MAISHA NI DUARA LEO UKO HAPA KESHO UKO PALE



NAFASI ZA SENSA 2022 www.tamisemi.go.tz JIANDAE KUHESABIWA

Kama wewe hupendelei kusoma sikiliza audio SEHEM YA 3
Mara baada ya kupambazuka Joseph aliamua kumtumia Doreen message akimuomba waonane. Basi jioni ikafika na Joseph alionana na Doreen wakatembea umbali wa Kilometer mbili bila kuongeleshana chochote, wakafika katika daraja Joseph akasimama na kumwambia Doreen.
" Nataka niku suprize!" Doreen akafurahi Sana lakini Joseph hakuonesha kuwa mwenye furaha. Joseph kwa upole kabisa
"I love you So much Doreen" Doreen akamjibu "I know that sweetheart, ooh Leo umeniamulia uniongelee kimombo baby "(huku akicheka) Joseph
"Ah! Si unajua tena nimekaa na wewe Sana kwahiyo saivi kizungu hakinipigi chenga". Joseph akaendelea kusema
"Unajua katika maisha Classes is inevitable (matabaka hayakwepeki) , wewe ni binti wa kitajiri Sana Doreen, haustahili kuwa na mtu Kama Mimi. Mimi ni fukara siwezi kuwa na wewe" Doreen akamuwahi "Joseph nilishakukataza hizo kauli Mimi sizipendi, nimekupenda wewe na sijakupendea vitu"
Joseph :"Nalitambua hilo Doreen lakini imefikia hatua Kaka yako Josten anataka kuniua Mimi na amekuja nyumbani kwetu amefanya uharibifu mkubwa Sana wa genge langu na kutaka kuniua nashkuru mungu nilikuwa nimetoka kidogo, hivi ninavyoongea mama bado hali yake mbaya kisa tu mahusiano yangu na yako. Jana sijalala mama amenitaka nichague kuendelea nayeye au niendelee na wewe nimuache mama. I have no option anymore Doreen (Sina chaguo tena) japo naumia kwa sababu nakupenda Sana na Sina budi kukuacha, ahsante kwa kila kitu ulichonifanyia na Kama nilikukwaza kwa namna yoyote naomba unisamehe Sana. Ila ninachotaka kuku suprize Leo ni kuwa kuanzia hivi nitakapogeuka nyuma, Mimi na wewe itabaki story tu, siwezi kuhatarisha maisha yangu na kwa familia yangu nakupenda Sana Doreen na acha tu niseme Good luck nakutakia maisha mema. "
Joseph akaanza kuondoka Doreen hakuamini anachokisikia na anacho kiona, akabaki tu kuita "Joseph! Joseph! Joe! Joe!Joeeeee!" (Huku akilia bila ya Joseph kurudi nyuma). Hakuamini kilichomkuta naye akarudi kwao. Joseph aliamua kurudi kwenye biashara yake ya awali ya kuuza mitumba barabarani, lakini siku zote hizo Doreen alikuwa akimuomba basi walau alale nae hata mara moja maana walikuwa hawajawahi kulala tangu wameanza mahusiano. Lakini Joseph alikataa kata kata, ikapita Kama miezi miwili hivi bado Doreen akimsumbua Joseph kuhusu swala la kulala nae. Wahenga wanasemaga MTOTO AKILILIA WEMBE, MPE UMKATE NYWELE ZIMEMUOTA.
Basi Joseph ikabidi ampe Doreen kile alichokihitaji na baada ya hapo Doreen hakumtafuta tena Joseph na mawasiliano wakakata.
Basi ilipita Kama mwezi mmoja ivi na wiki kadhaa mama Doreen, Doreen na Grace wakiwa dinning wanakula. Ghafla Doreen akanyanyuka na kukimbilia kwenye sink Kama mwenye kutaka kutapika flani ivi Kisha akarudi kuendelea kula. Mama ake akamuuliza
"what's wrong my daughter??" (Una shida gani binti yangu) Doreen akamjibu "Am okay Mom" basi akaendelea kula Kama tonge tano ivi tena akakimbilia kwenye sink na kutapika Kisha akarudi kuendelea kula. Mama ake akamuuliza tena,
"una shida gani Doreen?" Doreen akamjibu yupo sawa. Lakini mama safari hii hakuridhika na majibu, "I Know my daughter very well, shida nini binti yangu!! Eenh come on Doreen" (Kwa upole kabisa) Doreen akaanza kulia mama ake huku akimbembeleza.
Doreen: "Mom, najua mnatumia pesa nyingi Sana kunisomesha! Mnanipenda Sana na sijawahi kukukosea mom, naomba unisamehe Mimi nimeteleza katika hili" (huku machozi yakimbubujika) mama akachanganyikiwa Sana: "kwahiyo Doreen, u-natak-a ku-ku-sema wewe ni..." Hapo hapo mama akadondoka chini ghafla na Josten anaingia ndani anakuta mama ndo ameanguka.
Josten:"what happened to mom! What happened??" (Kwa kupaniki Sana) Basi akaamua kuita Houseboy waje wamsaidie mama kumuuingiza ndani ya gari, wakati wanatoka getini baba nae anaingia..anakuta watu wanatoka lakini hawapo sawa.
Baba "Hey Jay, what happened??" Josten: "Mama ameanguka ghafla bila sababu ndo tunampeleka hospital."
Baba:"Okay basi tangulieni me ngoja nibadilishe gari nakuja soon" (kwa kupaniki) Basi mama Doreen akawahishwa hospital kwa haraka na kila mtu alikaa akimuombea kwa nafasi yake. Baada ya muda kadhaa daktari akawaruhusu kumuona mgonjwa kwani alikuwa ananafuu. Baba alianza kuingia ndani haraka haraka
" My heartbeat colonizer, unaendeleaje" kwa mapozi kabisa na sauti ya puani mama alijibu "Naendelea vizuri sultan wangu, pole na kazi"
Baba:"Ahsante Sana malkia wangu wa nguvu, vipi ni kipi kilikusibu."
Mama:"Oh! Yaani we acha tu, Kwanza kabla ya yote naomba umchukue Doreen nenda nae kwa daktari akampime mimba." Baba alishangaaa ila hakusema chochote zaidi ya kufata Kama alivyoambiwa na mkewe. Doreen akachkuliwa na kupimwa ujauzito.

Kama umependezwa na simulizi yangu ya leo weka comment hapo chini au Kama unaswali nitakujibu punde.

KARIBU TENA

Comments

Post a Comment

Popular posts from this blog

VITU VYA KUFANYA KARIBIA NA MITIHANI.

CHEKA WITH INTERNATIONAL ADMIN

JINSI YA KUANDAA VIUNGO VYA PILAU VYENYE HARUFU NZURI.