Posts

Showing posts from February, 2022

NAMNA YA KUWEKA BAJETI

50% ya kipato chako iweke kwa ajili ya matumizi yako ya Kila siku Kama chakula, mavazi, umeme, Kodi, maji n.k Watu wengi huwa wanajipunja Sana hapa na ndo mana unaishi kwa kujitesa. Kama unaingiza 1M basi laki tano itenge kwa ajili ya hayo mahitaji muhimu ya mara kwa mara Kama vile chakula, umeme, Kodi, nauli na mavazi. Watu wengi wakipata fedha wanaweka akiba yote na kusahau kuwa Kuna vitu wanavihitaji kila siku, si ajabu kukuta mtu ameweka akiba na bado amekopa madeni mengi tu kwa ajili ya chakula. Hapa utawasikikia watu mimi siwezi kuweka akiba bwana , kila nikiweka naila! wanasahau kwamba hutakiwi kuweka pesa yote unayoipata kama akiba kwa sababu itakushinda tu, utahitaji kula utaanza kula akiba. Tunatafuta pesa ili tujikimu kimaisha na sio kujitesa kimaisha. Lakini kumbuka kuweka nusu tu ya kipato chako kwenye mahitaji muhimu 30% ya kipato chako itenge kwa ajili ya matakwa yako (your wants) mfano: unataka kununua gari, unataka kutoka out, unataka kumfanyia mtu surp

MAMBO YA KUYAACHA ILI UFANIKIWE

1.KUACHA KUSIKILIZA WATU WANAOKUKATISHA TAMAA Watu wakukukatisha tamaa hawawezi kukosekana yawezekana ni familia yako, ndugu zako, mpenzi wako, rafiki yako, walimu wako, wafanyakazi mwenzako, jirani zako Kama anakukatisha tamaa usimsikilize Kuna watu wao Kila siku wapo kukatisha watu tamaa tu na kama ikitokea umeanguka kidogo utasikia si unaona nilisema Mimi hukuniskiliza, Mimi najua... basi hapo kwake furaha tele akiona na wewe kweli umekata tamaa. 2.KUACHA KUJILAUMU KWA MAKOSA YA NYUMA Kuna watu kwa sababu tu alishafanya kosa fulani katika maisha yake basi ndo atajihukumu hadi anaingia kaburini, Mimi nilifanya iki jamani labda ndo sababu n.k hata mungu husamehe na kupotezea makosa. Wewe sio mkosaji Kama Farao hupaswi kujilaumu kwa makosa uliyofanya yakakupelekea kufeli. 3.KUACHA KUJIDHARAU Ukijidharau wewe mwenyewe nani atakaekuamini? Hayupo jikubali na usijishushe. Jiamini katika unachokifanya wewe sio wakuwa chini siku zote. 4.KUKAA KWA MUDA MREFU BILA KUFANYA MAAMUZI K

SEHEMU 9 ZITAKAZOKUFANYA UWE MILLIONAIRE

Image
International Admin 1. HUDUMA ZA KIFEDHA (financial services) Hapa unaweza kufanya huduma mbalimbali Kama vile za kibenki, uwakala wa mitandao ya simu na bank, mikopo,makampuni ya bima n.k watu wengi hujipatia fedha kupitia mifumo hiyo Kama uwakala hakikisha unalenga eneo linalokuwa na mjongeo wa watu wengi Kama vile barabarani, vyuoni,n.k Unaweza kwenda kufungua bonus account kwa NMB bank kima Cha chini ni elfu hamsini yani hizo bonus account wewe unakuwa unaiacha pesa yako kwa miezi kuanzia 3 bila kuitoa ila wanakuwa wanakulipa kwa ongezeko la asilimia fulani kwa mwezi kadri unavoiacha. Kwa hiyo utalipwa kutokana na kiwango Cha pesa zako wanakuwa na % za kugawa faida. Au unaweza kununua hisa (shares) kwa wale wasioelewa hisa naomba niwatolee mfano: Mimi na marafiki zangu 3 tunaanzisha kampuni mtaji ulotumika elfu kumi, mimi nimetoa elfu 5 mmoja katoa elfu 3 na mwingine elfu mbili kwahiyo mgawanyo wetu wa umiliki wa ile kampuni Mimi nitamiliki 50% mwingine ata

