio SEHEM YA 2
Baada ya masaa kadhaa Joseph alirudi nyumbani kwao na mizigo yake kabla kuingia ndani alikuta unga umetapakaa ardhini mithili ya mchanga wa beach na vitu vingine vyote viko chini na banda limebomolewa. Akaingia tu ndani kwao huku akiwa mwenye mshangao Kama rubani aliyepoteza mawasiliano akashangaa kumkuta mama yake ana hali mbaya sana na mdogo wake Rose akimpepea. Akashindwa hata asijue la kufanya akabaki tu kumuuliza Rose
"Kimetokea nini?" Rose alimkata jicho tu Kaka yake bila kumwambia chochote basi ikabidi tu naye ajumuike kumuuguza mama pale kwa muda huku hata haelewi kilichotokea.
Ikafika jioni hali ya mama ikawa nafuu kidogo ndipo mama alipoanza kuongea.
"Rose mwanangu, naomba utupishe kidogo nina maongezi na Kaka yako!" Rose akawaacha wafanye mazungumzo:
""Joseph mwanangu, yote haya yasingetokea sama na wewe, na Leo hii laiti Kama ungekuwepo hapa wakati ule basi usingekuwepo duniani kabisa. Hivi kwanini lakini Joseph unataka utuache katika hali gani??""" (Huku akilia)
Joseph: "Mama ni Kama bado sijakupata vizuri nini unamaanisha unaongea kwa mafumbo tata Sana, sijaelewa mama angu.
Mama akamjibu "Unajifanya huelewi utanielewa tu, nilishakuonya mapema sana kuhusu mahusiano na binti yule wa kitajiri ukanidanganya ni mteja wako, leo hii Kaka yake amekuja na kundi kubwa la watu walitaka kukuua bahati nzuri haukuwepo ndo wakafanya hayo uliyoyakuta. Sasa Kama Mimi kweli mama yako mzazi naomba uachane na Doreen au Uendelee na Doreen uachane na mimi. Nimemaliza na usiku mwema"" mama akainuka na kuingia ndani, Joseph aliingia ndani akichanganyikiwa hajui la kufanya mama anamtaka na Doreen hayuko tayari kumpoteza. Basi ilifika hadi saa nane usiku hajalala anawaza tu, ghafla akasikia hodi mlangoni kwake. Akauliza ni nani wewe (sauti ikasikika)
"Fungua tu utanijua hapo hapo " Joseph akafungua mlango na alishangaaa kumkuta mdogo wake Rose " Najua tu Kama hadi sasaivi haujalala unafikiria Kati ya mama au Wifi Doreen, mda ule mama alivyonambia niondoke nilijificha pembeni na nikawasikia yote mliyokuwa mkiongea. Najua unampenda Sana Doreen, Mimi nipo na wewe bega kwa bega Kaka mwanzo mpaka mwisho" akamfata Kaka yake wakakumbatiana na kufarijiana mpaka asubuhi

Kama umependezwa na simulizi yangu ya leo weka comment hapo chini au Kama unaswali nitakujibu punde.

KARIBU TENA

Comments

Popular posts from this blog

VITU VYA KUFANYA KARIBIA NA MITIHANI.

CHEKA WITH INTERNATIONAL ADMIN

JINSI YA KUANDAA VIUNGO VYA PILAU VYENYE HARUFU NZURI.