CHEKA WITH INTERNATIONAL ADMIN

VIDEO ZA VICHEKESHO
NGUMI ZA KIMATAIFA πŸ˜‚ MTOTO WA KITANGA πŸ˜‚ UKOME KULA KWA WATU πŸ˜‚ VITUKO VYA PUNGASESEπŸ˜‚ HUYU JAMAA NOMA SANA πŸ˜‚ KUMBE WAKINA HANSCANA WANAPATA SHIDA HAWASEMI πŸ˜‚ UTAPENDA NGUMI ZA WAPENDANAO πŸ˜‚ UTAPENDA BARAKOA ZA WAPENDA KULA πŸ˜‚ SARAKASI ZA MASHA LOVE πŸ˜‚ kILICHOMKUTA JINI LA BUZA NJOO NIKUAGE πŸ˜‚πŸ˜‚ MIMI SI WAKO πŸ˜‚ WAPEMBA NOMAπŸ˜‚ BINTI ANAVOONESHA JEURI YA BOOM UNAUNGUZA KUKU?? πŸ˜‚ SaBINA πŸ˜‚ MAPAMBIO YANANOGA πŸ˜‚ SALAMA KAIKUBALI πŸ˜‚ GOOOOO! πŸ˜‚ UTAPENDA KIBONGE ANAVOCHEZA πŸ˜‚ HUYU DOGO ANABALAA πŸ˜‚πŸ˜‚ DOGO ANAJUA πŸ˜‚ HASIRA ZA KIHEHE πŸ˜‚ HII MICHEZO HII πŸ˜‚ HII ENGLISH πŸ˜‚ KUMBE NDO MAMBO YENU MKIWA GYM πŸ˜‚ 20. πŸ˜‚πŸ˜‚ HIZI MOVIE ZA WAHINDI SITAKI TENA πŸ˜‚ BABA JUMA NA MTIHANI WA HESABU
Baba juma alikaa kwa kutulia sebuleni akisoma gazeti mara ghafla mwanae juma anakuja na mtihani wa hesabu umeandikwa sifuri. Bila kuchelewesha akaanza kumpiga ngumi na mateke
Baba Juma: Pumbavu mkubwa wewe unakuwa Kama jini mauno, yani Mimi natoa fedha zangu ndo unapata sifuri!! Enzi zangu niko chuo kikuu UDOM napata A kama zote Hizi akili za mama ako hizi kwetu hakuna
Basi akaendelea kumpiga mtoto vibaya Sana huku akimlaumu, mara mke wake akaingia Mke:We baba Juma! baba Juma! Muache mtoto utamuua huyo, huo mtihani wako huo tumeutoa kwenye kabati 🀣🀣

BINTI WA FORM FOUR AKATALIWA KWENDA TUTION
Binti mmoja wa shule fulani ivi akiwa ametupia na begi lake mgongoni akiwa anatoka anamkuta baba yake sebuleni
Baba: Haya kumekucha tena, unaenda wapi?
Binti:Leo tumeambiwa twende tution mwalim anakuja kufundisha logarithm
Baba:Hakuna kwenda leo, rudi ndani
Binti:(huku akilalamika) Sasa mwalimu katuambia tusikose na inatoka kwenye practical ya NECTA
Baba:(Akamchapa kibao cha nguvu) Puumbavu! Mama ako mwenyewe alikuwa anaaga ivo ivo anaenda twisheni kumbe anakuja kwangu! RUDI NDANI 🀣🀣

INTERVIEW YA MAMA WA KUSINI
Mtangazaji:Habari ya wakati mama, naona umetokelezea ile mbaya uko live ndani ya Jadizo TV watanzania wanataka kuskia, Eti Kati ya Kondeboy na Harmonize unamkubali Nani?
Mama:Mimi namkubali Kondeboy, Kwanza haringi, anasaidia watoto na wamama Kila mtu anampenda . Huyo Harmonize simkubali wala nini nikimuona Buushit 🀣🀣

BABA ASIYEJUA KIZUNGU
Kijana wa Buza alikaa barazani na baba yake wakizungumza Mara Paap! Pisi ya kijana inakuja pale. Kijana akaona Wala isiwe tabu.
Kijana: Habari yako Monica, ndo umefata kile kitabu chako Cha speak English my father can not understand
Monica: Ndio, nipe na kile Cha where we are going to meet
Kijana: where we can meet Sina nimebakiwa na We can meet under mango tree
Monica: Sawa basi uje na daftari la summary la don't come late
Baba: Heee inaonekana binti unapenda Sana kusoma vitabu vyote hivyo
Kijana: Eeeh baba, huyu ndo kipanga wetu wa shule mitihani yote anatuongezea
Baba: Alaa kumbe basi hongera Sana, kamuongezee na kile Cha I understand all your stupid you're talking about 🀣🀣

BIBI KIZEE AMTOA NDUKI MWIZI
Kutana na Bibi aliyechangamka kutoka mbagala alikuwa anapita uchochoni kibaka akamvamia akampiga mtama wa nguvu akampora simu na pochi akaanza kukimbia. Bibi akaanza kumkimbiza huku anaita kelele za Mwizi Kibaka akaona isiwe tabu ebu nimdondoshee pochi lake labda atarudi, wapi Bibi yumo. Kibaka akakimbia akaona ngoja nimdondoshee na simu yake, bibi akaiokota akaendelea kumkimbiza Kibaka: We bibi unataka nini (huku akihema) pochi lako nimekupa! Simu yako nimekupa! Unanidai nini tena?
Bibi:Nyoo! Na ule mtaja je?? 🀣🀣

SAFARI YANGU YA KIMARA KWA BONYOKWA
Siku hiyo nimependeza mwenyewe nimetulia ndani ya daladala mara konda katika kukusanya nauli akaniruka, nikamnyooshea TSH.400/= akaipita nadhani hakuiona. Basi we ikafika mwisho wa gari nashuka nikaona ngoja nimpe konda hela yake,
Mimi: Konda umesahau nauli yako hii Konda:Sijasahau na nilikuwa nakusubiria kwa hamu ulivyopendeza uondoke na nauli yangu nikukimbize 🀣🀣

MWANAFUNZI WA CHUO BAADA YA KUMALIZA BOOM
Mwanafunzi wa chuo fulani ivi baada ya kumaliza boom akaamua ampigia baba ake simu Mwanafunzi: Baba pesa imeisha hali nimbaya watu wanajiua tu huku na Mimi nitajiua baada ya kukosa pesa
Baba:Huku hali ni tete mwanangu Sina la kufanya zaidi ya kukutakia R.I.P na mungu akulaze mahali salama 🀣🀣

MUHIMU
Nitakuwa niki post vichekesho na masimulizi hapa mara kwa mara usikae mbali nakukumbusha kutembelea blog mara kwa mara.

Kama umependeza somo langu la leo weka comment hapo chini au Kama unaswali nitakujibu punde.

KARIBU TENA

Comments

Post a Comment

Popular posts from this blog

VITU VYA KUFANYA KARIBIA NA MITIHANI.

JINSI YA KUANDAA VIUNGO VYA PILAU VYENYE HARUFU NZURI.