ZIJUE FAIDA ZA MITANDAO
Huwezi kuona faida za mitandao Kama yenyewe ndio chanzo kikubwa Cha kukumalizia bando. Unaweza kutumia mitandao Kama ifuatavyo
KUJIPATIA ELIMU.
Watu wengi wanaingia YouTube , Facebook, Instagram, Google, Twitter, n.k kupata elimu za vitu mbalimbali Kama vile taaluma, mapishi, mavazi, biashara, mahusiano,kushona, ubunifu, teknolojia n.k
CHANZO CHA KIPATO
wanatumia mitandao Kama Facebook, YouTube, Instagram, Twitter, na michezo mbalimbali mtandaoni kujipatia kipato. Ukiwekeza katika mtandao utaona matunda yake yapo inahitaji uvumilivu kidogo.
KURAHISISHA MAWASILIANO
Leo hii mtu aliyoko China anaweza kuwasiliana na mtu aliyoko Tanzania moja kwa moja ndani ya muda mfupi. Watu hufikisha taarifa kwa watu wengi walengwa ndani ya muda mfupi kupitia makundi mbalimbali ya mitandaoni Kama makundi ya WhatsApp na Facebook.
BURUDANI
Kila aina ya burudani utakayoihitaji ipo mtandaoni, wewe Kama ni mpenda mziki, tamthilia, katuni, vichekesho, kusoma vitabu n.k basi utayakuta yote hayo mitandaoni
BIASHARA
Watu wengi hufanya biashara mitandaoni na hujipatia wateja wengi kupitia mitandao, tunaona wajasiriamali wengi, wafanya biashara wakubwa kwa wadogo, madalali wote wakifanya biashara mitandaoni na wanajiingizia kipato
KUENDELEZA MAHUSIANO
Zamani ilikuwa tabu Sana kwa wapenzi kuwasiliana endapo wapo mbalimbali ilichukua muda Sana mpaka kutuma barua aghalabu mahusiano kuvunjika. Lakini siku hizi watu hata wakawa mbali wanaweza kuwasiliana Kama wako karibu
Kama umependeza somo langu la leo weka comment hapo chini au Kama unaswali nitakujibu punde.
SHUKRANI ,,Mungu akubariki
ReplyDeleteAmiin
DeleteUbarikiwe pia
Shukrani sana ubarikiwe
ReplyDeleteAmiin
DeleteKaribu
Very nice 👍👍👍
DeleteThanks dear be blessed
DeleteCongratulations admin
ReplyDeleteThanks a lot
DeleteBe blessed
ReplyDeleteAmiin
DeleteThe same to you
Goo job
ReplyDelete