CHEKA WITH INTERNATIONAL ADMIN

Image
VIDEO ZA VICHEKESHO NGUMI ZA KIMATAIFA 😂 MTOTO WA KITANGA 😂 UKOME KULA KWA WATU 😂 VITUKO VYA PUNGASESE😂 HUYU JAMAA NOMA SANA 😂 KUMBE WAKINA HANSCANA WANAPATA SHIDA HAWASEMI 😂 UTAPENDA NGUMI ZA WAPENDANAO 😂 UTAPENDA BARAKOA ZA WAPENDA KULA 😂 SARAKASI ZA MASHA LOVE 😂 kILICHOMKUTA JINI LA BUZA NJOO NIKUAGE 😂😂 MIMI SI WAKO 😂 WAPEMBA NOMA😂 BINTI ANAVOONESHA JEURI YA BOOM UNAUNGUZA KUKU?? 😂 SaBINA 😂 MAPAMBIO YANANOGA 😂 SALAMA KAIKUBALI 😂 GOOOOO! 😂 UTAPENDA KIBONGE ANAVOCHEZA 😂 HUYU DOGO ANABALAA 😂😂 DOGO ANAJUA 😂 HASIRA ZA KIHEHE 😂 HII MICHEZO HII 😂 HII ENGLISH 😂 KUMBE NDO MAMBO YENU MKIWA GYM 😂 20. 😂😂 HIZI MOVIE ZA WAHINDI SITAKI TENA 😂 BABA JUMA NA MTIHANI WA HESABU Baba juma alikaa kwa kutulia sebuleni akisoma gazeti mara ghafla mwanae juma anakuja na mtihani wa hesabu umeandikwa sifuri. Bila kuchelewesha akaanza kumpiga ngumi na mateke Baba Juma: Pumbavu mkubwa wewe unakuwa Kama jini mauno, yani Mimi

LIFE STAR

Image
International Admin Maisha ni Kama nyota unayoiona juu angani ili ufurahie maisha inabidi uwe na pembe tano Kama nyota. Utaweza kuyafurahia maisha yako kwa amani na raha kama utazingatia pembe tano zifuatazo za maisha yako. 1. MUNGU Haimaanishi Sasa uanze kukesha msikitini/kanisani ndo utakuwa karibu na mungu bali mshirikishe mungu katika chochote unachofanya maana hata mchawi humuomba mungu "eh mwenyezi mungu nijaalie nifanikiwe kumroga fulani" mda mwingine mambo yetu hayaendi kwa sababu hatumtegemei mwenyezi mungu. Kama mwenyezi mungu anasaidia waja wake wa aina zote wachamungu, washirikina, wahalifu. Iweje ashindwe kukusaidia pale utakapo muomba? Tumtegemee mwenyezi mungu kwa kila kitu tunachokifanya. 2. PESA Utashindwa kufanya chochote unachokitaka kukifanya kama hauna pesa, badala yake utaishia kutamani tu " dah! natamani ningekuwa na hela ningesaidia familia yangu, ningesaidia masikini, ningefanya...n.k." (hauwezi kutoa

JINSI YA KUTENGENEZA SABUNI YA MAJI

Image
International Admin MAHITAJI •Sulphonic acid (salfonik asid) •Soda Ash •Gryserine •Perfume (pafyum) • Rangi •Slace • Chumvi ya mawe •Formalin (fomalin) •Alka VIFAA ✓Kikombe Cha Lita moja ✓Kijiko Cha chakula ✓Beseni ✓Ndoo ya Lita 20 tupu ✓Maji Lita 20 HATUA 1. Mimina maji lita moja kwenye beseni 2. Ongeza nusu Lita ya sulphonic acid 3. Ongeza slace nusu 4. Weka soda ash nusu HALAF KOROGA UPANDE MMOJA (Yani Kama utaanza kukoroga kwenda kushoto basi mwanzo mwisho utakoroga upande huo huo) 5.Weka chumvi ya mawe nusu (halaf koroga) 6. Changanya Alka nusu na maji lita tano pembeni (halaf mimina kwenye mchanganyiko na koroga upande ule ule ulioanza nao) 7. Weka Formalin vijiko vinne 8. Chukua rangi kijiko kimoja koroga pembeni halaf mimina kwenye mchanganyiko 9. Weka perfume vijiko 2 au 3 halafu KOROGA (perfume utanunua harufu uipendayo na hizi sio za kujipulizia mwilini) NB Kazi ya gryserine hii inawekwa ili kuua bacteria

