Posts

VITU VYA KUFANYA KARIBIA NA MITIHANI.

Image
Karibu sana,basi leo tuko na namna ya kujiandaa wakati wa kukaribia mitihani ili uweze kufanya vizuri. 1. ACHA UOGA Kuna watu wanaogopa Sana wakikaribia kufanya mitihani na hii hali hupelekea kokosa hali ya kutojiamini na kusoma kwa ku panic. 2. JUA MADA ZOTE ZA KILA SOMO UNALOSOMA. Kuna watu wanaingia kwenye mtihani bila kujua hilo somo Lina mada zipi. Hatakama ukashindwa kujua moja kwa moja kila mada lakini kwa uchache ujue mada inahusu nini. 3. SOMA KWA LENGO (TARGET) Tumia muda mwingi kusoma kile unachokielewa kuliko kukimbiza Kurasa /Slides hata Kama hauelewi. Hii itakufanya ushindwe kujiamini ukiingia katika mtihani kwani kila utakachokutana nacho utakuwa hukijui vizuri unajua juu juu tu. Lakini ukiingia na kitu ambacho umekielewa vizuri ukikutana nacho utakijibu kwa weledi na kukupa hamasa ya kujibu maswali mengine vizuri. 4. SOMA MITIHANI ILIYOPITA (Past Papers) Kusoma mitihani iliyopita hii itakusaidia kukupa muongozo wa maswali yanavokuwa lakini pia

VIGEZO VYA KULIPWA YOUTUBE

Image
Karibu sana katika blog yangu Leo naenda kukuletea vigezo vya kulipwa YouTube. Kwanza kabisa mtu yeyote anaweza kumiliki account ya YOUTUBE na akalipwa. Kitendo Cha wewe kuwa na account ya email ya Google (Gmail) tayari inakufanya uwe na YouTube account. YouTube ni mtandao ambao unazidi kushika Kasi na kuingizia kipato watu wengi kila siku. Una uwezo wa kuweka videos zako watu wakaangalia na ukalipwa pia. VITU VYA KUWA NAVYO WAKATI WA KUFUNGUA ACCOUNT YA YOUTUBE 1. Fungua Gmail account katika simu yako. JINSI YA KUFUNGUA GMAIL ACCOUNT ✓ Ingia Google ✓ Andika Gmail sign up ✓ Utaletewa form ya kujaza taarifa zako binafsi ✓ Kisha utakubaliana na masharti ya Gmail kwa kubonyeza kitufe kilichoandikwa Agree baada ya kujaza form yako ✓ Tayari utakuwa na Google account (Gmail) 2. Baada ya kuwa na account ya Google utaingia youtube uta click kwenye icon ya juu kabisa upande wa kulia itakayokuwa inawakilisha Gmail account yako. 3. Utaenda katika my channel 4. Ut

JINSI YA KUJITENGENEZEA JINA (BRAND) KUPITIA MITANDAO

Image
Kwanza, unatakiwa ujitambue wewe ni Nani na unafanya nini mitandaoni Kisha uje uyafanye yafuatayo: 1. WEKA PROFILE PICTURE (DP) . Watu wengi wanaweka picha za katuni, midoli, maua, wananyama, logo, au picha za watu wengine. Hakuna mtu ambae anavutiwa na vikatuni nakadhalika. Unachotakiwa kufanya ni kuweka professional photo. Professional photo haipigwi mwili mzima, Wala watu hawaweki mapozi. Unaweza kuangalia hapa chini mfano wa professional photo na itapendeza Kama utaipiga na simu au kamera yenye quality. Professional photo huanza kuvuta makini ya mtu na kukufanya uonekane uko makini (serious) na unachokifanya. 2. WEKA ACCOUNT YAKO PUBLIC Kuna watu account zao wanaziweka private Sana Sana Instagram. Kama unataka kufanya biashara au watu wajue unachokifanya usiweke account yako private. Weka Public kila mmoja aweze kuona unachokifanya. 3. TENGENEZA WAFUASI WENYE THAMANI (VALUABLE FOLLOWERS). Kuna watu wanatabia ya ku follow watu hovyohovyo kwa lengo la kujipatia follower

JINSI YA KUTENGENEZA MANGO PICKLE (CHACHANDU YA EMBE) NYUMBANI

Image
Karibu tena katika darasa letu la mapishi basi leo naenda kukuletea namna ya kuandaa achari ya embe nyumbani unaweza kula kwa ugali au chochote ukipendacho. MAHITAJI. ✓Maembe mabichi (usitumie embe zilizoiva au zilizoanza kuiva) ✓ Pilipili mbichi (kama ukipenda) ✓ Achari masala ✓Masala ya kuwasha ✓ Mafuta ya kupikia ✓ Binzari ya njano (tumeric powder) ✓ Chumvi kiasi. MATAYARISHO. ✓ Osha vizuri embe zako na uzikate Kate saizi uipendayo lakini usimenye maganga (Kata vikonyo cha juu na chini) ✓ Loweka embe zako weka na chumvi kwa muda wa siku mbili au tatu Kisha utazianika kwa siku moja au mbili. (Angalia zisikauke Sana zitaleta ugumu wakati wa kula) ✓ Weka mafuta jikoni mpaka yapate moto Kisha yatoe yaweke pembeni yapoe yawe Kama ulivyoyatoa dukani. ✓Chukua chombo chenye nafasi ya kutosha changanya vitu vyote pamoja na mafuta mpaka vichanganyike vizuri ✓ Kisha anika mchanganyiko wako kwa siku kadhaa ili uive vizuri na hapo utakuwa tayari kwa matumizi

