SEHEMU 9 ZITAKAZOKUFANYA UWE MILLIONAIRE


International Admin

1. HUDUMA ZA KIFEDHA (financial services)
Hapa unaweza kufanya huduma mbalimbali Kama vile za kibenki, uwakala wa mitandao ya simu na bank, mikopo,makampuni ya bima n.k watu wengi hujipatia fedha kupitia mifumo hiyo Kama uwakala hakikisha unalenga eneo linalokuwa na mjongeo wa watu wengi Kama vile barabarani, vyuoni,n.k Unaweza kwenda kufungua bonus account kwa NMB bank kima Cha chini ni elfu hamsini yani hizo bonus account wewe unakuwa unaiacha pesa yako kwa miezi kuanzia 3 bila kuitoa ila wanakuwa wanakulipa kwa ongezeko la asilimia fulani kwa mwezi kadri unavoiacha. Kwa hiyo utalipwa kutokana na kiwango Cha pesa zako wanakuwa na % za kugawa faida. Au unaweza kununua hisa (shares)kwa wale wasioelewa hisa naomba niwatolee mfano:
Mimi na marafiki zangu 3 tunaanzisha kampuni mtaji ulotumika elfu kumi, mimi nimetoa elfu 5 mmoja katoa elfu 3 na mwingine elfu mbili kwahiyo mgawanyo wetu wa umiliki wa ile kampuni Mimi nitamiliki 50% mwingine atamiliki 30% na mwingine 20% kwa hiyo Kama tukiamua kufanya kila Tsh.500 iwe sawasawa na hisa moja kwa hiyo Mimi nitakuwa na hisa10 katika ile kampuni. Sasa Kama watu watahitaji kuongezeka basi atanunua kila hisa kwa Tsh.500/= na faida ikipatikana atalipwa kulingana na idadi ya hisa zake. Mwenye hisa nyingi atapata faida kubwa Kwa hiyo Kuna makampuni hapa Tanzania yanauza hisa na watu wanayatumia Kama sehemu ya kuwekeza pesa zao mfano UTT Amis, DCB bank, JATU Kwahiyo badala ya kuweka tu hela zako zote bank zikawa zimekaa tu na kuambulia makato bora kuwekeza pia kwenye makampuni ya hisa lakini pia usiweke zote maana Kama ikitokea bei ya hisa ikashuka utakuwa umeingia hasara. Lakini wengine wananunua hisa. Labda Kama umenunua hisa 10 kwa elfu 6 unavizia tu zikipanda bei maana zinakuwa zinapanda Mara nyingi labda nangoja zifike hisa moja kwa 1000 nikiuza nitakuwa na hisa elfu 10 wanasema money is in the money (pesa iko ndani ya pesa)

2. UBUNIFU (Technology)
Teknolojia ni ubunifu wa kutambua tatizo na kulifanyia kazi. Watu wengi wanadhani ni kutengeneza magari ,kompyuta na marobot tu ndio teknolojia laahasha hata aliyegundua watu wanapata shida njiani wakishikwa na kiu akaanzisha maji ya kandoro na vinywaji vya njiani ni teknolojia hiyo. Kwahiyo angalia unaona changamoto gani na utaitatua kwa njia gani hapo utakuwa tayari unajiingizia pesa kwa sababu umetatua changamoto za watu. Kama unaweza kugundua au kutengeneza mifumo mbalimbali mfano Mark Zuckerberg alivyogundua Facebook, Bilgate alivogundua Microsoft, kutengeneza vitu mbalimbali usiache hiyo ndio teknolojia na wanasemaga wenzetu teknolojia yao ipo juu kwa sababu wanazidi kutatua matatizo ya watu Kama kugundua simu kwa mawasiliano, mitandao ya kijamii, magari ,maroboti, kwa hiyo na wewe una kitu Cha kuisaidia jamii, sio lazima ufikirie mambo makubwa Sana hata choo Cha njian utakuwa unajizolea pesa

3. HUDUMA ZA AFYA (Health Services)
Sidhani Kama Kuna mtu anapenda kufa jamani mtu akiumwa tu kidogo huyo anaanza kuhangaika na madawa. Kwa hiyo unaweza kuanzisha hospital, dispensary, pharmacy hata mtaani,au ukawa unauza viti vya walemavu,n.k na hapo utapata wateja maana kila siku watu wanaumwa ,pia unaweza kutoa elimu kuhusu afya Kama wewe umebobea kwenye maswala ya afya kupitia mitandao ya kijamii na ukajiingizia fedha.

