MAMBO YA KUYAACHA ILI UFANIKIWE

1.KUACHA KUSIKILIZA WATU WANAOKUKATISHA TAMAA
Watu wakukukatisha tamaa hawawezi kukosekana yawezekana ni familia yako, ndugu zako, mpenzi wako, rafiki yako, walimu wako, wafanyakazi mwenzako, jirani zako Kama anakukatisha tamaa usimsikilize Kuna watu wao Kila siku wapo kukatisha watu tamaa tu na kama ikitokea umeanguka kidogo utasikia si unaona nilisema Mimi hukuniskiliza, Mimi najua... basi hapo kwake furaha tele akiona na wewe kweli umekata tamaa.

2.KUACHA KUJILAUMU KWA MAKOSA YA NYUMA
Kuna watu kwa sababu tu alishafanya kosa fulani katika maisha yake basi ndo atajihukumu hadi anaingia kaburini, Mimi nilifanya iki jamani labda ndo sababu n.k hata mungu husamehe na kupotezea makosa. Wewe sio mkosaji Kama Farao hupaswi kujilaumu kwa makosa uliyofanya yakakupelekea kufeli.

3.KUACHA KUJIDHARAU
Ukijidharau wewe mwenyewe nani atakaekuamini? Hayupo jikubali na usijishushe. Jiamini katika unachokifanya wewe sio wakuwa chini siku zote.

4.KUKAA KWA MUDA MREFU BILA KUFANYA MAAMUZI
Kwanini ukae ukiwazia zaidi eti bado nafikiria niamue nini , unakaa miezi sita yote hujafanya maamuzi wewe una hatari kubwa Kama hela yenyewe utakuwa ushaitumia na bado hujafanya kitu chochote kwa sababu ulikuwa unangoja ufikirie . Ndio tunatakiwa kufikiria kwa umakini lakini sio kwa kukaa mda mrefu hadi unasahau unafikiria nini. Utamkuta mtu anapesa utasikia hapa najishauri nifanye biashara gani basi hadi mwakani bado anajishauri tu.

5.KUTAKA KILA KITU UWE SAHIHI
Hakuna mkamilifu, Sasa wewe unajitahidi kabisa kukwepa upungufu Yani ukishaona Jambo umekosea basi unaacha unahisi halikufai. Mara nyingi watu wa aina hii wanaanza Jambo na wakikutana na changamoto kidogo tu wanaacha na kuhamia kufanya kitu kingine. Hauwezi kukamilika kwa Kila jambo lakini haimaanishi uzembee kwa makusudi.

6.KUACHA TABIA YA KUGHAIRISHA MAMBO MUHIMU
Kila Jambo unalopanga unaghairisha tu nitaanza mwakani nitaanza kuwa serious tarehe moja wewe endelea kughairisha tu muda haukusubiri utabaki Kuona wenzako wanaofanikiwa ni Freemasons kumbe wewe haukufanya maamuzi mapema, ulighairisha mambo mengi Sana na kusema utaanza badae,kesho, mwezi ujao, mwakani, n.k

7.KUACHA VISINGIZIO
Watu hawaishiwi na sababu, Mimi Sina elimu, Sina kipaji, Sina mtaji, Sina pesa, Sina mda, Sina connection, n.k siku tu utakayoacha visingizio basi njia za mafanikio zitafunguka. Maana unajitengenezea mazingira ya kufeli wewe mwenyewe kwa visingizio vyako hivyo unavyojitengenezea

8.KUKIMBIA MATATIZO
Matatizo jamani yapo tu Kila siku ukipatwa na changamoto usiikimbie kabiliana nayo, Kama ambavyo leo hii utadondosha bunda la pesa chooni likawa linaelea kwenye sink pale juu utalitoa utalipangusa na kuendelea na maisha basi hivo hivo ndo ufanye kwa changamoto nyingine. Nikichkua penseli nzuri ya HB nikiwaita watu nikauliza nani anaitaka Kila mtu ataitaka lakini nikiamua kuivunja Kati kwa Kati nikauliza tena nani anaitaka watu wengi wataghairi lakini mjanja ni yule atakae chukua hivyo hivyo ataichonga na kuitumia tena. Hivyo basi mafanikio yapo katika changamoto. Shida yetu tunazikimbia changamoto nyingi ndo mana hatufanikiwi.

9.USIACHE KUTUMIA KIDOGO ULICHONACHO
Kuna watu wanasubiri mpaka awe na elimu kubwa au awe na pesa nyingi ndo aje afanye jambo, utakesha jaman ukisubiria ukubwa. Mimi binafsi Sina elimu kubwa kuwazidi wasomaji wa blog yangu wala Sina hata Diploma wala degree lakini najiamini na najikubali na elimu yangu hii hii ya sekondari nitafanikiwa tu. kwanini ungojee hadi uwe na diploma? degree? masters? PHD? Kwanini ungoje upate hela yote ndo uanze?? Anza sasa

10.KUKAA BILA KUFANYA CHOCHOTE
Kuna watu wamesoma hawajapata ajira na wengine hawakusoma hawana ajira basi Kila siku watashinda tu vijiweni na kwenye magenge ya umbea wakilalamika tu ah! Maisha magumu Sana siku izi nipo nipo tu Sina mishe yoyote yani,Kama ukipata mishe nistue ivi kweli mtu akuhangaikie kukutafutia mishe wewe zaidi ya ambavyo ungejitafutia mwenyewe?? Usikae tu kwa kubweteka pika basi hata karanga mda mnapiga story uuze na sio kukaa tu bila kufanya jambo lolote

Kama umependeza somo langu la leo weka comment hapo chini au Kama unaswali nitakujibu punde.

KARIBU TENA

Comments

  1. Replies
    1. Karibu Sana Mr.Yoherny nipo kwa ajili yenu

      Delete
    2. Jambo jema, ni mazuri tunayapata kutoka kwako mtaalamu.......
      International Admin mtu mzito kutoka India na Nyonyoma wake wa mchongo πŸ™ŒπŸ™Œ

      Delete
    3. πŸ˜‚πŸ˜‚ shukran Sana umeamua kunifurahisha

      Delete
  2. My sister you make me feel strong coz of what you ever post stay blessed and continue to teach me love you alot

    ReplyDelete
    Replies
    1. Thanks a lot dear, let's learn. From each other
      I love you more

      Delete

Post a Comment

Popular posts from this blog

VITU VYA KUFANYA KARIBIA NA MITIHANI.

CHEKA WITH INTERNATIONAL ADMIN

JINSI YA KUANDAA VIUNGO VYA PILAU VYENYE HARUFU NZURI.