JINSI YA KUPIKA BIRIANI TAMU YA KUKU

Image
Kaributena katika darasa letu la mapishi basi leo naenda kukuletea namna ya kuandaa biriani nzuri ya kuku. MAHITAJI kuku 1kg Mchele wa basmati/ wakawaida (Hapa nitatumia nusu) Vitunguu maji 1/4 Nyanya zilizosagwa tano Nyanya ya mkebe Vitunguu saumu punje 10 Pilipili za kijani 4 Mafuta 1/4 Mdalasini vijiti 5 Hiliki punje 10 Tangawizi vijiko 2 vya chakula Majani ya nanaa yaliyokatwa kibakuli kidogo 1 Binzari nyembamba kijiko 1 cha chai Chumvi kijiko 1 cha chai Manjano 1/2 kijiko cha chai Zafarani 1/2 kijiko cha chai Kotmiri iliyokatwa 1/4 kikombe Maziwa ya mtindi kikombe 1 Njegere (ukipenda) JINSI YA KUANDAA Loweka mchele w kwa dakika 15 hadi 30 Weka mafuta kwenye sifuria, yakishapata moto kaanga vitunguu maji hadi viwe na rangi ya brown kisha chota vitunguu robotatu ya ulivyovikaangaweka pembeni vingine vibaki kwenye sufuria. Twanga kwa pamoja binzari nyembamba, kitunguu swaumu, tangawizi, nusu ya pilipili na vijiti vya mdalasini, kisha weka robo tatu ya vit

PILAU TAMU YA NYAMA.

Image
NAFASI ZA SENSA 2022 www.tamisemi.go.tz JIANDAE KUHESABIWA Karibu tena, basi leo International Admin anakuletea namna ya kupika pilau tamu ya nyama. Usiondoke angalia mwanzo mwisho, enjoy! MAHITAJI ✓ Mchele (unaweza kuwa basmati au wakawaida) ✓ Nyama (mbuzi au ng'ombe) ✓ Viazi mbatata kiasi ✓ Unga wa pilau (nimeelekeza katika post ya nyuma hapo namna ya kuandaa) ✓ Chumvi kiasi ✓ Mafuta kiasi ✓ Vitunguu maji vitatu kitunguu swaum kilichopondwa ✓Binzari nyembamba (uzile) uloweke kwenye maji kidogo. . NAMNA YA KUPIKA 1. Chemsha nyama yako mpaka iive itie na chumvi kiasi (Supu iweke pembeni) 2. Kaanga viazi mbatata na viive (visiwe brown) Kisha vitoe vikiwa bado na rangi nyeupe. (Wengine hawakaangi, ila ukikaanga mbatata zako zitakuwa na ladha nzuri zaidi) 3. Kaanga vitunguu maji mpaka viwe brown (angalia visiungue vitabadili ladha ya chakula) 4. Weka mdalasini kaanga pamoja, Kisha weka uzile na hiliki na unga wa pilau kidogo Kish

JINSI YA KUANDAA VIUNGO VYA PILAU VYENYE HARUFU NZURI.

Image
NAFASI ZA SENSA 2022 www.tamisemi.go.tz JIANDAE KUHESABIWA Karibu kwa mara nyingine ukiwa na International Admin leo nitaenda kukuonesha namna ya kuandaa viungo vya pilau vyenye harufu. Ni rahisi sana, enjoy! MAHITAJI ✓ Mdalasini mzima vijiti vikubwa vitano ✓ Binzari nyembamba kibakuli kidogo kimoja ✓Karafuu kibakuli kidogo kimoja ✓ Pilipili manga kibakuli kidogo kimoja ✓ Hiliki nzima kibakuli kidogo kimoja ✓ Uwatu kibakuli kidogo kimoja ✓Mustard seed kibakuli kidogo kimoja MATAYARISHO 1. Chukua frying pan weka jikoni weka na viungo vyako vyote Kisha koroga kidogo kidogo ili usiviunguze (Moto uwe wa kiasi visiungue) 2. Ukimaliza ipua na viache vipoe 3. Chukua blender ya kusagia viungo na uvisage Kisha vitakuwa tayari kutumiwa (Kama hauna blender chukua kinu kidogo na mchi na uviponde ponde Kisha chekecha kwa kichujio Cha chai, japo itakuchukua mda kidogo) Kama umependezwa na pishi langu la leo weka comment hapo chini au Kama unaswal