SABABU ZITAKAZO FANYA UCHELEWE KUFIKA KATIKA MAFANIKIO

KUPENDA RAHA Kuna watu hawapedi kujitesa wanapenda raha sana kula bata sana wanasahau Kama wanatakiwa kupamba wawe na uchumi mzuri. Kwa hali hii utakesha ukitafuta mafanikio KUGHAIRISHA MAMBO. Kila Jambo analolipanga anaghairisha unasema utaanza kesho utaanza kuwa serious kesho utafanya hiki badae. Unaamka unasema utafanya hiki leo unajikuta hujafanya unahamishia kesho hivo hivo mpaka Leo una viporo vya mambo mengi ambayo haukuyafanya bado. MIPANGO MINGI BILA HATUA. Kuna watu wakichukua notebook zao na madaftari wakaanza kukusimulia mipango yao yani utavutiwa na kusema safi sana lakini hakuna hatua yoyote wanayoichukua kuyafanyia kazi mawazo yao. Hivyo basi usiwe mtu wa namna hii mipango mingi Matendo machache. KUSOMA BILA KUELIMIKA. Kuna watu wamesoma lakini wanashindwa kutumia elimu yao kuiishi katika maisha yao. Wewe umeenda kujifunza kutengeneza kitu fulani lakini utabaki tu kusimulia nilienda kufundishwa kutengeneza cake Mimi na hautaki

HASARA ZA MITANDAO

Image
International Admin Hakuna chenye faida kikakosa hasara. Mitandao ina hasara zake nyingi hivyo Kila mtu inampasa kuziangalia kwa jicho la tatu. KUINGILIA FARAGHA Kupitia mitandao watu wanaingilia faragha za watu kwa kuchukua au kutizama taarifa zako bila idhini yako. Kwa jina la kitaalam wanaitwa Hackers, lakini pia mtu anaweza akarusha maudhui ya faragha ambayo yanaingilia faragha ya mtu kwa jina la kimtaani wanaita Connection . Napenda nikushauri kutoweka taarifa zako binafsi kwenye mitandao ya kijamii maana ni faragha yako.watu wengi hawajui kuwa hata mwaka na tarehe ya kuzaliwa ni faragha. UDANGANYIFU NA UTAPELI Watu wengi wamelia mitandaoni watu wanatangaza biashara unaipenda unalipia hupati bidhaa. Wengine wanajifanya wako nje ya nchi wanaleta bidhaa kwa bei rahisi mfano anaweza kuigiza yeye ni mhindi kumbe ni mtanzania yuko Buza amekaa anaandaa matangazo ya kutapeli watu. Lakini hata matumizi ya application mbalimbali Kama vile Snapchat n.k zin

ZIJUE FAIDA ZA MITANDAO

Image
International Admin. Huwezi kuona faida za mitandao Kama yenyewe ndio chanzo kikubwa Cha kukumalizia bando. Unaweza kutumia mitandao Kama ifuatavyo KUJIPATIA ELIMU. Watu wengi wanaingia YouTube , Facebook, Instagram, Google, Twitter, n.k kupata elimu za vitu mbalimbali Kama vile taaluma, mapishi, mavazi, biashara, mahusiano,kushona, ubunifu, teknolojia n.k CHANZO CHA KIPATO wanatumia mitandao Kama Facebook, YouTube, Instagram, Twitter, na michezo mbalimbali mtandaoni kujipatia kipato. Ukiwekeza katika mtandao utaona matunda yake yapo inahitaji uvumilivu kidogo. KURAHISISHA MAWASILIANO Leo hii mtu aliyoko China anaweza kuwasiliana na mtu aliyoko Tanzania moja kwa moja ndani ya muda mfupi. Watu hufikisha taarifa kwa watu wengi walengwa ndani ya muda mfupi kupitia makundi mbalimbali ya mitandaoni Kama makundi ya WhatsApp na Facebook. BURUDANI Kila aina ya burudani utakayoihitaji ipo mtandaoni, wewe Kama ni mpenda mziki, tamthilia, katuni, viche