Posts

Showing posts from June, 2023

JINSI YA KUPIKA MAANDAZI

Image
JINSI YA KUPIKA MAANDAZI LAINI. MAHITAJI YA MAANDAZI 1. Unga - 5 Vikombe. 2. Tui la Nazi zito vugu vugu - 1 ¼ kikombe. 3. Sukari - 3/4 kikombe cha chai. 4. Samli iliyoyayushwa au mafuta - 3 vijiko vya Supu. 5.Hamirah - 2 Vijiko vya Supu. 6. Hiliki - 1/2 Kijiko cha chai. 7. Mafuta ya kukaangia. NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA. 1. Ndani ya kibakuli kidogo, mimina hamira na na vijiko viwili vya kulia vya tui. Weka kando mpaka hamira ianze kufura, kama dakika 5-10. 2. Pasha samli moto: 3. Ndani ya bakuli kubwa au sinia, changanya unga, sukari, iliki na samli ikiwa bado moto moto. 4. Mimina hamira ndani ya mchanganyiko wa unga. 5. Changanya na ukande huku ukitumia lile tui la nazi. Tui likipungua unaweza ukaongeza maziwa. 6. Kanda unga mpaka uwe laini. 7. Kata madonge *12 au 15 uyaweke kwenye baraza iliyonyunyiziwa unga na uyafunike ili yapate kufura na yasikauke. *Ukipenda maandazi manene fanya madonge 12. Ukipenda mepesi fanya madonge 15. 8. Madonge yakifura,

JINSI YA KUPIKA DAGAA WATAMU ZAIDI

Image
🥕🧅Jifunze Jinsi Ya Kupika roast la Dagaa mwanza Watamu 🥕🧅 🥕🧅 MAHITAJI 🥕🧅 1️⃣ Dagaa 2️⃣ Limao 3️⃣ Karoti 4️⃣ Bamia 5️⃣ Kituunguu Maji 6️⃣ Kitunguu Thoum 7️⃣ Pilipili Mbuzi 8️⃣ Pilipili Manga 9️⃣ Pilipili Boga 1️⃣0️⃣ Nyanya Maji 1️⃣1️⃣ Tomato Paste 🥕🧅 NAMNA 🥕🧅 1️⃣ Toa Vichwa Dagaa Wako 2️⃣ Chemsha Maji Yakichemka Yaipue 3️⃣ Weka Dagaa Kwenye Maji Ya Moto Kwa Dk20 Ili Uchafu Na Mawe Vitoweke 4️⃣ Waoshe Dagaa Vile Wewe Unataka Kama Na Sabuni, Maji Mara8 Ili Mradi Wawe Salama Kwa Utafunaji 5️⃣ Waweke Kwenye Nyungo/ungo Watawanye Waweke Juani Ili Wakauke Kupunguza Matumizi Ya Mafuta Kipindi Unawakaanga 6️⃣ Kipindi Dagaa Wapo Juani Andaa Viungo Vyako Kwa Usafi Na Kuvikata Kwa Mikato Upendayo 🔛 Bamia 🔛 Karoti 🔛 Pilipili Boga 🔛 Pilipili Manga 🔛 Kitunguu Maji 🔛 Kitunguu Thoum 7️⃣ Weka Sufuria Jikoni Tia Mafuta Ya Kula Weka Na Chumvi Kiasi Yakipata Moto Weka Dagaa Zako Kaanga, Wakianza Kuwa Na Rangi Ya Udhur