SABABU ZITAKAZO FANYA UCHELEWE KUFIKA KATIKA MAFANIKIO

KUPENDA RAHA
Kuna watu hawapedi kujitesa wanapenda raha sana kula bata sana wanasahau Kama wanatakiwa kupamba wawe na uchumi mzuri. Kwa hali hii utakesha ukitafuta mafanikio

KUGHAIRISHA MAMBO.
Kila Jambo analolipanga anaghairisha unasema utaanza kesho utaanza kuwa serious kesho utafanya hiki badae. Unaamka unasema utafanya hiki leo unajikuta hujafanya unahamishia kesho hivo hivo mpaka Leo una viporo vya mambo mengi ambayo haukuyafanya bado.

MIPANGO MINGI BILA HATUA.
Kuna watu wakichukua notebook zao na madaftari wakaanza kukusimulia mipango yao yani utavutiwa na kusema safi sana lakini hakuna hatua yoyote wanayoichukua kuyafanyia kazi mawazo yao. Hivyo basi usiwe mtu wa namna hii mipango mingi Matendo machache.

KUSOMA BILA KUELIMIKA.
Kuna watu wamesoma lakini wanashindwa kutumia elimu yao kuiishi katika maisha yao. Wewe umeenda kujifunza kutengeneza kitu fulani lakini utabaki tu kusimulia
nilienda kufundishwa kutengeneza cake Mimi na hautaki kujaribu hata kidogo tangu umefundishwa.
hawatakua sawa yule anaejua na asiyejua, wakiwa sawa basi wewe unaejua unakuwa umesoma tu Ila hujaelimika

KUTILIA MANANI MANENO YA WATU
wanavyokuzungumzia vibaya Mda mwingine familia, ndugu, jamaa , marafiki na jirani wanaweza kukuzungumzia vibaya ili ukate tamaa na ukisema uwafatishe ndo unapotea kabisa. Utaskia biashara ya nguo wewe sasaivi hailipi kabisa utatupa pesa zako bure, wewe hunioni mimi nimerudisha frem anataka kujifananisha yeye na wewe . Hapa duniani huwezi kuwa sawa na mwingine wakati unalalamika biashara fulani ina hasara Sana na mda huo huo Kuna mtu ina mlipa Sana. Kwa hiyo tafuta wapi unapokosea ujirekebishe lakini usiache kufanya Jambo. YEYE SIO WEWE Kuna usemi napendaga sana kuutumia "Hautofika safari yako ikiwa wewe ni mtu wa kutupa mawe njiani kwa Kila mbwa anaye kumbwekea, wengine hawana meno wana bweka tu ili usijue kuwa hawana uwezo wa kung'ata"

Kama umependeza somo langu la leo weka comment hapo chini au Kama unaswali nitakujibu punde.

KARIBU TENA

Comments

Popular posts from this blog

VITU VYA KUFANYA KARIBIA NA MITIHANI.

CHEKA WITH INTERNATIONAL ADMIN

JINSI YA KUANDAA VIUNGO VYA PILAU VYENYE HARUFU NZURI.