Posts

Showing posts from June, 2022

JINSI YA KUPIKA MAKANGE YA SAMAKI

Image
Kaributena katika blog yangu uko na International Admin leo naenda kukuletea pishi la Makange ya samaki. Makange ni kati ya mboga rahisi sana kupika na utashangaa kujua kuwa huenda ulikuwa unajichelewesha kuandaa mboga hiyo nyumbani kwako kwa kuogopa vile unayakuta katika hoteli kubwa nyingi na yanavyowekwa kwenye sahani. Huenda umetamani kupika mboga ya makange kwa muda mrefu lakini ukadhani kwa namna ulivyowahi kuiona kwenye sahani, siyo mboga rahisi kupika. TUANZE MAHITAJI ✓ Kitunguu kimoja ✓ Nyanya kubwa 3 ✓ Karoti moja ✓ Hoho moja ✓ Ndimu moja ✓Kitunguu saumu na tangawizi iliyosagwa kijiko kimoja (vyote kwa pamoja) ✓ Tomato fresh 2 ✓ Chumvi kiasi ✓ Binzari nyembamba na pilipili manga ya unga kijiko kimoja cha chakula ✓ Curry powder kijiko kimoja cha chakula ✓ Binzari ya mchuzi kijiko kimoja cha chai ✓ Soya sauce ya kukoza vijiko 3 vya chakula ✓ Maji robo kikombe ✓ Mafuta ya kupikia vijiko 3-4 ✓ Spice ya samaki kijiko 1 Cha chakula ✓ Samaki mkubwa mmo

HISTORIA YA SAMIA SULUHU HASSAN

Image
Samia Suluhu Hassan alizaliwa mnamo tarehe 27/01/1960 katika visiwa vya Zanzibar. Alianza elimu ya msingi mnamo 1966-1972 katika shule tofauti tofauti zilizopo Unguja na Pemba yaani Zanzibar. Alianza katika shule ya CHAWAKA (Unguja), Kisha alihamia katika shule ya msingi ZIWANI (Pemba) na alimaliza katika shule ya msingi ya Mahonda. Elimu yake ya sekondari alianza 1973-1976 .Alisoma katika shule mbili, 1973-1975 alisoma katika shule ya sekondari ya Ngambo (Unguja) Kisha mwaka 1976 alihamia shule ya Lumumba (Unguja) ambapo alihitimu elimu ya sekondari. Hakuendelea tena na masomo ya chuo kwa muda huo. Aliajiriwa katika serikali ya Zanzibar Kama mchapishaji ambapo alipanda ngazi na kuwa Afisa mipango mnamo 1987-1988. Samia Suluhu Hassan alijiendeleza kielimu huku akiwa mtumishi wa serikali kwa kusoma kozi fupi mbalimbali Kama vile Sheti ya takwimu kabla ya kujiunga na Taasisi ya Maendeleo na uongozi ya Mzumbe Morogoro ambapo alifanikiwa kuhitimu stashahada ya juu ya utawala