NAMNA YA KUWEKA BAJETI

50% ya kipato chako iweke kwa ajili ya matumizi yako ya Kila siku Kama chakula, mavazi, umeme, Kodi, maji n.k Watu wengi huwa wanajipunja Sana hapa na ndo mana unaishi kwa kujitesa. Kama unaingiza 1M basi laki tano itenge kwa ajili ya hayo mahitaji muhimu ya mara kwa mara Kama vile chakula, umeme, Kodi, nauli na mavazi. Watu wengi wakipata fedha wanaweka akiba yote na kusahau kuwa Kuna vitu wanavihitaji kila siku, si ajabu kukuta mtu ameweka akiba na bado amekopa madeni mengi tu kwa ajili ya chakula. Hapa utawasikikia watu mimi siwezi kuweka akiba bwana , kila nikiweka naila! wanasahau kwamba hutakiwi kuweka pesa yote unayoipata kama akiba kwa sababu itakushinda tu, utahitaji kula utaanza kula akiba. Tunatafuta pesa ili tujikimu kimaisha na sio kujitesa kimaisha. Lakini kumbuka kuweka nusu tu ya kipato chako kwenye mahitaji muhimu

30% ya kipato chako itenge kwa ajili ya matakwa yako (your wants) mfano: unataka kununua gari, unataka kutoka out, unataka kumfanyia mtu surprise, unataka kumiliki aina flani ya simu,n.k

20% kwa ajili ya uwekezaji, kuweka akiba na kulipa madeni. Usiyaache tu madeni ivi ivi hakuna siku utapata hela maalumu kwa ajili ya kulipa madeni, kufanya uwekezaji na kuweka akiba. Wanasema haba na haba hujaza kibaba. The more you decrease your want the more you increase your investment (Kadiri unavopunguza matakwa yako ndo unavoongeza uwekezaji wako) Akili kichwani mwako

Kama umependezwa na somo langu la leo weka comment hapo chini au Kama unaswali nitakujibu punde.

KARIBU TENA

Comments

Post a Comment

Popular posts from this blog

JINSI YA KUTENGENEZA TAMBI NZURI ZA DENGU

JINSI YA KUANDAA VIUNGO VYA PILAU VYENYE HARUFU NZURI.

JINSI YA KUPIKA MAKANGE YA SAMAKI