LIFE STAR


International Admin

Maisha ni Kama nyota unayoiona juu angani ili ufurahie maisha inabidi uwe na pembe tano Kama nyota. Utaweza kuyafurahia maisha yako kwa amani na raha kama utazingatia pembe tano zifuatazo za maisha yako.
1. MUNGU
Haimaanishi Sasa uanze kukesha msikitini/kanisani ndo utakuwa karibu na mungu bali mshirikishe mungu katika chochote unachofanya maana hata mchawi humuomba mungu "eh mwenyezi mungu nijaalie nifanikiwe kumroga fulani" mda mwingine mambo yetu hayaendi kwa sababu hatumtegemei mwenyezi mungu. Kama mwenyezi mungu anasaidia waja wake wa aina zote wachamungu, washirikina, wahalifu. Iweje ashindwe kukusaidia pale utakapo muomba? Tumtegemee mwenyezi mungu kwa kila kitu tunachokifanya.

2. PESA
Utashindwa kufanya chochote unachokitaka kukifanya kama hauna pesa, badala yake utaishia kutamani tu " dah! natamani ningekuwa na hela ningesaidia familia yangu, ningesaidia masikini, ningefanya...n.k." (hauwezi kutoa kile usichokuwa nacho-- amka tafuta pesa). Sio kosa lako kuzaliwa katika familia ya kimaskini, ila ni kosa lako kuendelea kuuishi umaskini na kufa masikini kwa sababu maisha yako una fursa kubwa mkononi kwako kuyatengeneza.
Umuhimu wa pesa
✓ uwezo wa kununua unachokitaka na sio unachokipata Hapa nitatoa mfano wa mtu mwenye pesa akienda sehemu ya kula ataagiza kile achajisikia kula bila wasiwasi. Lakini kwa yule mwenye pesa kichele ataagiza menyu kwanza ili aangalie chakula gani ataweza kukimudu kulingana na mfuko wake.
✓ uhuru wa kusaidia wengine Kama nilivyosema awali huwezi kutoa kile usichokuwa nacho.

3. UJUZI
Wenye kuingiza pesa ni wale wenye ujuzi wa jambo fulani tu haijalishi una ujuzi gani ila utumie kuwa pesa. inawezekana wewe ukawa unajua kushona, kujenga, kuremba, kupamba maharusi, Mwalim,daktari,injinia, unaweza kupika chips, vitumbua, maandazi,n.k huo ndo ujuzi wako utakaokuingizia pesa komaa nao.Na usichoke kuongeza ujuzi sio kwamba wewe ni mpishi wa cake tu basi ukaridhika nao, Jifunze kushona, kupodoa, kuchora, n.k ila muhimu ni kwamba usichoke kuongeza maarifa uliyo nayo maana hata mwenye degree analipwa zaidi ya mwenye diploma

4. AFYA.
Tunakumbukaga mambo yote lakini tunasahau jambo la msingi Kama huna afya ni mgonjwa utashindwa hata kuubadilisha ujuzi wako kuwa pesa maana itakupasa ushinde hospital au nyumbani ukihudumiwa. Na ukifanya masihara hata ukiwa na pesa utaishia kukaa kitandan tu na kuwaita watu wakatoe pesa kweny ATM za matibabu yako na hutofurahia pesa zako. Tunakunywa pombe kupita kiasi, sigara, uzinifu,hatuchukui tahadhari za magonjwa Kama malaria, UTI, typhoid n.k halafu tunapoteza mda, pesa na nguvu nyingi kuhangaika na kujitibu badala tungejikita kwenye kusaka pesa zaidi.kuna magonjwa unakuta yamekupata tu mungu amekupangia na mengine tunaendaga kujitafutia. Ebu chukuria upo hoi kitandani unaumwa halafu unapigiwa simu twende sehem fulani Kuna dili la pesa ndefu leo
tayari utakuwa ushaikosa kwahiyo tujari afya zetu Kama unatakiwa kula wewe Kula , Kama kulala hakikisha unalala vizuri, n.k

5. MTANDAO MZURI UNAOKUZUNGUKA
Sasa hivi unatakiwa uwe na mtandao wa watu ambao unaweza kupanga Jambo lako wakakusapoti , inaweza kua familia yako, marafiki zako, wafanyakazi wenzako, wanafunzi wenzako,n.k lakini nasisitiza Sana kujenga mahusiano mazuri na familia yako hata Kama uwezo wa kukusapoti kifedha hawana basi hata kwa mawazo watakusaidia na kukuombea dua . Mtandao wawatu ndo utakusaidia wewe kupata wepesi katika mambo mengi unayoyafanya hakikisha watu wanaokuzunguka wana uwezo wakukusaidia kwa namna moja ama nyingine na Kama hauna tafuta . Kwa lugha ya kingereza wanaita connection
"Hauwezi kuendelea Kama kila siku unakutana na watu wale wale tu katika maisha yako"

Kama umependeza somo langu la leo weka comment hapo chini au Kama unaswali nitakujibu punde.

KARIBU TENA

Comments

  1. Umeupiga mwingiiiii sana International Admin, sema nini! You have something to approach my mind sema una masiala mengi 🀣🀣🀣

    ReplyDelete
    Replies
    1. Thanks a lot dear
      I have a lot to the society but being funny is just because I'm comedian too

      Delete
  2. Jadi umejtahd sema kasomee uandish wa habar tuu

    ..

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ahsante Sana
      Siwezi kuachana na Cyber Security nataka nilinde media zangu from hackers n.k

      Delete

Post a Comment

Popular posts from this blog

VITU VYA KUFANYA KARIBIA NA MITIHANI.

CHEKA WITH INTERNATIONAL ADMIN

JINSI YA KUANDAA VIUNGO VYA PILAU VYENYE HARUFU NZURI.