JINSI YA KUTENGENEZA SABUNI YA MAJI
MAHITAJI
•Sulphonic acid (salfonik asid)
•Soda Ash
•Gryserine
•Perfume (pafyum)
• Rangi
•Slace
• Chumvi ya mawe
•Formalin (fomalin)
•Alka
VIFAA
✓Kikombe Cha Lita moja
✓Kijiko Cha chakula
✓Beseni
✓Ndoo ya Lita 20 tupu
✓Maji Lita 20
HATUA
1. Mimina maji lita moja kwenye beseni
2. Ongeza nusu Lita ya sulphonic acid
3. Ongeza slace nusu
4. Weka soda ash nusu HALAF KOROGA UPANDE MMOJA (Yani Kama utaanza kukoroga kwenda kushoto basi mwanzo mwisho utakoroga upande huo huo)
5.Weka chumvi ya mawe nusu (halaf koroga)
6. Changanya Alka nusu na maji lita tano pembeni (halaf mimina kwenye mchanganyiko na koroga upande ule ule ulioanza nao)
7. Weka Formalin vijiko vinne
8. Chukua rangi kijiko kimoja koroga pembeni halaf mimina kwenye mchanganyiko
9. Weka perfume vijiko 2 au 3 halafu KOROGA (perfume utanunua harufu uipendayo na hizi sio za kujipulizia mwilini)
NB
Kazi ya gryserine hii inawekwa ili kuua bacteria
Vifaa utavipata katika maduka ya malighafi
Kama umependeza somo langu la leo weka comment hapo chini au Kama unaswali nitakujibu punde.
Comments
Post a Comment