HASARA ZA MITANDAO
Hakuna chenye faida kikakosa hasara. Mitandao ina hasara zake nyingi hivyo Kila mtu inampasa kuziangalia kwa jicho la tatu.
KUINGILIA FARAGHA
Kupitia mitandao watu wanaingilia faragha za watu kwa kuchukua au kutizama taarifa zako bila idhini yako. Kwa jina la kitaalam wanaitwa Hackers, lakini pia mtu anaweza akarusha maudhui ya faragha ambayo yanaingilia faragha ya mtu kwa jina la kimtaani wanaita Connection . Napenda nikushauri kutoweka taarifa zako binafsi kwenye mitandao ya kijamii maana ni faragha yako.watu wengi hawajui kuwa hata mwaka na tarehe ya kuzaliwa ni faragha.
UDANGANYIFU NA UTAPELI
Watu wengi wamelia mitandaoni watu wanatangaza biashara unaipenda unalipia hupati bidhaa. Wengine wanajifanya wako nje ya nchi wanaleta bidhaa kwa bei rahisi mfano anaweza kuigiza yeye ni mhindi kumbe ni mtanzania yuko Buza amekaa anaandaa matangazo ya kutapeli watu. Lakini hata matumizi ya application mbalimbali Kama vile Snapchat n.k zinafanya watu waonekane watofauti kuliko uhalisia. Siku hizi ukiingia mitandaoni unaweza kujihisi peke yako ndo una muonekano mbaya lakini ni utapeli tu na udanganyifu wa mitandao. Wengine wanatengeneza website na kujifanya wao ni makampuni mbalimbali, kwahiyo kuwa makini na Kila unachokiona mitandaoni.
KUPUNGUA NGUVU KAZI NA UFANISI
Watu wengi tumekuwa tukitumia muda mwingi kupita kupita kwenye mitandao tukitafuta udaku, michezo, n.k hii imefanya watu wengi kufanya vitu kwa uwezo wa chini maana anafanya Jambo huku yuko na simu anashangaa Facebook, Instagram, Twitter, WhatsApp n.k imefikia hatua mtu simu yake imekuwa sehemu ya mwili akiiacha kidogo tu hana amani. Mitandao ni mizuri lakini tuitumie kwa viwango na tuwe na mipaka katika maisha yetu ya Kila siku
MMOMONYOKO WA MAADILI
Vijana wengi wamekuwa wakiharibikiwa kutokana na kuiga maisha ya watu wengine pamoja na wasanii wanayoyaona huko mitandaoni. Haikatazwi kumuiga mtu Ila watu wengi wanaiga maadili yasiyofaa katika jamii.
HABARI ZA UONGO
Kwa sababu Kila mtu ana Uhuru wa kutuma maudhui mitandaoni basi watu wengi wamekuwa wakitengeneza habari zao za uongo na kuzituma mitandaoni. Hii inaleta mtafaruku kidogo katika jamii hivyo basi hakikisha taarifa unazozichukua na kuzisambaza kutoka mitandaoni zitoke kwenye vyanzo vyenye kuaminika.
Kama umependeza somo langu la leo weka comment hapo chini au Kama unaswali nitakujibu punde.
Comments
Post a Comment