4. ARDHI NA UJENZI (Real estate and construction)
Wekeza katika ardhi, kadri siku zinavozidi kwenda ardhi inazidi kupanda bei itafikia hatua wajukuu zetu huko watashindwa kumiliki ardhi kwa kununua watakodi tu Kama China hakuna pakujenga watu wanakodi hewa anaongeza ghorofa anaishi na analipa Kodi. Nyinyi wenyewe mashahidi zamani kupanga chumba au nyumbani ilikuwa nafuu kuliko sasa. Kama una pesa unaweza kujenga nyumba ukapangisha na kila mwezi ukajiingia pesa nzuri, unaweza ukaanzisha kilimo katika ardhi yako ukapata mkwanja na ardhi bado ikawa ya kwako, unaweza kupanda miti ya mbao baada ya miaka 7-10 ukauza kwa mamilion ya pesa. Huu ndo uwekezaji wa muda mrefu na utakaokutoa na pia utasaidia kutunza hewa ya Oxygen, ivi ushawahi kufikiria Kama ulijaaliwa kumiliki ardhi labda ulipewa, kununua au kwa urithi ukiwa na miaka 15 ukaamua kupanda miti ya mbao mpaka ukiwa na 25 ukishauza tayari unakuwa umeshafanikiwa vizuri. Hapa vijana wengi tunashindwa kufikiria maana tunatoka faida ya hapo hapo na ndo mana tunapata shida Sana hata badae tutakuwa watu wakuhangaika kutafuta pesa .Katika maisha lazima uwe na mipango ya muda mrefu na ya muda mfupi ili kukidhi maisha ya kila siku. Vijana wengi huwa hatutaki kuwekeza uwekezaji wa muda mrefu, tunataka pesa za mkupuo tunazipata na zinashida Mara moja. Yote kwa yote naomba tuwekeze sana katika ardhi maana hii ni rasilimali kubwa sana katika nchi yoyote. Waingereza wanasema The Country which destroy her soil, destroy herself (Nchi inayoharibu udongo wake inajiharibu yenyewe )

5. ELIMU (Education)
Unaweza kuwa mwalimu ukawa unajiingizia kipato kwa kutumia elimu uliyo nayo, Kama Mimi hapa ni mwanachuo lakin ninapokuwa likizo natumia elimu yangu kufundisha tution wanafunzi sekondari na msingi najipatia pesa. Lakini unaweza kufungua tution ukakubalika Kama kina Mgote, Ali Abdallah, Ngaiza, Josephat (kwa upande wa Dar es salaam) au ukawa unauza material ya elimu, au ukatengeneza au ukagharamikia kutengeneza platform za wanafunzi kusoma online na kila wakizitumia watu unapata pesa, au ukafundisha useremala, make up, cake, kushona n.k ukapata hela jaman ujuzi ulionao wowote ule ni pesa tumia ukuingizie pesa Kama mnakumbuka pale kweny life star

6. BURUDANI (Entertainment and recreation)
Hakuna asiependa burudani Kuna watu wanapenda kusikiliza masimulizi,kusoma hadithi, kusikiliza muziki, kuchekesha,kuwa MC, kuwa mchezaji mpira Kama Feitoto, Morrison,samata, kuwa mwimbaji kaswida au injili Yani kila mtu anapenda Cha kwake na huwezi kukosa mashabiki maana watu tupo wengi Sana. Kuna watu wanapenda kuigiza, lakini pia Kama wewe ni mtaalamu wa computer unaweza kutengeneza games, movie's, animation, production na effects mbalimbali kwahiyo ni wewe na utatuburudishaje ili upate pesa

7. USAFIRISHAJI (Transportation)
Unaweza miliki vyombo vya Moto au majini, au ukawa mbunifu Kama Uber na bolt Yani ni wewe tu mfano Abood na mabasi yake , Azam ana boti zake n.k Yan hutakiwi kufikiria malengo madogo tu yaani uishie kuwa boda boda tu jaman hatutofika. Yani Kuna watu hapa hata hawajawahi kufikiria kumiliki kuanzia 100Million, kampuni zao, yeye anawaza akipata ugali tu kushnehi hapana tubadilike na watu wenye hela wote walipoelezeaga malengo yao watu waliwacheka sana na kuona kuwa hayatawezekana lakini sasaivi ndo wanaelewa kuwa inawezekana. Mimi nitafurahi Sana huko badae humu ndan ya blog yangu kuona kuna watu waliyafanyia kazi haya wakawa mamilionaire, Billionaire. Kuanzia leo ANZA KUFIKIRIA MAMBO MAKUBWA kwa sababu huwezi ukatenda nje ya vile unavofikiria kichwani

8. NISHATI (Energy)
Unaweza kufungua sheli ya mafuta au gas Kama sasaivi magari ya gas yashaanza kuwa mengi, unaweza kuuza mitungi ya gas, solar power, ukauza taa za solar au vifaa vya solar n.k

9. CHAKULA (Food)
Kila siku watu wanakula na ndo Mana mwenye genge kwa siku ataingiza pesa kuliko mwenye duka maana watu wanakula kila siku kuliko kununua kiberiti na mshumaa. Unaweza kufungua hotel, restaurant, cafeteria,hata mama ntilie kwa kuanzia sio mbaya. Unaweza ukawa unauza nafaka na vinywaji mbalimbali n.k
✓Mwisho kabisa naomba niseme hizo zote ndo sehemu zilizowatoa watu wengi duniani na hata matajiri wa dunia
NB:
Be the right person in the right industry ( kuwa mtu sahihi katika kiwanda sahihi) Usibake fani angalia wapi wewe utaweza na sio lazima ufanye vyote.

Kama umependeza somo langu la leo weka comment hapo chini au Kama unaswali nitakujibu punde.

KARIBU TENA

Comments

Post a Comment

Popular posts from this blog

VITU VYA KUFANYA KARIBIA NA MITIHANI.

CHEKA WITH INTERNATIONAL ADMIN

JINSI YA KUANDAA VIUNGO VYA PILAU VYENYE HARUFU NZURI.